RATIBA YA MECHI ZA LIGI KUU BARA AMBAZO NI VIPORO



IKIWA kwa sasa Ligi Kuu Tanzania Bara ipo raundi ya pili ya lala salama , kuna mechi tatu ambazo zitachezwa baada ya kupangiwa ratiba upya ambapo ratiba ya awali mambo yalikwenda tofauti.


Viporo hivyo vitatu vipo namna hii:-Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 73 itamenyana na Yanga iliyo nafasi ya pili na pointi 67 itakuwa Julai 3,2021, Uwanja wa Mkapa, saa 11:00 jioni.



KMC iliyo nafasi ya 6 na pointi 42 itamenyana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 73, Julai 7, Uwanja wa CCM Kirumba.

Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes itamenyana na Coastal Union ya Juma Mgunda, Julai 11, Uwanja wa Mkapa.




Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO