NABI AMPATA MBADALA WA METACHA MNATA YANGA

 


KOCHA Mkuu wa Yanga, Nasreddine Nabi amemjumuisha kikosini kipa wa timu ya vijana, Geofrey Magaigwa ili kuchukua nafasi ya Metacha Mnata ambaye amesimamishwa kutokana na suala la utovu wa nidhamu.

 

Yanga U20, ilifanikiwa kufanya vizuri kwenye Ligi ya Vijana ambapo ilishika nafasi ya pili baada ya kupoteza mchezo wa fainali dhidi ya Mtibwa kwa mabao 2-1 kwenye Uwanja wa Azam Complex, Chamazi, Dar.

 

Geofrey Magaigwa ni miongoni mwa wachezaji ambao kwa sasa wamekuwa wakifanya mazoezi na timu ya wakubwa inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassrednine Nabi.

 

Akizungumza na Championi Jumamosi, Mkurugenzi wa Mashindano wa Klabu ya Yanga, Thabit Kandoro alisema kuwa: “Kwanza tumefarijika sana na timu ya vijana ambayo imefanya vizuri katika mashindano pamoja na vipaji vikubwa walivyovionyesha.

 

“Tunaweka mikakati mizuri ya kufanya kitu kikubwa zaidi kwa vijana kwa ajili ya msimu ujao ili kuhakikisha tunalichukua kombe la vijana.

 

“Kocha Nabi na benchi zima la ufundi lilikuwa linashuhudia mashindano ya vijana yaliyofanyika Chamazi na wamevutiwa sana na vipaji vyao, hivyo ameanza kumjumuisha Geofrey kwenye timu kubwa badala ya Metacha ambaye amesimamishwa kwa sasa,” alisema Kandoro.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA