YANGA YATOA TAMKO KUHUSU MECHI YAO DHIDI YA SIMBA

 


UONGOZI wa Yanga umeweka wazi kuwa kuelekea mchezo wao wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Simba, Julai 3 watapata ushindi kutokana na maandalizi ambayo wameyafanya huku wakiwataka watani zao wa jadi kutobadili muda.

Ikumbukwe kwamba mchezo wa Julai 3 ulipaswa kuchezwa awali Mei 8 ila uliyeyuka mazima baada ya Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) kueleza kwamba kuna mabadiliko ya muda.

Ule wa awali ulipangwa saa 11:00 jioni ila masaa machache kabla ya mchezo huo kuchezwa huku mashabiki wakiwa wameanza kuingia taarifa kutoka TFF kupitia kwa Ofisa Habari, Cliford Ndimbo ilieleza kuwa mchezo huo utachezwa saa 1:00 jioni, jambo ambalo Yanga waliweka wazi kwamba hawatacheza muda huo kwa kuwa ni kinyume cha kanuni.

Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz ameweka wazi kwamba hawana hofu na mchezo wao wa watani wa jadi ila jambo la muhimu wasibadili muda.

"Hatuna mashaka na kikosi chetu na kwenye mechi zetu ambazo zimebaki tuna amini kwamba tutafanya vizuri bila mashaka.

"Kikubwa ni kwamba wasibadili muda wafuate utaratibu ambao umewekwa na kusiwe na makandomakando," amesema.

Kwenye msimamo wa ligi, Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nasreddine Nabi ipo nafasi ya pili na pointi 67 huku Simba ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 73.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA