MAPOKEZI YA MTAMBO WA MABAO YANGA NI NOMA


 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa umeandaa jezi zaidi ya 100 kwa ajili ya mapokezi ya mshambuliaji wao mpya Said Ntibazonkiza ambaye anatarajiwa kutua Bongo hivi karibuni.

Habari zinaeleza kuwa Said anatarajiwa kuwasili Bongo kesho kuungana na wachezaji wenzake kwa kuwa alikuwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Burundi. 

Nyota huyo raia wa Burundi ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga kinachonolewa na Cedric Kaze alisaini dili la miaka miwili.


Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa muda wowote kuanzia sasa nyota huyo anaweza kujiunga na wachezaji wenzake kambini kwa kuwa maandalizi yamekamilika.


"Tumeweka maandalizi kwa ajili ya kuweza kumpokea Said ambaye yupo zake Burundi tayari tumeandaa zaidi ya jezi 100 zenye majina yake hivyo itakuwa kazi rahisi kwake kujua namna gani tunatambua mchango wake na namna ambavyo mashabiki wanamkubali.


"Pia anatambua kwamba anakuja kwenye timu ya Wananchi ambao wanahitaji matokeo chanya kama ambavyo kwa sasa tunafanya, mashabiki wasiwe na mashaka kila kitu kuhusu kuja tutatoa taarifa," amesema.


Yanga ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo ikiwa na pointi 31 baada ya kucheza mechi 13 haijapoteza mchezo ndani ya ligi zaidi ya kuambulia sare nne.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA