Posts

Showing posts from November, 2020

AZAM FC BADO WANAUHITAJI UBINGWA

Image
  KIUNGO wa Klabu ya Azam, Salum Abubakar ‘Sure Boy’ amefunguka kuwa changamoto ya kupata matokeo mabaya kwenye michezo yao iliyopita ya Ligi Kuu Bara haijawaondoa kwenye plani zao, kwani bado wanaamini wana nafasi kubwa ya kupambania ubingwa msimu huu.    Azam ilianza kwa kasi msimu huu kwa kushinda michezo saba mfululizo,ilipunguzwa na Mtibwa Sugar, Uwanja wa Jamhuri, Morogoro kwa kufungwa bao 1-0. Jana Novemba 30 ilikubali sare ya kufungana bao 1-1 na Biashara United, Uwanja wa Karume na kuifanya ifikishe jumla ya pointi 26 ikiwa nafasi ya pili na ile ya kwanza ipo mikononi mwa Yanga yenye pointi 31.   Sure Boy amesema matokeo hayo mabaya ni sehemu ya mpira na wanachokifanya hivi sasa ni kurekebisha makosa yao na kujipanga kwa ajili ya kuhakikisha wanashinda michezo ijayo.   “Kama timu ambayo ina malengo ya kutwaa ubingwa msimu huu ni wazi tulikuwa kwenye wakati mgumu sana kutokana na matokeo mabaya kwenye michezo yetu iliyopita.   “Lakini kwenye mchezo wa soka kuna wak

SIMBA KUTUA BONGO LEO KUJIWINDA DHIDI WANAIGERIA

JIMENEZ AZUNGUMZIA HALI YAKE

Image
MSHAMBULIAJI wa Wolves, Raul Jimenez amezungumza kwa mara ya kwanza kupitia twitter baada ya kufanyiwa upasuaji kutokana na mshtuko kwenye ubongo.  Raia huyo wa Mexico amezungumza kwa mara ya kwanza  baada ya kufanyiwa upasuaji kwa kuwa alipata mshtuko alipogongana na David Luiz kwenye mchezo wa Ligi Kuu Engand Jumapili ambapo Arsenal ilipoteza kwa kufungwa mabao 2-1. Nyota huyo amesema kuwa bado yupo kwenye matibabu na anaamini kwamba atarejea uwanjani hivi karibuni kwa kuwa anaendelea vizuri.  Jimenez ameweka wazi kuwa shukrani zake ni kwa Mungu pamoja na mashabiki ambao wamekuwa wakimtumia ujumbe kwa ajili ya kumjulia hali na kumuombea kheri. "Asante kwa sapoti kupitia meseji zenu mashabiki, nipo kwenye maendeleo mazuri kwa sasa na nina matumaini kwamba nitarejea uwanjani hivi karibuni," amesema. Wolves pia wameweka taarifa kwamba nyota huyo anaendelea vizuri baada ya kufanyiwa upasuaji kwa kuwa ulikwenda vizuri katika hospitali ya London hivyo atarejea uwanjani hi

NGORONGORO HEROES MZIGONI TENA BAADA YA KUFUZU AFCON

Image
USHINDI walioupata jana, Ngorongoro Heroes wa bao 1-0 dhidi ya Sudani Kusini umewapa nafasi ya kutinga michuano ya Kombe la Mataifa Afrika kwa Vijana chini ya miaka 20.(Afcon) Bao pekee la Ngorongoro lilipatikana dakika ya 55 kupitia kwa Kassim Shaban baada ya kipa wa timu hiyo kutema mpira uliopigwa na Kelvin John. Kesho Desemba 2 inatarajiwa kuwa fainali kati ya Ngorongoro Heroes ambao ni wenyeji dhidi ya Uganda ambao walishinda mabao 3-1 dhidi ya Kenya kwenye mchezo wa nusu fainali ya kwanza iliyochezwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu. Afcon ya vijana inatarajiwa kufanyika nchini Mauritania mwakani, ambapo kupitia michuano ya Cecafa inayoshirikisha timu za Afrika Mashariki na Kati Ngorongoro Heroes imepata tiketi hiyo. Nahodha wa Ngorongoro Heroes, Kelvin John amesema kuwa ushindi ambao waliupata jana ni zawadi kwa mashabiki hivyo watapambana kesho kupata ushindi mbele ya Uganda kwenye hatua ya fainali.

MSHAMBULIAJI SIMBA AFUNGUKIA ISHU YAKE YA KUTUA YANGA

Image
  IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba, Charlse Ilanfya yupo kwenye hesabu za kutolewa kwa mkopo ndani ya kikosi hicho kinachonolewa na Sven Vandenbroeck huku timu yake ya zamani ya KMC ikitajwa kuwa miongoni mwa zile ambazo zinamhitaji pamoja na Yanga. Ilanfya ambaye kabla ya kuibukia ndani ya Simba kwenye usajili wa dirisha kubwa msimu huu alikuwa kwenye hesabu za kutua Yanga msimu wa 2018/19 kabla ya dili lake kubuma na kuibukia ndani ya KMC na sasa yupo zake Simba. Habari zinaeleza kuwa kutokana  na kuwekwa benchi ndani ya Simba kwa kuwa nafasi anayocheza ina washambuliaji tengemeo ambao ni John Bocco na Meddie Kagere amekuwa akiishia benchi. Kwenye mechi 11 ambazo Simba imecheza ameanza kikosi cha kwanza mechi moja ilikuwa mbele ya Tanzania Prisons jambo ambalo linamfungulia njia ya kuomba kutoka kwa mkopo.  Ilanfya kuhusu jambo hilo amesema kuwa:”Bado sijapata taarifa rasmi na kuhusu kuomba kuondoka kwenda KMC ama Yanga hilo siwezi kulizingumzia kwa sasa,” . Msimu uliopita akiwa

JKT TANZANIA YAKWAMA KUSEPA NA POINTI TATU NDANI YA DAKIKA 450

Image
  KIKOSI cha JKT Tanzania kipo kwenye wakati mgumu kwa sasa baada ya kushinda mbele ya Mwadui FC kwa mabao 6-1 kimekwama kupata ushindi kwenye mechi zake tano ambazo ni dakika 450 mfululizo zaidi ya kuambulia sare mbili na kupata vipigo mechi tatu. Chini ya Kocha Mkuu, Abdalah Mohamed, ‘Bares’ kikosi kimecheza mechi 13, kimeshinda mechi mbili huku kikipoteza mechi saba na kutoa sare nne kipo nafasi ya 16 na pointi zake 10 kibindoni. Mara ya mwisho kushindi ilikuwa ni Oktoba 25, mbele ya Mwadui 1-6 JKT Tanzania Uwanja wa Mwadui Complex baada ya hapo mechi zake zinazofuata mambo yamekuwa magumu. Adam Adam mshambuliaji namba moja wa kikosi cha JKT Tanzania aliweka rekodi ya kuwa mshambuliaji wa kwanza kufunga hat trick ndani ya ligi kwa msimu wa 2020/21 ana jumla ya mabao sita. Mambo yalikuwa namna hii baada ya kupata ushindi wake wa pili mbele ya Mwadui:-Oktoba 30, JKT Tanzania 1-1 Azam FC, Uwanja wa Azam Complex. Novemba 4, Namungo 2-2 JKT Tanzania, Uwanja wa Majaliwa. Novemba 21

SAFU YA USHAMBULIAJI YANGA YAMLIZA KAZE

Image
  LICHA ya kupata ushindi kwenye mechi zake mbili mfululizo na kusepa na pointi sita zote mbele ya Azam FC, Novemba 25 na mbele ya JKT Tanzania, Novemba 28 kwa ushindi wa bao mojamoja, Kocha Mkuu wa Yanga, Cedric Kaze amesema kuwa tatizo linalomuumiza ni ubutu wa washambuliaji wake. Ikiwa ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 13 na kibindoni ina pointi 31 imefunga mabao 15 ndani ya dakika 1,170 ikiwa na wastani wa kufunga bao moja kila baada ya dakika 78. Kinara wa utupiaji wa mabao ndani ya kikosi hicho ni mshambuliaji wake namba moja Michael Sarpong mwenye mabao matatu. Akizungumza na Saleh Jembe, Kaze amesema kuwa kwa sasa kinachoisumbua safu yake ya ushambuliaji ni kushindwa kumalizia nafasi ambazo wanazitengeneza ndani ya uwanja. “Kwenye mechi zetu ambazo tunacheza huwa tunatengeneza nafasi nyingi ila wachezaji wangu wengi wanashindwa kuzitumia jambo ambalo inapaswa lifanyiwe kazi haraka. “Kupata pointi tatu ni jambo la msingi ila ni muhimu pia kupata mabao mengi ili

DAKTARI WA MARADONA AFANYIWA UCHUNGUZI KUHUSIKA NA KIFO GWIJI HUYO

Image
  WAENDESHA mashitaka nchini Argentina wanamchunguza daktari wa  Diego Maradona, Leopoldo Luque, wakimshuku kwa kuua kufuatia kifo cha nyota huyo wa soka kilichotokea Novemba 25 mwaka huu.   Polisi mjini Buenos Aires wameisaka nyumba na kliniki ya daktari huyo huku wakijaribu kubaini iwapo ulikuwepo uzembe katika matibabu baada ya upasuaji aliofanyiwa Maradona. Maradona ambaye alikuwa na umri wa miaka 60 alifariki dunia kutoka na shinikizo la damu nyumbani kwake ambako alikuwa akiendelea kupona baada ya kufanyiwa upasuaji.   Polisi wanashuku kwamba nyota huyo wa soka aliruhusiwa  kwenda nyumbani  kwake akiwa bado hajatimiza  masharti ya  kumruhusu atoke hospitalini, ikiwemo kupewa wauguzi au nesi wa kumhudumia saa 24, wataalamu wa uraibu, kupewa daktari anayeweza kumuita wakati wowote na gari la kubebea wagonjwa lenye vifaa vya kumsaidia kupumua.   Maafisa wanataka kufahamu kuhusu uhusika wa daktari Luque katika mipango ya kupona kwa Maradona katika nyumba ya nyota huyo.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMANNE

Image
  MUONEKANO wa ukurasa wa mbele Gazeti la SPOTI XTRA Jumanne,  nakala yake ni jero tu usikubali kukosa nakala yako

BIASHARA UNITED YAGAWANA POINTI MOJAMOJA NA AZAM FC KARUME, MARA

Image
 KIKOSI cha Biashara United, wanaopenda kujiita Wanajeshi wa mpakani leo Novemba 30 wamelazimisha sare ya kufungana bao 1-1 dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Karume. Biashara United chini ya Kocha Mkuu, Francis Baraza imekubali kugawana pointi mojamoja na Azam FC. Azam FC inabidi wajilaumu wenyewe kwa kushindwa kupata ushindi kwenye mchezo wa leo kwa kuwa walianza kufunga dakika 20 kupitia kwa Ayoub Lyanga. Bao hilo lilidumu mpaka kipindi cha pili ambapo Biashara United iliweka usawa dakika ya 58 kupitia kwa Thomas Omwenga aliyepiga shuti kali akiwa nje ya 18. Sare hiyo inafanya Azam FC kufikisha pointi 26 baada ya kucheza mechi 13 ikiwa nafasi ya tatu na Biashara United inafikisha jumla ya pointi19 baada ya kucheza mechi 13. Pia Biashara United ilikosa penalti kupitia kwa Leen Kissu ambaye amesema kuwa ilikuwa bahati mbaya.

NGORONGORO HEROES YATINGA FAINALI YA CECAFA KWA MBINDE

Image
TIMU ya Taifa ya Tanzania ya Vijana chini ya umri wa miaka 20, Ngorongoro Heroes leo Novemba 30 imetinga hatua ya fainali ya mashindano ya Cecafa kwa mbide baada ya kupata ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Sudani Kusini. Mchezo wa leo ambao umechezwa Uwanja wa Black Rhino Academy Karatu ulishuhudia dakika 45 timu zote mbili zikienda kwenye vyumba vya kubadilishia nguo zikiwa zimetoshana nguvu. Iliawachukua Ngorongoro Heroes dakika 10 kupata bao la uongozi kupitia kwa Kassim Haruna aliyepachika bao hilo dakika ya 55 baada ya beki wa Ngorongoro, David Kameta kutoa pasi kati iliyokutana na Kelvin John aliyeachia shuti likakutana na kipa aliyetema mpira uliokutana na Haruna.

YANGA YAGOMA KUSHUKA NAFASI YA KWANZA NDANI YA LIGI KUU BARA

Image
 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa malengo yao ni kubaki nafasi ya kwanza ndani ya Ligi Kuu Bara mpaka mzunguko wa pili utakapomeguka ili watimize malengo yao ya kutwaa ubingwa. Yanga ipo nafasi ya kwanza baada ya kucheza mechi 13 imekusanya jumla ya pointi 31 na haijapoteza mchezo ndani ya ligi zaidi ya kuambulia sare nne. Ushindi wake mfululizo kwa mechi mbili na mabao yao mawili umeifanya izidi kujijengea ufalme kileleni huku Deus Kaseke akiibuka shujaa kwenye mechi zote mbili mfulukizo ilikuwa mbele ya Azam FC Uwanja wa Azam Complex na mbele ya JKT Tanzania Uwanja wa Mkapa. Mechi zote mbili Kaseka alitupia bao mojamoja na kuipa timu yake pointi tatu mazima ambazo zimewafanya wajikite kileleni. Ofisa uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema:"Sisi ni Wananchi, hatuna presha na kile ambacho tunakifanya zaidi ya kuongeza juhudi ili kupata matokeo chanya. "Kwa namna ambavyo tunafanya malengo yetu ni kuona kwamba tunabaki kileleni mpaka mzunguko wa pili utakapokamil

UGANDA YATINGA FAINALI CECAFA

Image
  KIKOSI cha timu ya Taifa ya Uganda chini ya miaka 20 leo Novemba 30 kimetinga hatua ya fainali ya mashindano ya Cecafa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1. Mchezo wa leo ambao umechezwa Uwanja wa Black Rhino Academy kipindi cha kwanza kilikamilika Uganda wakiwa mbele kwa mabao 2-0. Mabao ya Uganda yalifungwa na Kenneth Semakula dk ya 23 na Avian Bogere aliyefunga mabao mawili dk ya 26 na 64. Lile la Kenya lilifungwa na Enock Wanyama dakika ya 81. Ushindi wa Uganda unawafanya wamsubiri mshindi wa mechi kati ya Tanzania ambao ni wenyeji v Sudani ya Kusini utakaochezwa saa tisa na nusu Uwanja wa Black Rhino Academy.  Fainali itachezwa Desemba 2.

USHINDI MBELE YA WANAIGERIA WAIPA MATUMAINI SIMBA KUTUSUA KIMATAIFA

Image
 UONGOZI wa Simba umesema kuwa kwa namna ambavyo wameanza kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya mabingwa baada ya kushinda jana, Novemba 29 bao 1-0 mbele ya Plateau United wana imani watafika hatua ya makundi. Kikosi hicho kinachonolewa na Sven Vandenbroeck kesho kinatarajiwa kuwasili Bongo baada ya kumaliza dakika 90 za mwanzo wakiwa ugenini nchini Nigeria wana dakika 90 nyingine Uwanja wa Mkapa. Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, ambapo Simba inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili iweze kusonga mbele ila ikifungwa itakuwa na kibarua kizito cha kupata ushindi ikiwa, itafungwa bao moja zitaongezwa dakika na mshindi asipopatikana ngoma itakwenda matuta kwa kuwa itakuwa ni 1-1.   Mtendaji Mkuu wa Klabu ya Simba, Barbara Gonzalez amesema kuwa ushindi ambao wameupata na namna mazingira yalivyokuwa magumu yanawapa nafasi ya kupata matokeo mazuri na kupenya hatua ya makundi. "Tumeanza vizuri na ni matumaini yetu kwamba ni Mungu amejibu maombi yetu hivyo kwa nam

NUSU FAINALI KOMBE LA CECAFA NI MWENDO WA REKODI TU

Image
  LEO macho na maskio ya mashabiki wa mpira Bongo kwa muda vitaweka nguvu kubwa Arusha ambapo mashindano ya Cecafa kwa timu za taifa chini ya miaka 20 yanafanyika ambapo ni hatua ya nusu fainali. Michauano hiyo ilianza Novemba 22 na inatarajiwa kumalizika Desemba 2 kwa fainali kuchezwa kwa wale watakaoshinda leo mchezo wa hatua ya nusu fainali. Tanzania inawakilishwa na timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20 Ngorongoro Heroes ambao mwendo wao unaleta matumaini ya timu hiyo kufanya vizuri ikiwa itaendelea na morali ya kupambana. Hapa ni namna mambo yalivyokuwa twende sawa:- Safari yao Mechi ya ufunguzi ilichezwa Novemba  22 ambapo Ngorongoro Heroes ilifungua kwa kishindo kwa ushindi wa mabao 6-1 Uwanja wa Black Rhino, Karatu, Arusha kwa kuwashushia kichapo hicho timu ya Taifa ya Djibout. Watupiaji kwa Tanzania ilikuwa ni Tepsi Theonasy,Abdul Hamis aliyefunga mabao matatu wengine ni Kheleffin Hamdoun na Kassim Haruna hawa walifunga bao mojamoja na lile la kufutia machozi kwa D

AZAM FC: SIO KIPIGO CHA YANGA TU, TIMU ILIKUWA HAICHEZI MPIRA UNAOELEWEKA

Image
  UONGOZI wa Azam FC umeweka wazi kuwa haukuwa na sababu ya kuendelea na Kocha Mkuu Aristica Cioaba raia wa Romania kwenye benchi lao la ufundi kwa kuwa alikuwa anawatoa kwenye reli ya kutwaa ubingwa. Cioaba ambaye ana tuzo ya kocha bora kwa mwezi Septemba na jina lake pia liliingia kwenye fainali ya kumsaka kocha bora wa mwezi Oktoba iliyopo mikononi mwa Cedric Kaze wa Yanga, alifutwa kazi  Novemba 26 kwa kile kilichoelezwa kuwa mwendo mbovu wa timu. Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa kupoteza kwao mbele ya Yanga kwa kufungwa bao 1-0 Novemba 25 sio sababu ya Cioaba kufutwa kazi bali matokeo mabovu yaliyokuwa yanaitoa timu kwenye reli ni sababu kuu ya kufutwa kwake kazi. “Unajua wengi wanadhani kwamba Aristica Cioaba amefutwa kazi kwa sababu ya kufungwa na Yanga, hapana haipo hivyo hata kidogo, tuligundua kwamba timu inatoka kwenye reli hasa tukiwa na lengo la kutwaa ubingwa mambo yanakwenda tofauti. “Kwa timu yenye malengo kila baad

SIMBA YAANZA SAFARI KUREJEA DAR KUWAVUTIA KASI WAZEE WA FIGISUFIGISU

Image
KLABU ya Simba leo Novemba 30 inataraja kuanza safari ya kurejea Tanzania wakitokea nchini Nigeria ambapo walikuwa kwenye majukumu ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika. Licha ya kuwekewa vigingi vingi kwenye mchezo wa jana wakiwa ugenini Simba ilipambana na kupata matokeo hivyo ina kazi ya kufanya kwenye mchezo wa marudio ili iweze kusonga mbele. Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateau United ya Nigeria kwenye mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa New Jos. Safari itaanza alfajiri kutoka Jos hadi Abuja, mchana kikosi kitaondoka Abuja kwenda Addis Ababa, Ethiopia ambapo kitafika usiku na kupumzika hapo.  Kikosi kinatarajia kutatua Tanzania kupitia Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro siku ya Jumanne, Desemba Mosi, saa 10:00 jioni. Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, Uwanja wa Mkapa, na bao la ushindi kwa Simba lilifungwa na Clatous Chama dakika ya 53.

NGORONGORO HEROES KAZINI LEO HATUA YA NUSU FAINALI

Image
  KOCHA Mkuu wa Timu ya Taifa ya Vijana chini ya miaka 20, Ngorongoro Heroes,  Jamhuri Kihwelo amesema kuwa anaamini vijana watafanya vizuri leo Novemba 30 kwenye mchezo dhidi ya Sudan Kusini. Mchezo wa leo ni hatua ya nusu fainali michuano ya Cecafa ambayo inafanyika Arusha,Tanzania ikiwa ni wenyeji. Khiwelo amesema :"Tulicheza mechi nyingi za kirafiki kwa ajili ya maandalizi na sasa tupo kwenye hatua ngumu tupo tayari kupata ushindi, imani yetu ni kwamba tutafikia lengo letu. "Mashindano ni magumu licha ya kwamba tulifanikiwa kushinda mechi mbili mpaka kufika hapa, kikubwa ni kwamba tunajua tuna mzigo mkubwa na mzito kwa ajili ya kufikia kile ambacho tunakihitaji. "Ushirikiano umekuwa mkubwa kutoka kwa viongozi mpaka mashabiki hili linatupa nguvu ya kufanya vizuri katika mchezo wetu," . Mchezo wa leo utachezwa Uwanja wa Black Rhino, Karatu,Arusha.

MSHAMBULIAJI WA SIMBA AIPIGIA HESABU YANGA

Image
  IMEELEZWA kuwa nyota wa Simba Charles Ilanfya yupo kwenye hesabu za kutua ndani ya Klabu ya Yanga kwa mkopo. Habari zinaeleza kuwa hatua hiyo imefikia baada ya nyota huyo kuomba ruhusa ya kusepa kwa mkopo ndani ya timu hiyo inayonolewa na Sven Vandenbroeck kutokana na ugumu wa namba. Akiwa Simba ambapo alijiunga hapo akitokea Klabu ya KMC amecheza mchezo mmoja wa Ligi Kuu Bara na hakuyeyusha dakika zote 90 ilikuwa dhidi ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela. Nyota huyo ameomba kurejea KMC ikiwa mambo yatakuwa magumu basi anaweza kwenda Yanga ambao walikuwa kwenye hesabu za kuipata saini yake msimu wa 2018/19 kabla hajaibukia KMC zama zile akiwa ndani ya Mwadui FC. "Ilanfya ameona kwamba mambo ni magumu ndani ya Simba hivyo ameomba kuondoka akapate nafasi ya kucheza kwa kuwa hapati ndani ya kikosi hiki. "Timu ya kwanza anayofikiria ni KMC na ya pili ni Yanga ambao walikuwa wanahitaji saini yake zamani, " ilieleza taarifa hiyo. Ofisa Habari wa KMC,

AZAM FC KAMILI GADO KUIVAA BIASHARA UNITED

Image
 LEO kikosi cha Azam FC kitakuwa na kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United mchezo utakaochezwa Uwanja wa Karume, Mara. Huu unakuwa ni mchezo wa kwanza kwa kaimu kocha mkuu, Vivier Bahati kukaa kwenye benchi la ufundi baada ya Aristica Cioaba kufutwa kazi Novemba 26. Akizungumza na Saleh Jembe, Bahati amesema kuwa maandalizi yapo sawa na wana amini kwamba watapata matokeo chanya mbele ya wapinzani wao Biashara United. "Maandalizi yapo sawa hivyo imani yetu ni kuona kwamba timu inapata matokeo chanya ambayo yatatufanya turejee kwenye ramani. "Kukosa matokeo kwenye mechi zetu zilizopita kwetu ni darasa hivyo mashabiki watupe sapoti tunaamini tutafanya vizuri," amesema. Azam FC ilipoteza michezo miwili mfululizo ndani ya ligi kwa kufungwa mabao mawili ndani ya dakika 180 ikiwa ugenini na nyumbani. Ilifungwa bao 1-0 na KMC Uwanja wa Uhuru na ilifungwa na Yanga bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex. Ikiwa imecheza mechi 12 imekusanya pointi 25 na kinar

CAVAN AFANYA YAKE AIBEBA UNITED AKITOKEA BENCHI

Image
 MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Manchester United, Edinson Cavan, jana Novemba 29 aliingia akitokea benchi na kutupia mabao mawili  na kuifanya Manchester United kushinda mabao 3-2 dhidi ya Southampton ikiwa ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Nyota huyo raia wa Uruguay aliingia dakika ya 45 kipindi cha pili akichukua nafasi ya Mason Grennwood  na alifunga mabao hayo mawili na kutoa pasi moja ya bao. Manchester United ilikwenda mapumziko ikiwa imefungwa mabao 2-0 ila kipindi cha pili ilipindua meza kibabe. Bruno alifunga bao dakika ya 59 kwa pasi ya Cavan na yeye alipachika mabao dakika ya 74 na 90+2.

SVEN: TUNA KAZI NGUMU YA KUFANYA KIMATAIFA

Image
 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa licha ya kushinda mchezo wa kwanza kwenye Ligi ya Mabingwa hatua ya awali bado kazi haijaisha lazima wajiweke sawa kwa ajili ya mchezo wa marudio. Jana, Novemba 29, Simba ilishinda bao 1-0 dhidi ya Plateau United kwenye mchezo wa awali ya Ligi ya Mabingwa nchini Nigeria uliochezwa Uwanja wa New Jos. Bao la ushindi lilifungwa na nyota Clatous Chama dakika ya 53 kwa pasi ya kiungo mwenzake Luis Miquissone. Sven amesema:"Wapinzani wetu wana nguvu na walijaribu kiufundi kutafuta goli lakini walishindwa kutokana na uimara wa wachezaji wangu katika hilo ninawapongeza.  "Matokeo tuliyopta ni mazuri lakini bado hatujamaliza kazi kwa sababu wiki ijayo tuna dakika 90 zingine." amesema. Mchezo wa marudio kwa timu hizi unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, Uwanja wa Mkapa na Simba inahitaji ushindi ama sare ya aina yoyote ili isonge mbele hatua ya mtoano.

BEKI WA KULIA WA YANGA KIBWANA SHOMARI ATOA KAULI YA MATUMAINI

Image
 BEKI wa kulia wa Klabu ya Yanga, Kibwana Shomari amesema kuwa kwa sasa anaendelea vizuri hivyo ana matumaini ya kurejea uwanjani hivi karibuni. Kibwana alipata majeraha ya bega wakati timu yake ilipokuwa ikisaka pointi tatu mbele ya Azam FC, Uwanja wa Azam Complex. Mchezo huo uliochezwa Novemba 25, Yanga ilishinda bao 1-0 lililopachikwa kimiani na Deus Kaseke. Kibwana hakuweza kumaliza dakika zote 90 alitolewa nje ili kupewa huduma ya kwanza. Kibwana amesema:"Kwa sasa ninaendelea vizuri na nina amini kwamba nitareja uwanjani hivi karibuni kuendelea na kazi ya kusaka ushindi kwa ajili ya timu yangu. "Matibabu ambayo nimepata yananifanya nizidi kuwa imara zaidi hivyo ni suala la kuendelea kuomba dua na kusubiri muda nitakaporudi uwanjani namna hali iakavyokuwa," amesema. Yanga ni vinara wa Ligi Kuu Bara wakiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13 hawajapoteza mchezo wanafuatiwa na Azam FC ambayo imecheza mechi 12 ikiwa nafasi ya pili na pointi 25.

SIMBA YAPENYA MBELE YA WANAIGERIA LICHA YA VIKWAZO

Image
  KIKOSI cha Simba, leo Novemba 29 kimeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya wenyeji wao Plateau United kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa Afrika.  Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa New Jos, nchini Nigeria wenye uwezo wa kuchukua jumla ya mashabiki 40,000 ulikuwa na visa vingi kwa wenyeji wakiwa na lengo na kuwatoa Simba mchezoni. Bao la ushindi limepatikana dakika ya 53 kupitia kwa Clatous Chama kwa pasi ya Luis Miquissone ambaye alikuwa ni mwiba kwa Plateau United. Miongoni mwa vikwazo ambavyo walikuwa wanaweka watu wa Nigeria ni pamoja na kuwabugudhi waandishi wa Habari wa Tanzania katika kufanya ripoti ya matukia. Pia jana, Novemba 28 licha ya jitihada za uongozi wa Simba kuomba matangazo yarushwe mubashara kupitia Azam Tv jamaa waligoma na kuweka ngumu mpaka leo siku ya mchezo Azam Tv hawakupewa haki ya kutangaza mubashara zaidi ya kutangaza kupitia kwa radio. Habari nyingine ni kwamba Simba walipigwa mkwara kwenye upande wa kutumia wapishi wao mwanzo na kuleta u

OLE GUNNER: FERNANDES KAMA RONALDO

Image
  OLE Gunnar Solskjaer, Kocha Mkuu wa Manchester United amesema kuwa nyota wake Bruno Fernandes ni kama Cristiano Ronaldo.  Hivi karibuni baada ya nyota huyo kufanya vizuri ndani ya United amekuwa akifananishwa na Ronaldo ambaye aliwahi kuitumikia timu hiyo na wote ni raia wa Ureno. Fernandes amefunga jumla ya mabao 21 katika mechi 35 ndani ya United tangu atue hapo Januari mwaka huu akitokea Sporting Lisbon na ana jumla ya asisti 15. Solskjaer amesema:"Fernandes ni kama Ronaldo yeye amekuwa msaada mkubwa kwa wachezaji kuwahamasiha wapambane zaidi wakiwa ndani ya uwanja hilo ni jambo nzuri," .

LIGI YA MABINGWA: PLATEAU UNITED 0-0 SIMBA

Image
 Uwanja wa New Jos Ligi ya Mabingwa Afrika Novemba 29, hatua ya awali Kipindi cha kwanza Plateau United 0-0 Simba Dakika ya 39, Dilunga anachezewa faulo Dakika ya 38 Plateau wanakosa nafasi ya kuifunga Simba Dakika ya 35 Onyango anapewa huduma ya kwanza Dakika ya 34 Onyango anaokoa hatari  Dakika ya 33 Mlinda mlango wa Plateau Abubakari Adam anaokoa hatari Dakika ya 32 Manula anaokoa hatari Dakika ya 31 Luis anaokoa hatari iliyokuwa inamfuata Manula Dakika ya 30 Plateau wanapeleka mashambulizi kwa Manula Dakika ya 29 Onyango anaokoa hatari Dakika ya 27 Abha Omari anapelekea mashambulizi kwa Manula Dakika ya 25 Plateu United wanarusha mpira kuelekea kwa Simba Dakika ya 20 Manula anachezewa faulo Dakika ya 18 Plateau wanapiga kona haileti matunda Dakika ya 17 Luis anacheza faulo Dakika ya 16 Jonas Mkude anachezewa faulo Dakika ya 15 Kapombe anampa pasi Bocco Dakika ya 13 Plateu United wanapiga kona haizai matunda Dakika ya 10 Manula anaokoa hatari langoni mwake 

ZIDANE: NILIMWAMBIA MARADONA KWAMBA NI MCHEZAJI BORA

Image
  ZINADINE Zidane, Kocha Mkuu wa Real Madrid amesema kuwa alipata bahati ya kuzungumza na Diego Maradona na alimwambia kwambe yeye ni aina ya wachezaji bora ndani ya uwanja. Zidane amesema kuwa taarifa za kutangulia mbele za haki kwa gwiji huyo zilimshtua na kumfanya afikirie mambo mengi kuhusu uwezo wa Maradona. Maradona alitangulia mbele za haki Novemba 25 akiwa nyumbani, Argentina ikiwa ni muda mfupi baada ya kutimiza miaka 60. Zidane amesema:"Hakuwa mtu mwenye maneno mengi ila utendaji zaidi, nilipata bahati ya kuzungumza naye na nilimuambia kwamba yeye ni mchezaji bora na mwenye uwezo ndani ya uwanja. "Kwa kuwa ametangulia basi hakuna namna imani ni kwamba uwezo wake utadumu kwenye mioyo ya wanafamilia ya michezo," .

KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA PLATEAU UNITED

Image
  KIKOSI cha Simba kitakachoanza leo Novemba 29 dhidi ya Plateau United,  Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali

SOKA LA AFRIKA NA UPUUZI WA KIPUUZI

Image
Anaandika Saleh Jembe  NAJARIBU kujiuliza maswali rundo lakini jibu ni moja tu kuwa mpira wa Afrika na hasa sisi chini ya Jangwa la Sahara umejaa upuuzi wa kipuuzi ambao unafanana sana. Ishu yangu ni kuona Plateau United FC kuzuia mechi isionyeshwe LIVE kwa kuwa wana haki hiyo. Swali la kwanza wanajua ni kipindi cha Covid 19 Pili wanajua mashabiki wao wangependa kuwaona wakipambana na Simba Tatu, runinga ni mapato na matangazo ya wachezaji.  Hakuna anayeshiriki kuendesha timu ya soka atasema hahitaji fedha. Wakati mwingine unajiuliza hivi Plateau wanataka KUIDHULUMU Simba hadi wanakubali kupoteza kila kitu? WANATAKA KUWANYONGA SIMBA? Nafikiri ni akili za hovyo na hata hazistahili kujadiliwa na inaonyesha kiasi gani soka la Nigeria ni UBABAISHAJI wa kiwango cha juu kupitiliza. Wanigeria wanaoiogopa Simba kiasi hiki hadi kufanya mambo ya KIPUUZI kiasi hiki.

KIKOSI CHA SIMBA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA PLATEAU UNITED

Image
  KIKOSI cha Simba kitakachoanza leo Novemba 29 dhidi ya Plateau United,  Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya awali

SIMBA YATAJA NAMNA ITAKAVYOWAVAA WANIGERIA LEO

Image
 SVEN Vandenbroeck, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa ataanza mchezo wa leo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Plateau United kwa kuwekeza nguvu kubwa kwenye ulinzi kabla ya kushambulia. Simba ipo ndani ya mji wa Jos ambapo saa 12:00 jioni itakuwa ndani ya Uwanja wa New Jos kusaka ushindi kwenye mchezo wa awali wa Ligi ya Mabingwa na ule wa marudio unatarajiwa kuchezwa kati ya Desemba 4-9, Uwanja wa Mkapa.  Kocha huyo raia wa Ubelgiji ameongeza kuwa malengo ya kuanza kujilinda ni kuwasoma wapinzani wake ili ajue mbinu za kuwavuruga zitakazomfanya ajue uimara wao pamoja na udhaifu ndani ya uwanja.  Uwanja wa Jos una uwezo wa kuchukua mashabiki 40,000 ila hawatakuwepo ndani ya Uwanja kwa kuwa Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) limetoa muongozo wa kutaka mechi zichezwe bila ya mashabiki kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.  "Tutaanza na kuimarisha ulinzi mwanzo ili tujue uimara na mapungufu ya wapinzani wetu, tunatambua kwamba mchezo utakuwa mgumu ila tuta

MAPOKEZI YA MTAMBO WA MABAO YANGA NI NOMA

Image
 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umeandaa jezi zaidi ya 100 kwa ajili ya mapokezi ya mshambuliaji wao mpya Said Ntibazonkiza ambaye anatarajiwa kutua Bongo hivi karibuni. Habari zinaeleza kuwa Said anatarajiwa kuwasili Bongo kesho kuungana na wachezaji wenzake kwa kuwa alikuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Burundi.  Nyota huyo raia wa Burundi ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Cedric Kaze alisaini dili la miaka miwili. Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa nyota huyo anaweza kujiunga na wachezaji wenzake kambini kwa kuwa maandalizi yamekamilika. "Tumeweka maandalizi kwa ajili ya kuweza kumpokea Said ambaye yupo zake Burundi tayari tumeandaa zaidi ya jezi 100 zenye majina yake hivyo itakuwa kazi rahisi kwake kujua namna gani tunatambua mchango wake na namna ambavyo mashabiki wanamkubali. "Pia anatambua kwamba anakuja kwenye timu ya Wananchi ambao wanahitaji matokeo chanya kama ambavyo kwa sasa tunafa

AZAM FC YAZIPIGIA HESABU POINTI TATU ZA BIASHARA UNITED

Image
 AZAM FC kesho itakuwa Uwanja wa Karume, Mara kusaka pointi tatu mbele ya Biashara United. Ikiwa chini ya kocha msaidizi, Vivier Bahati ambaye amepewa mechi mbili ataanza kumaliza dakika zake 90 kesho kabla ya kumaliza na Gwambina FC. Bahati amepewa mechi hizo baada ya Aristica Cioaba kufutwa kazi Novemba 26 kutokana na kile kilichoelezwa matokeo mabovu ndani ya timu. Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Azam FC Zakaria Thabit amesema kuwa maandalizi yapo sawa na kila mmoja yupo tayari kusaka pointi tatu muhimu. "Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Biashara United ni matumaini yetu kwamba tutafanya vizuri na kupata pointi tatu ili turejee kwenye ubora wetu," amesema. Azam FC inashuka uwanjani ikiwa na kumbukumbu ya kupoteza mechi mbili mfululizo, ilianza kupoteza mbele ya KMC kwa kufungwa bao 1-0 Uwanja wa Uhuru na ikapoteza mbele ya Yanga kwa kufunga bao 1-0 Uwanja wa Azam Complex. Kwenye msimamo ipo nafasi ya pili baada ya kucheza mechi 12 ime