Posts

Showing posts from June, 2021

VIDEO: SIMBA YAITANGAZIA KIAMA YANGA, NABI AFUMUA KIKOSI KISA CHAMA

Image
KUELEKEA mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba v Yanga, Julai 3, Simba yaitangazia kiama Yanga, kisa Chama Nasreddine Nabi afumua kikosi ni ndani ya Krosi Dongo.   

ZIDANE ANAWEZA KUIBUKIA UFARANSA

Image
ZINEDINE Zidane aliyekuwa Kocha Mkuu wa Real Madrid imeelezwa kuwa huenda akawa Kocha Mkuu wa  Ufaransa. Timu ya taifa ya Ufaransa inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Deschamps amekiongoza kikosi hicho kuenguliwa kwenye hatua ya 16 bora ya Euro 2020. Ufaransa iliondolewa kwenye Euro 2020 kwa penalti 5-4 dhidi ya Uswisi baada ya dk 90 ubao kuwa 3-3. Timu hiyo ilikuwa inapewa nafasi ya kutwaa taji hilo lililokuwa mikononi mwa Ureno ambayo nayo pia ilitolewa.

SANCHO SASA NI MALI YA MANCHESTER UNITED

Image
 MANCHESTER United imekamilisha dili la usajili wa winga wa Borussia Dortmund kwa kanuni atajiunga na timu hiyo mara baada ya Euro 2020 kukamilika. Imechukua muda wa misimu miwili kwa United kujadili dili la Sancho na mabosi wake ila awali walikuwa wanavutana katika suala la dau ambalo walikuwa wanataka ilikuwa ni Euro milioni 100. Sancho ataibuka ndani ya Old Trafford baada ya kupewa dili la miaka mitano na atakuwa hapo mpaka 2026 inaelezwa kuwa amekamilisha kila kitu jambo pekee analosubiri ni kufanyiwa vipimo na sasa yupo katika majukumu ya timu ya Taifa ya England inayoshiriki Euro 2020. Kocha Mkuu wa Manchester United inayoshiriki Ligi Kuu England, Ole Gunnar Solskjaer inaelezwa kuwa anahitaji kufanya maboresho katika kikosi chake na usajili wake ni wa muda mrefu. Sancho atakuwa rasmi ni mali ya United pale atakapofanyiwa vipimo kwa mujibu wa ripoti.

VIDEO: HAJI MANARA AWEKA WAZI KUWA WATAWAFUNGA YANGA MABAO MATATU

Image
OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa mchezo wao dhidi ya Yanga, Julai 3 wanaweza kuwafunga mabao matatu kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara ambao unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa.  Ameweka wazi kuwa jambo la msingi kwa waamuzi ni kufuata kanuni na kwa namna walivyojipanga basi hazitapungua tatu.  

SIMBA YATAKA KUSEPA NA UBINGWA MBELE YA YANGA

Image
  HAJI Manara, Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa wanaamini kwamba kwenye mchezo wao ujao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga watapata pointi tatu muhimu ili watangazwe kuwa mabingwa. Ikiwa ipo nafasi ya kwanza na pointi 73 inahitaji pointi tatu ili kufikisha pointi 76 ambazo hazitafikiwa na watani wao wa jadi walio nafasi ya pili na pointi 67 ndani ya ligi. Manara amesema kuwa maandalizi ya mchezo yapo kamili hivyo wataingia uwanjani wachezaji kwa nidhamu na wakitambua kwamba utakuwa mchezo mgumu huku hesabu zao ikiwa ni kupata pointi tatu ili watangazwe kuwa mabingwa. "Mechi itakuwa ngumu hilo lipo wazi na tunawaheshimu wapinzani wetu lakini ni lazima tupate pointi tatu ili tutangazwe kuwa mabingwa. "Niwaombe mashabiki wajitokeze kwa wingi na mara baada ya mchezo tuwapigie makofi wachezaji kwa wingi kwa kuweza kutwaa ubingwa wa ligi mara nne mfululizo," .

JEMBE LA KAZI YANGA LARUDI KAZINI, KAMILI KUIVAA SIMBA

Image
  ABDUL Shaibu, 'Ninja' beki wa kati ndani ya kikosi cha Yanga amerejea tayari kikosini kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba.  Nyota  huyo alikuwa  nje ya uwanja kwa muda akitibu majeraha aliyopata katika mechi za ushindani ndani ya ardhi ya Bongo. Huenda akawa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Simba Julai 3, Uwanja wa Mkapa kutokana na uzoefu wa mechi hizo kubwa ambapo aliweza kuwa kwenye kikosi cha kwanza walipokutana ndani ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar. Mchezo wake wa mwisho kuonekana ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora baada ya hapo alikuwa nje ya uwanja akitibu majeraha. Taarifa kutoka Yanga zimeeleza kuwa beki huyo alianza mazoezi binafsi wakati timu ilipokuwa na mchezo dhidi ya Biashara United na sasa amejiunga na wachezaji wenzake.

VIDEO: MO NA MANJI USO KWA USO

Image
KUNA uwezekano mkubwa wa Mohamed Dewji, 'Mo' ambaye ni Mwenyekiti wa Bodi ya Wakurugenzi Simba pamoja na Yusuph Manji aliyekuwa Mwenyekiti wa Yanga huenda wanaweza kukutana Uwanja wa Mkapa kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa Julai 3.   

POLISI TANZANIA YATAJA NAFASI WANAYOHITAJI NDANI YA LIGI

Image
MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kumaliza ligi ndani ya tano bora. Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 42 ipo nafasi ya 7, nafasi ya tano ipo mikononi mwa Namungo FC yenye pointi 43 imecheza mechi 32. Mchezo wake uliopita ndani ya ligi iligawana pointi mojamoja na Ruvu Shooting mchezo uliochezwa Juni 24 ambapo mabao ya kila timu kwa wachezaji walifunga kwa kichwa. Alikuwa ni David Oromi kwa Ruvu Shooting dk 34 alifunga kwa kichwa na usawa kwa Polisi Tanzania uliwekwa na Tarig Seif kwa kichwa. Kocha huyo amesema:"Tuna mechi zimebaki hizo tutapambana kupata pointi tatu muhimu ili kufikia malengo yetu ya kumaliza ligi ndani ya tano bora. "Ushindani ni mkubwa hilo tunalijua hivyo tunapambana ili kupata ushindi katika mechi ambazo zimebaki," .

YANGA YATOA TAMKO KUHUSU MECHI YAO DHIDI YA SIMBA

Image
  UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Julai 3 watapata ushindi kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya huku wakiwataka watani zao wa jadi kutobadili muda. Ikumbukwe kwamba mchezo wa Julai 3 ulipaswa kuchezwa awali Mei 8 ila uliyeyuka mazima baada ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kueleza kwamba kuna mabadiliko ya muda. Ule wa awali ulipangwa saa 11:00 jioni ila masaa machache kabla ya mchezo huo kuchezwa huku mashabiki wakiwa wameanza kuingia taarifa kutoka TFF kupitia kwa Ofisa Habari, Cliford Ndimbo ilieleza kuwa mchezo huo utachezwa saa 1:00 jioni, jambo ambalo Yanga waliweka wazi kwamba hawatacheza muda huo kwa kuwa ni kinyume cha kanuni. Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz ameweka wazi kwamba hawana hofu na mchezo wao wa watani wa jadi ila jambo la muhimu wasibadili muda. "Hatuna mashaka na kikosi chetu na kwenye mechi zetu ambazo zimebaki tuna amini kwamba tutafanya vizuri bila mashaka. "Kikubwa ni

VIDEO: SIMBA YASAJILI WATATU WAPYA

Image
OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamekamilisha usajili wa wachezaji watatu kimyakimya kwa makubaliano ya kuwalinda wachezaji hao wasiweze kujulikana.   

BIASHARA UNITED YAWAITA YANGA WAFANYE BIASHARA YA KIPA

Image
 UONGOZI wa Biashara United, umeweka wazi ikiwa mabosi wa Yanga wanahitaji saini ya kipa wao namba moja, Daniel Mgore ni suala la kukaa mezani ili kufanya mazungumzo. Imekuwa ikielezwa kuwa, Yanga inahitaji kuboresha kikosi chao hasa upande wa mlinda mlango baada ya kipa wao namba moja, Metacha Mnata kusimamishwa kutokana na utovu wa nidhamu, huku mkataba wake ukielekea ukingoni. Pia katika kikosi hicho, Faroukh Shikalo na Ramadhan Kabwili ambao ndiyo makipa waliobaki, nao mikataba yao inaelekea kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Akizungumza na Spoti Xtra, Mwenyekiti wa Biashara United, Seleman Mataso, alisema kuwa hawana tatizo ikiwa kuna timu inahitaji kumpata kipa wao ni suala la kukaa mezani.   “Hakuna ambaye anaweza kumzuia mchezaji, huyu Mgore tumemkuza wenyewe kutoka timu ya vijana, kama kuna timu inamuhitaji iwe Yanga ama Azam FC, ni suala la kuzungumza," . Kipa huyo alipata nafasi ya kuitwa kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars, msimu uliopita alimaliza

ISHU YA LUIS KUIBUKIA YANGA MANARA AFUNGUKA

Image
 WAKATI tetesi zikieleza kuwa kiungo wao fundi wa kutumia mguu wa kushoto kufunga Luis Miquissone yupo kwenye rada za Yanga uongozi wa Simba umesema kuwa bado dili hilo halijakamilika na mkwanja unaohitajika ni mrefu. Ndani ya ligi, Luis akiwa ametupia mabao 9 amefunga mabao 7 kwa mguu wa kushoto huku moja akitumia mguu wa kulia na lingine alifunga kwa kichwa dk 90 mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa. Haji Manara Ofisa Habari wa Simba amesema kuwa hakuna taarifa yoyote kuhusu mchezaji huyo kuuzwa na badala yake timu itakayomhitaji lazima itoe mkwanja mrefu kupata saini yake. "Hakuna ambaye anaweza kusema kwamba mchezaji wa Simba ni mali yao kwa sasa, hakuna tetesi za namna hiyo eti unasema mchezaji anatakiwa na timu fulani wakati bado ana mkataba? "Kuna mob ambayo inapenda kwenda na mambo hasa yanapotokea na tunayajua ila sio kwa hili hakuna jambo kama hilo, Simba tupo tofauti kabisa, ikiwa kuna timu kutoka Tanzania inamuhitaji Luis ijiandae kutoa dola milioni 10

RATIBA YA MECHI ZA LIGI KUU BARA AMBAZO NI VIPORO

Image
IKIWA kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara ipo raundi ya pili ya lala salama , kuna mechi tatu ambazo zitachezwa baada ya kupangiwa ratiba upya ambapo ratiba ya awali mambo yalikwenda tofauti. Viporo hivyo vitatu vipo namna hii:-Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 73 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 67 itakuwa Julai 3,2021, Uwanja wa Mkapa, saa 11:00 jioni. KMC iliyo nafasi ya 6 na pointi 42 itamenyana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 73, Julai 7, Uwanja wa CCM Kirumba. Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes itamenyana na Coastal Union ya Juma Mgunda, Julai 11, Uwanja wa Mkapa.

YANGA WATAJA SABABU ZA KUCHUKUA UBINGWA WA SIMBA

Image
HASSAN Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa bado wana nafasi ya kutwaa ubingwa kwa kuwa kikosi chao kinazidi kuimarika kila leo. Kwenye mataji yote mawili ikiwa ni la ligi pamoja na lile la Kombe la Shirikisho mabingwa watetezi ni Simba ambapo wametinga hatua ya fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Azam FC huku Yanga wakitinga hatua ya fainali kwa ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Biashara United. Yanga ipo katika  nafasi ya pili katika  msimamo wa Ligi Kuu  Bara, huku ikiwa na  pointi 67 ikiongozwa na  kinara wa Simba wenye  pointi 73.   Akizungumza na  Spoti Xtra, Bumbuli  alisema kuwa kila kitu  kipo katika utaratibu  wake katika suala la  maandalizi, kwa hiyo  wamejipanga kuchukua  ubingwa wa FA.   “Maandalizi  yanaendelea vizuri  kama kawaida, niseme  tu kwamba tumejipanga  kuchukua ubingwa  katika pande zote.   "Kikosi chetu kinazidi  kuimarika kila siku  na sitaki kuongea  sana, lakini mtajionea  wenyewe kinachoenda  kutokea, lazima  tuchukue ubingwa,”  alis

VIDEO: SIMBA, TUNASHINDA MBELE YA YANGA, WACHEZAJI WOTE WAPO SAWA

Image
OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wanaamini kwamba kuelekea kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Yanga, Julai 3 watashinda na kuchukua pointi tatu pamoja na kutwaa ubingwa wa Ligi Kuu Bara.  

YANGA YATENGA BILIONI 8.1 ZA CAF

Image
  K LABU ya Yanga,  imetenga kitita  cha Sh bilioni 8.1  ili kuhakikisha  msimu ujao timu  yao inafanya vizuri kwenye  michuano watakayoshiriki  ikiwemo michuano ya kimataifa  inayosimamiwa na Shirikisho la  Soka Afrika (CAF).   Yanga msimu ujao inatarajiwa  kushiriki Ligi Kuu Bara, Kombe la  FA na michuano ya kimataifa kati  ya Kombe la Shirikisho Afrika na  Ligi ya Mabingwa Afrika.   Bajeti hiyo imetangazwa,  Jumapili na kupitishwa na  wanachama wa  klabu hiyo katika  mkutano wao mkuu  uliofanyika kwenye  Ukumbi wa DYCCC,  Chang’ombe, Dar es  Salaam. Katika bajeti  hiyo iliyotolewa  na Mwenyekiti wa  Yanga, Mshindo  Msolla, kiasi  hicho cha fedha  kitatumika kwa ajili  ya mishahara ya  wachezaji ambacho  ni Sh bilioni 4.9. Msolla alisema Sh milioni 854.7  zimetengwa kwa ajili ya bonasi  kwa wachezaji wao lengo ni  kuwaongezea morali ya kupambana  ndani ya uwanja ili kuhakikisha  wanapata matokeo mazuri ya  ushindi. Aliongeza kuwa, klabu hiyo  itakusanya fedha hizo kutoka 

SIMULIZI YA FAMILIA ILIYOLINDWA ISIKAMATWE NA POLISI

Image
SIMULIZI ya familia iliyolindwa isikamatwe kwa kutengeneza pombe ya jadi dhidi ya Polisi:- Nilizaliwa kwenye familia masikini sana na wakati nilikuwa na umri wa miaka sita, baba yangu aliiacha familia yetu kwa sababu ya shida na aliamua kwenda nchi nyingine.  Mama  yangu aliachwa kutulea na hii ilimfanya aanze kuuza pombe ya jadi ili kutupeleka shule na pia kulipia mahitaji yetu ya msingi kama vile kodi na chakula. Walakini, miezi michache iliyopita, Polisi walipiga mjeledi juu ya watengeneza pombe za jadi katika eneo letu na yeyote aliyekamatwa alifungwa maisha. Niliogopa sana mama yangu kwa sababu hii haikumtisha. Kufikia wakati huu, nilikuwa na miaka 20 na nilikuwa nikimsaidia pia. Tulikuwa masikini sana na hivi ndiyo tu tungeishi. Pamoja na Polisi kutuwinda mchana na usiku na mama yangu akiwa mkaidi kwamba ataendelea kuuza bia, niliamua kutafuta njia mbadala za kumlinda asikamatwe na Polisi.  Nilifikiria kuajiri  baadhi ya mamluki kwa usalama lakini kwa kuwa s

BREAKING: SIMBA QUEENS YAMALIZANA NA MSHAMBULIAJI WA MABAO

Image
 RASMI Simba Queens imempa dili la miaka miwili mshambuliaji Aisha Juma kuitumikia timu hiyo. Nyota huyo ambaye ni mshambuliaji msimu uliopita wa 2020/21 alikuwa anakipiga ndani ya timu ya Alliance Girls ambapo amedumu kwa zaidi ya misimu miwili. Msimu uliopita nyota huyo kwa mujibu wa rekodi za mfalme wa soka la Wanawake Tanzania na mwandishi wa Global Group, Issa Liponda, maarufu kama mbuzi  alitupia mabao 27.  Unakuwa ni usajili wa pili kwa Simba Queens ambao ni mabingwa mara mbili wa taji la Ligi ya Wanawake ambapo Juni 29 walimtambulisha Brenda Chaora kuwa kocha mpya wa viungo.

VIDEO: KARIA APETA TFF,YANGA WAJA NA MIKAKATI MIZITO

Image
MGOMBEA wa nafasi ya Urais ndani ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF), Wallace Karia amepeta kwenye mchujo wa awali pia Yanga wameweka mikakati mizito.   

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

Image
PRESHA kubwa kwa sasa ni kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa kutokana na watani hawa wa jadi kuwa kwenye vita ya kusaka pointi tatu. Kikubwa ni kwamba mashabiki wanahitaji kuona mpira ukichezwa huku ile presha sijui ya timu moja haitaleta timu ikitakiwa kufutwa kwa kuwa timu yenyewe inayotajwa kuwa haitapeleka timu haijatoa taarifa rasmi. Jambo la msingi kuelekea kwenye mchezo huo kwa sasa kwa Shirikisho la Soka Tanzania ni kuangalia namna gani ratiba yao itakuwa na kuwasiliana pia na Serikali yasije kutokea yale ya Mei 8 ngoma ikabadilishwa wakati mashabiki wapo uwanjani. Kila kitu kipangwe vizuri na utaratibu uwekwe kwa kuwa nimeona kwa sasa tayari taarifa kuhusu zile tiketi na namna ya kuweza kuingia uwanjani zikiwa zimewekwa wazi.  Kikubwa ambacho kinahitajika kwa mashabiki ambao watajitokeza Uwanja wa Mkapa kuacha kubeba matokeo uwanjani na kuendelea kufanya maandalizi yao kwa hesabu ili kupata pointi tatu.

MTAMBO WA MABAO UPO TAYARI KUTUA YANGA

Image
 YUSUPH Mhilu, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Kagera Sugar kwa sasa anawasubiri Yanga ili aweze kusaini dili jipya kwa ajili ya kuwatumikia kwa msimu ujao wa 2021/22. Habari zimeeleza kuwa nyota huyo licha ya kuwa bado ana dili la mwaka mmoja ndani ya Kagera Sugar anafikiria kuondoka ikiwa atapata dil jipya. “Mhilu bado yupo Kagera Sugar lakini anaweza kuondoka ikiwa atapata ofa kubwa na malengo yake ni kuweza kupata changamoto mpya hivyo kwa sasa anasubiri mabosi wa Yanga na Azam FC waweze kukamilisha mpango wao,” ilieleza taarifa hiyo. Mhilu mwenyewe aliliambia Championi Jumatatu kwamba anahitaji kupata changamoto mpya iwe ndani ya Bongo ama nje yeye yupo tayari kucheza. “Ninafikiria sana kwenda kucheza nje ya nchi ili kuwa imara zaidi ya hapa lakini imani yangu ni kwamba inawezekana na ninaweza. wa kuwa nina kipaji na uwezo mkubwa,” alisema Mhilu mwenye mabao. Imekuwa ikieelezwa kuwa Mhilu ambaye aliwahi kucheza ndani ya Yanga yupo kwenye mpango wa kusajiliw

BWALYA WA AL AHLY KUTUA SIMBA ISHU YAKE IPO HIVI

Image
  NYOTA wa timu ya Al Ahly ya Misri, Walter Bwalya inaelezwa kuwa dili lake la kutua Simba limefika hatua nzuri baada ya mabosi wa timu hiyo kuwa na mpango wa kumuondoa katika kikosi hicho. Bwalya alikuwa anapigiwa hesabu na Simba kwa muda mrefu jambo ambalo linawafanya waendelee kuiwinda saini yake ili aweze kujiunga na kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Bara. Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes inahitaji saini ya mshambuliaji mmoja na anayetajwa kuwa katika hesabu za Simba ni Bwalya. Taarifa zinaeleza huenda Simba ikapata saini ya mshambuliaji huyo kwa mkopo wa mwaka mmoja katika usajili wa msimu ujao. "Al Ahly na Simba mazungumzo yanakwenda vizuri na muda wowote ikiwa dili litajibu anawezeza kusajiliwa Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja ila ishu kubwa ni kwenye upande wa mshahara wa mchezaji huyo hapo ndipo mvutano upo," ilieleza taarifa hiyo.

VIDEO: VIDEO MPYA YA ALIKIBA NI KAMA MUVI VILE

Image
VIDEO mpya ya AliKiba ambayo itaachiwa leo Juni 30 ni kama muvi vile inaitwa Salute  

UJERUMANI WAKUBALI YAISHE EURO 2020

Image
  JOACHIM Low, Kocha Mkuu wa Ujerumani amesema kuwa huwa inatokea kwa wachezaji wazuri kutolewa katika hatua ya mtoano kutokana na makosa ambayo wanayafanya hivyo kwa kilichowatokea kwao hamna namna ya kuzuia. Katika mchezo wa hatua ya 16 bora ndani ya Euro 2020, Ujerumani ilikubali kuona ubao wa Uwanja wa Wembley ukisoma England 2-0 Ujerumani. Ni Raheem Sterling dk 75 alipachika bao la kwanza na lile la pili lilipachikwa na nahodha Harry Kane dk ya 86 na kuwaondoa wapinzani wao huku England ikitinga hatua ya robo fainali ambapo itakutana na Ukraine iliyoshinda mabao 2-1 Sweden. Kwa upande wa Kocha Mkuu wa England, Gareth Southgate amesema kuwa wachezaji walitumia nguvu nyingi kusaka ushindi mbele ya timu imara jambo ambalo kwao liliwapa matunda. England imeweza kushinda jumla ya mechi 14 na ililazimisha sare nne huku ikipoteza ushindi katika jumla ya mechi 15 ambazo wamekutana katika mashindano yote pamoja na mechi za kirafiki tangu Mei 10,1930.

UKRAINE YATINGA ROBO FAINALI EURO 2020

Image
 KATIKA mchezo wa hatua ya 16 bora hatimaye Ukraine imetinga hatua ya robo fainali kwa ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya Sweden. Ni Oleksandr Zinchenko dk 27 alifungua pazia la ushindi kwa Ukraine likawekwa usawa na Emil Forsberg. Mpaka dk 90 zinakamilika ubao wa Uwanja wa Hampden Park ulikuwa unasoma Sweden 1-1 Ukraine. Kwenye dk 30 zs nyongeza ni Artem Dovbyk alipachika bao dk 120+1 na kuifanya timu yake ya Taifa ya Ukraine kutinga hatua ya robo fainali. Ni Marcus Danielson dk 99 alionyeshwa kadi nyekundu na kuwafanya Sweden kumaliza pambano hilo la Euro 2020 wakiwa pungufu.

WANAYANGA KWA HILI MMETISHA AISEE

YANGA: HATUNA PRESHA DHIDI YA SIMBA, TUNAWAPIGA

MAISHA YA SHILINGI YA BERNARD MORRISON NA UTAMU WAKE

VIDEO: MZEE MPILI USO KWA USO NA INJINIA, MECHI DHIDI YA SIMBA WANA IMANI YA KUSHINDA

Image
MZEE Mpili,Mwanachama wa Yanga amekutana na Injinia Hersi Said ambaye ni Makamu Mwenyekiti katika masuala ya Usajili ndani ya Yanga, kuelekea kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Julai 3, Mzee Mpili amesema kuwa ana watu na wana amini kwamba watashinda mchezo huo.  

VIDEO: MASHABIKI YANGA WAMCHONGEA MO KWA MANJI

Image
MARA baada ya aliyekuwa Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Yusuf Manji kuibuka kwenye mkutano mkuu wa Wanachama wa Yanga, mashabiki wamemsemea bosi huyo kuhusu suala la Mohamed Dewji wa Simba, 'Mo' kuwaonea hasa katika masuala ya uwekezaji ambao umefanywa na wapinzani wao Simba jambo lililowafanya wamuombe arudi tena.  

VIDEO: KARIA MGOMBEA PEKEE NAFASI YA URAIS, WENGINE WAPIGWA CHINI MAZIMA

Image
LEO Juni 29, Kamati ya Uchaguzi Mkuu wa Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kupitia Makamu Mwenyekiti wa Kamati ya Uchaguzi, Benjamini Kalume imetangaza majina ya wagombea ambao wamepita kwenye mchujo wa awali huku kwa upade wa nafasi ya Uraisi ni Wallace Karia amepitishwa peke yake kwa maelezo kuwa amekidhi vigezo na wengine watatu wakipigwa chini mazima.  

LISTI YA WAPIGA PENALTI YA UJERUMANI YAVUJA

JEMBE LA ARSENAL KUTUA CRYSTAL PALACE

KARIA APITISHWA MCHUJO WA UGOMBEA URAIS TFF

Image
MGOMBEA wa nafasi ya Urais katika Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF)  Wallace Karia amepenya kwenye mchujo wa awali na kumfanya awe mgombea pekee wa Urais wa TFF. Hii ni baada ya Hawa Mniga pamoja na Evance Mgeusa kikosa vigezo vinavyokidhi kwenda hatua inayofuata baada ya mchujo uliofanywa na Kamati ya Uchaguzi ya TFF. Kwa maana hiyo Wallace Karia anasubiri kwenda kuthibitishwa na Mkutano mkuu na si kumpigia Kura. Kwa mujibu wa Benjamin Kalume Makamu Mwenyekiti kamati ya Uchaguzi TFF.

SIMBA YAIKIMBIZA YANGA NDANI YA DK 450, KAZI JULAI 3

Image
  ZIKIWA zimebeki siku nne kwa watani wa jadi, Simba na Yanga kukutana Uwanja wa Mkapa, rekodi zinaonyesha kuwa makocha wawili Didier Gomes wa Simba na Nassredine Nabi wa Yanga walikuwa na kazi ya kukimbizana ndani ya dk 450. Kwenye mechi zao tano za hivi karibuni kwenye ligi Gomes alionekana kumkimbiza Nabi kwa kusepa na pointi nyingi ambazo ni 15 huku Nabi akisepa na pointi zake 10. Ni Gomes raia wa Ufaransa alishinda mechi zake 5 alizokaa kwenye benchi na alishuhudia jumla ya mabao 14 wachezaji wake wakifunga na mabao matatu waliokota kwenye nyavu zao. Ndani ya dakika 450 msako wa pointi 15 Simba ilisepa na pointi zote mazima ambapo ugenini ilikuwa kwenye mechi tatu na nyumbani ilikuwa kwenye mechi mbili. Mwendo wa Gomes ulikuwa namna hii:-Aprili 27, Simba 3-1 Dodoma Jiji,Uwanja wa Mkapa, Mei 29, Namungo 1-3 Simba,Uwanja wa Majaliwa, Juni 3, Ruvu Shooting 0-3 Simba, uwanja wa CCM Kirumba, Juni 19, Polisi Tanzania 0-1 Simba, Uwanja wa CCM Kirumba, Juni 22, Simba 4-1 Mbeya City

NABI AMPATA MBADALA WA METACHA MNATA YANGA

Image
  K OCHA Mkuu  wa Yanga,  Nasreddine Nabi  amemjumuisha  kikosini kipa  wa timu ya  vijana, Geofrey  Magaigwa ili  kuchukua nafasi  ya Metacha  Mnata ambaye  amesimamishwa  kutokana na  suala la utovu wa  nidhamu.   Yanga U20,  ilifanikiwa  kufanya vizuri  kwenye Ligi ya  Vijana ambapo ilishika nafasi  ya pili baada ya kupoteza  mchezo wa fainali dhidi ya  Mtibwa kwa mabao 2-1 kwenye  Uwanja wa Azam Complex,  Chamazi, Dar.   Geofrey Magaigwa ni miongoni mwa wachezaji ambao kwa sasa wamekuwa wakifanya mazoezi na timu ya wakubwa inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassrednine Nabi.   Akizungumza na  Championi  Jumamosi,  Mkurugenzi wa  Mashindano wa Klabu ya  Yanga, Thabit  Kandoro alisema  kuwa: “Kwanza  tumefarijika sana  na timu ya vijana  ambayo imefanya  vizuri katika  mashindano pamoja  na vipaji vikubwa  walivyovionyesha.   “Tunaweka  mikakati mizuri  ya kufanya kitu  kikubwa zaidi kwa  vijana kwa ajili  ya msimu ujao ili  kuhakikisha tunalichukua kombe  la vijana.   “Kocha Na

GOMES ATAJA MAJEMBE YAKE YANAYOMPA JEURI UWANJANI

Image
  K OCHA Mkuu wa  Simba, Didier  Gomes amefunguka  kuwa siri kubwa  ya ubora kikosi chake katika  kuchezea mpira inatokana  na balansi inayoletwa na  matumizi ya viungo wawili  wakabaji, kulinganisha na  wanapotumia kiungo mmoja  pekee. Ndani ya kikosi cha Simba,  Gomes amekuwa akiwatumia  zaidi Taddeo Lwanga na  Mzamiru Yassin kama pacha ya  viungo wakabaji ndani ya kikosi  chake katika michezo mingi, hali  inayowapa urahisi viungo wa juu  wa Simba kuwa na wakati mzuri  wa kuchezea mpira.   Akizungumza na  Championi  Jumamosi,  Gomes alisema:  “Tumekuwa tukitumia mifumo  mbalimbali kuendana na  wapinzani ambao tunakutana  nao, lakini naweza kusema  kikosi chetu kinakuwa na  balansi kubwa na kucheza vizuri  zaidi iwapo tunacheza na viungo  wawili wakabaji. “Lakini kuna wakati  tunalazimika kujitoa mhanga  kwa kutumia kiungo mmoja  pekee hasa tunapotumia mfumo  wa 3-5-2, kama ambavyo  tulicheza dhidi ya Mbeya City," . Mchezo ujao wa Simba ni dhidi ya Yanga unatarajiwa kuch