CAVAN AFANYA YAKE AIBEBA UNITED AKITOKEA BENCHI


 MSHAMBULIAJI wa Klabu ya Manchester United, Edinson Cavan, jana Novemba 29 aliingia akitokea benchi na kutupia mabao mawili  na kuifanya Manchester United kushinda mabao 3-2 dhidi ya Southampton ikiwa ugenini kwenye mchezo wa Ligi Kuu England.


Nyota huyo raia wa Uruguay aliingia dakika ya 45 kipindi cha pili akichukua nafasi ya Mason Grennwood  na alifunga mabao hayo mawili na kutoa pasi moja ya bao.


Manchester United ilikwenda mapumziko ikiwa imefungwa mabao 2-0 ila kipindi cha pili ilipindua meza kibabe.


Bruno alifunga bao dakika ya 59 kwa pasi ya Cavan na yeye alipachika mabao dakika ya 74 na 90+2.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO