JEMBE LA KAZI YANGA LARUDI KAZINI, KAMILI KUIVAA SIMBA

 


ABDUL Shaibu, 'Ninja' beki wa kati ndani ya kikosi cha Yanga amerejea tayari kikosini kujiunga na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba. 

Nyota  huyo alikuwa  nje ya uwanja kwa muda akitibu majeraha aliyopata katika mechi za ushindani ndani ya ardhi ya Bongo.


Huenda akawa sehemu ya kikosi cha Yanga kitakachoanza dhidi ya Simba Julai 3, Uwanja wa Mkapa kutokana na uzoefu wa mechi hizo kubwa ambapo aliweza kuwa kwenye kikosi cha kwanza walipokutana ndani ya Kombe la Mapinduzi, Zanzibar.


Mchezo wake wa mwisho kuonekana ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons katika mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 16 bora baada ya hapo alikuwa nje ya uwanja akitibu majeraha.

Taarifa kutoka Yanga zimeeleza kuwa beki huyo alianza mazoezi binafsi wakati timu ilipokuwa na mchezo dhidi ya Biashara United na sasa amejiunga na wachezaji wenzake.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA