BWALYA WA AL AHLY KUTUA SIMBA ISHU YAKE IPO HIVI

 


NYOTA wa timu ya Al Ahly ya Misri, Walter Bwalya inaelezwa kuwa dili lake la kutua Simba limefika hatua nzuri baada ya mabosi wa timu hiyo kuwa na mpango wa kumuondoa katika kikosi hicho.

Bwalya alikuwa anapigiwa hesabu na Simba kwa muda mrefu jambo ambalo linawafanya waendelee kuiwinda saini yake ili aweze kujiunga na kikosi hicho kinachoshiriki Ligi Kuu Bara.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes inahitaji saini ya mshambuliaji mmoja na anayetajwa kuwa katika hesabu za Simba ni Bwalya.

Taarifa zinaeleza huenda Simba ikapata saini ya mshambuliaji huyo kwa mkopo wa mwaka mmoja katika usajili wa msimu ujao.

"Al Ahly na Simba mazungumzo yanakwenda vizuri na muda wowote ikiwa dili litajibu anawezeza kusajiliwa Simba kwa mkopo wa mwaka mmoja ila ishu kubwa ni kwenye upande wa mshahara wa mchezaji huyo hapo ndipo mvutano upo," ilieleza taarifa hiyo.




Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA