BREAKING: SIMBA QUEENS YAMALIZANA NA MSHAMBULIAJI WA MABAO


 RASMI Simba Queens imempa dili la miaka miwili mshambuliaji Aisha Juma kuitumikia timu hiyo.


Nyota huyo ambaye ni mshambuliaji msimu uliopita wa 2020/21 alikuwa anakipiga ndani ya timu ya Alliance Girls ambapo amedumu kwa zaidi ya misimu miwili.

Msimu uliopita nyota huyo kwa mujibu wa rekodi za mfalme wa soka la Wanawake Tanzania na mwandishi wa Global Group, Issa Liponda, maarufu kama mbuzi  alitupia mabao 27.

 Unakuwa ni usajili wa pili kwa Simba Queens ambao ni mabingwa mara mbili wa taji la Ligi ya Wanawake ambapo Juni 29 walimtambulisha Brenda Chaora kuwa kocha mpya wa viungo.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA KUBADILI KIKOSI MBELE YA TP MAZEMBE AMBAO WATABADILI MFUMO KESHO

SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUINYOOSHA AIGLE NOIR KWA MKAPA ULICHEZWA HIVI