SIMBA YAANZA SAFARI KUREJEA DAR KUWAVUTIA KASI WAZEE WA FIGISUFIGISU
KLABU ya Simba leo Novemba 30 inataraja kuanza safari ya kurejea Tanzania wakitokea nchini Nigeria ambapo walikuwa kwenye majukumu ya kuiwakilisha Tanzania kwenye mchezo wa kimataifa wa Ligi ya Mabingwa Afrika.
Licha ya kuwekewa vigingi vingi kwenye mchezo wa jana wakiwa ugenini Simba ilipambana na kupata matokeo hivyo ina kazi ya kufanya kwenye mchezo wa marudio ili iweze kusonga mbele.
Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Sven Vandenbroeck iliibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Plateau United ya Nigeria kwenye mchezo wa awali uliochezwa Uwanja wa New Jos.
Kikosi kinatarajia kutatua Tanzania kupitia Uwanja wa ndege wa Kilimanjaro siku ya Jumanne, Desemba Mosi, saa 10:00 jioni.
Mchezo wa marudio unatarajiwa kuchezwa Desemba 5, Uwanja wa Mkapa, na bao la ushindi kwa Simba lilifungwa na Clatous Chama dakika ya 53.
Comments
Post a Comment