POLISI TANZANIA YATAJA NAFASI WANAYOHITAJI NDANI YA LIGI


MALALE Hamsini, Kocha Mkuu wa Polisi Tanzania amesema kuwa malengo makubwa ya timu hiyo ni kumaliza ligi ndani ya tano bora.

Ikiwa imecheza jumla ya mechi 32 imekusanya pointi 42 ipo nafasi ya 7, nafasi ya tano ipo mikononi mwa Namungo FC yenye pointi 43 imecheza mechi 32.

Mchezo wake uliopita ndani ya ligi iligawana pointi mojamoja na Ruvu Shooting mchezo uliochezwa Juni 24 ambapo mabao ya kila timu kwa wachezaji walifunga kwa kichwa.

Alikuwa ni David Oromi kwa Ruvu Shooting dk 34 alifunga kwa kichwa na usawa kwa Polisi Tanzania uliwekwa na Tarig Seif kwa kichwa.

Kocha huyo amesema:"Tuna mechi zimebaki hizo tutapambana kupata pointi tatu muhimu ili kufikia malengo yetu ya kumaliza ligi ndani ya tano bora.

"Ushindani ni mkubwa hilo tunalijua hivyo tunapambana ili kupata ushindi katika mechi ambazo zimebaki," .


Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA