SOKA LA AFRIKA NA UPUUZI WA KIPUUZI



Anaandika Saleh Jembe 

NAJARIBU kujiuliza maswali rundo lakini jibu ni moja tu kuwa mpira wa Afrika na hasa sisi chini ya Jangwa la Sahara umejaa upuuzi wa kipuuzi ambao unafanana sana.


Ishu yangu ni kuona Plateau United FC kuzuia mechi isionyeshwe LIVE kwa kuwa wana haki hiyo.


Swali la kwanza wanajua ni kipindi cha Covid 19

Pili wanajua mashabiki wao wangependa kuwaona wakipambana na SimbaTatu, runinga ni mapato na matangazo ya wachezaji. 

Hakuna anayeshiriki kuendesha timu ya soka atasema hahitaji fedha.


Wakati mwingine unajiuliza hivi Plateau wanataka KUIDHULUMU Simba hadi wanakubali kupoteza kila kitu? WANATAKA KUWANYONGA SIMBA?


Nafikiri ni akili za hovyo na hata hazistahili kujadiliwa na inaonyesha kiasi gani soka la Nigeria ni UBABAISHAJI wa kiwango cha juu kupitiliza.


Wanigeria wanaoiogopa Simba kiasi hiki hadi kufanya mambo ya KIPUUZI kiasi hiki.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA