UGANDA YATINGA FAINALI CECAFA

 


KIKOSI cha timu ya Taifa ya Uganda chini ya miaka 20 leo Novemba 30 kimetinga hatua ya fainali ya mashindano ya Cecafa baada ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-1.

Mchezo wa leo ambao umechezwa Uwanja wa Black Rhino Academy kipindi cha kwanza kilikamilika Uganda wakiwa mbele kwa mabao 2-0.

Mabao ya Uganda yalifungwa na Kenneth Semakula dk ya 23 na Avian Bogere aliyefunga mabao mawili dk ya 26 na 64.

Lile la Kenya lilifungwa na Enock Wanyama dakika ya 81. Ushindi wa Uganda unawafanya wamsubiri mshindi wa mechi kati ya Tanzania ambao ni wenyeji v Sudani ya Kusini utakaochezwa saa tisa na nusu Uwanja wa Black Rhino Academy. 


Fainali itachezwa Desemba 2.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO