Posts

Showing posts from May, 2021

MANCHESTER CITY INAMUHITAJI KANE, GREALISH

Image
IMERIPOTIWA kwamba kutokana na anguko la kifedha kwa timu nyingi England kutakuwa na mabadilishano ya wachezaji kwenye dirisha la usajili ili timu kutimiza malengo yao. Hii imetokana na janga la Virusi vya Corona ambalo lilisababisha mechi nyingi kuchezwa bila mashabiki ili kuchukua tahadhari na hilo lilichangia kwa kiasi kikubwa uchumi kuyumba. Miongoni mwa wachezaji ambao wanatajwa kuwa kwenye mabadilishano hayo ni pamoja na nyota ambaye anatikisa kwa sasa kwenye suala la usajili ambaye ni Harry Kane anayewindwa na Manchester City ambayo ipo tayari kufanya naye mabadilishano na Gabriel Jesus pamoja na Nathan Ake ili wapate saini ya mshambuliaji huyo. Imeelezwa kuwa kuna makubaliano ambayo yanaweza kufikiwa kwa sasa na timu hizo mbili ambapo Kocha Mkuu wa City, Pep Guardiola anahitaji kuboresha kikosi chake na hesabu zake ni Kane na mshikaji wake Jack Grealish ambaye anacheza ndani ya Aston Villa. Jesus mwenye miaka 24 hajawa na bahati chini ya Guardiola hivyo anaweza kuondoka

VIDEO: BABU TALE AKWERWA NA NENO MARAIS NCHINI

Image
BABU Tale amesema kuwa neno Rais liwe moja maana kuna Marais wengi kwa sasa sijui Shirikisho, Wasafi.   

HATMA YA RAMOS REAL MADRD KUJULIKANA MWEZI HUU

Image
JUNI inaonekana kuwa itakuwa ni mwisho wa nyota wa kikosi cha Real Madrid, Sergio Ramos kufahamu kwamba atabaki ndani ya kikosi hicho ama atasepa mazima. Mkataba wa nahodha huyo ndani ya kikosi hicho unameguka mwezi huu na mpaka sasa hakuna dalili zozote za kuzungumzia mkataba huo. Ramos mwenyewe wala Madrid hakuna ambaye ametoa taarifa kuhusu ishu ya dili lake hivyo mwezi huu hatma yake itajulikana namna itakavyokuwa. Ramos alijiunga na timu hiyo 2005 na amekaa kwa zaidi ya miaka 15 na amefanikiwa kutwaa mataji 22 pia ana mataji matatu ya Ligi ya Mabingwa Ulaya.

VIDEO: DIAMOND AOMBEWA KURA BUNGENI, SIMBA NA YANGA ZATAJWA

Image
KIKOSI cha Simba chapongezwa bungeni kwa kutinga hatua ya robo fainali, pia wameshauri kwamba kanuni ya Caf waangalie namna ya kupanga timu shiriki, pia amewaomba Watanzania kumpigia kura Diamond  

VIDEO: KUHUSU CARLINOS KWENDA SIMBA, MANARA AJIBU

Image
BAADA ya nyota wa Yanga, Carlos Carlinhos kuamua kuvunja mkataba na timu yake ya Yanga kuna shabiki aliweka wazi kwamba nyota huyo anaweza kuibukia ndani ya Simba, jambo hilo halikuachwa hivihivi, Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara alijibu  

VIDEO:TARIMBA AZUNGUMZIA BUNGENI ISHU YA KUYEYUKA KWA DABI, UENDESHAJI HAURIDHISHI

Image
TARIMBA amesema kuwa kuna watu walichungulia kwenye darubini zao na kuona kwamba wanakwenda kupigwa mabao mengi jambo waliloamua kufanya mpango wa kubadili ratiba  

SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA CARLINHOS KUSAINI MKATABA KWAO

Image
 BAADA ya mabosi wa Yanga kutangaza kuachana na kiungo wao Carlos Carlinhos imekuwa ikielezwa kuwa huenda akaibukia ndani ya kikosi cha watani zao wa jadi Simba. Carlinhos raia wa Angola amekuwa akifanya vizuri ndani ya ligi ila amekuwa akisumbuliwa na majeraha jambo mablo limemfanya awe nje ya uwanja kwa muda mrefu. Ana pasi tatu za mabao na amefunga pia idadi hiyo ya mabao na kumfanya ahusike kwenye jumla ya mabao sita ambayo ndani ya Yanga kati ya 43 yaliliyofungwa na timu hiyo iliyo nafasi ya pili na pointi zake 61 baada ya kucheza jumla ya mechi 29. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa Carlinhos hawezi kucheza ndani ya Simba kwa sasa kwani hana uwezo wa kugombania namba katika kikosi hicho. "Carlinhos kucheza kwenye kikosi cha mabingwa haiwezekani,hilo haliwezi kutokea," amesema.

SUALA LA USAJILI WAACHIWE MAKOCHA, MAPAMBAO YAENDELEE

Image
 ORODHA ya wachezaji ambao  wataripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi kwa sasa ipo wazi. Kim Poulsen Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, yeye ametaja kikosi hicho kwa ajili ya kuanza maandalizi rasmi hivyo ni muhimu kwa wachezaji ambao wameitwa watimize majukumu yao kwa wakati. Kikubwa ambacho kinatakiwa ni wachezaji kutambua kwamba Watanzania wanahitaji kuona matokeo chanya kwa kila mchezo ambao watacheza. Kuwa katika mechi ya kirafiki na kupata matokeo mazuri ni nafasi ya kuweza kujenga hali ya kujiamini na kuwa na mwendo mzuri kwa wakati ujao. Baada ya kikosi kutajwa tunaona kwamba kila mtu anakuwa na chaguo lake akihitaji kuona baadhi ya wachezaji ambao anawapenda kuwa kwenye kikosi. Hilo la kuitwa ama kutoitwa libaki mikononi mwa kocha kwa sababu yeye anajua aina ya wachezaji ambao anawahitaji katika kikosi. Kwa kumuachia kocha suala la wachezaji itapunguza ile presha ambayo huwa inaanza kwa mashabiki. Kazi ya mashabiki iwe

BREAKING: YANGA WATHIBITISHA KUACHANA NA CARINHOS

Image
  BREAKING: Yanga wamethibitisha kuvunja mkataba na kiungo wao  Carlos Carlinhos raia wa Angola ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda akitibu majeraha yake ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons. Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa wamefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake kwa pande zote mbili kukaa chini. Pia Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi imemshukuru kiungo huyo kwa huduma yake ndani ya Yanga.  Taarifa hiyo imeeleza namna hii:-

VIDEO: MORRISON AMPIGIA SIMU BOSI GSM

Image
BAADA ya kufunga bao lake bora la msimu mbele ya Namungo, kiungo Bernard Morrison amempigia simu bosi wake wa zamani ishu ni suala la kesi yake ile ya utata wa mkataba.   

MUANGOLA WA YANGA AVUNJA MKATABA, ASEPA BONGO

Image
 IMEELEZWA kuwa  Kiungo mshambuliaji wa Yanga, Carlos Sténio Fernandes Guimarães do Carmo maarufu kama Carlinhos amevunja mkataba na klabu yake ya Yanga. Sababu ya nyota huyo kuamua kuvunja mkataba wake huo ni kutokana na matizo ya kifamilia jambo ambalo limefanya aombe kusepa. Pia nyota huyo alikuwa anasumbuliwa na majeraha jambo ambalo limemfanya ashindwe kuonyesha makeke yake kwenye mechi nyingi za ligi pamoja na Kombe la Shirikisho. Mchezo wake wa mwisho kuonekana uwanjani ilikuwa ni wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Nelson Mandela wakati ubao uliposoma Tanzania Prisons 0-1 Yanga. Alikuwa akitibu majeraha ya nyama za paja ambayo aliyapata kwenye mchezo huo na hakuweza kumaliza dakika zote 90.

HAKUNA MCHEZAJI KAMA KANTE

Image
MCHAMBUZI wa masuala ya michezo, Martin Samuel amesema kuwa hakuna mchezaji kama kiungo mkabaji, N'Golo Kante ambaye anacheza ndani ya kikosi cha Chelsea kinachonolewa na Kocha Mkuu, Thomas Tuchel kutokana na jitihada zake binafsi kwenye kutimiza majukumu yake. Kante ndani ya miaka mitano ya hivi karibuni ametwaa mataji sita huku akiwa katika ubora wake uleule. Kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Ulaya mbele ya Manchester City aliweza kukata umeme kwa asilimia 100 bila kusababisha hata faulo moja. Samuel amesema kuwa Kante ana nafasi ya kuweza kuingia kwenye vita ya kuwania tuzo ya Ballon d'Or kwa mwaka 2021 bila mashaka pamoja na Robert Lewandowski ambaye amefunga jumla ya mabao 20 katika mechi 48 msimu huu akiwa ndani ya Bayern Munich. Kante ameshinda Kombe la Dunia akiwa na timu yake ya Ufaransa, ameshinda taji la Ligi ya Mabingwa Ulaya, ameshinda taji la Europa na ana mataji mawili ya Ligi Kuu England pamoja na taji moja la FA akiwa chini ya makocha watano tofauti. S

VIDEO: YANGA KUSUKA UPYA KIKOSI CHAKE, KUNA BEKI MBENINI PIA AINGIA ANGA ZAO

Image
IMEELEZWA kuwa Yanga ipo kwenye hesabu za kusuka kikosi chake upya ikiwa ni pamoja na safu ya ushambuliaji, kwa sasa inaelezwa kuwa kuna mshambuliaji ambaye anacheza ndani ya Kaizer Chiefs, Kambole huenda akasajiliwa na Yanga msimu ujao. Pia inasaka beki ambaye atakuwa mbadala wa nahodha Lamine Moro  

VIDEO: OKWI KURUDI SIMBA, GOMES KUAMUA

Image
EMANUEL Okwi, mshambuliaji wa zamani wa kikosi cha Simba anatajwa kurejea tena ndani ya kikosi hicho msimu ujao kwa ajili ya kutumikia timu yake ya zamani  

VIDEO: MZEE WA IRUDIWEIRUDIWE ALIAMUA KUJA TOFAUTI, SAPOTI ANAPATA

Image
MC Mboneke mzee wa irudiwe, irudiwe kutoka Mbeya anasema kuwa yeye maisha yake yote ya elimu na kukua ilikuwa ni Mbeya akiwa na elimu ya kidato cha sita.  Kupitia kile ambacho amesoma amesema kuwa matokeo ambayo anayapata kupitia elimu yake ni fani yake ambayo anaifanya kwa sasa na aliamua kuja kwa mtindo huo ili kuwa tofauti.   

NYAKATI NGUMU, BOCCO NI MKOMBOZI, TANZANIA INAWAHITAJI WENGI ZAIDI

Image
  HUENDA ingekuwa si tatizo la majeraha ya mara kwa mara ambayo yanamuandama nahodha wa Simba, John Raphael Bocco, mshambuliaji pekee ambaye amefunga zaidi ya mabao 100 ndani ya Ligi Kuu Bara kwa sasa tungekuwa tunaimba wimbo mwingine. Bocco amekuwa ni nguzo ndani ya Simba nyakati ngumu wakati timu hiyo ikihitaji matokeo katika Ligi ya Mabingwa Afrika hata ndani ya ligi amekuwa na asili hiyo. Ukumbuke mchezo uliochezwa Uwanja wa Kambarage wakati ubao ukisoma Mwadui 0-1 Simba, alikuwa Bocco aliyeamua pointi tatu zikaenda kwao. Ikumbukwe pia wakati Simba ikipambana kuweza kuandika ndoto za kutinga hatua ya nusu fainali mbele ya Kaizer Chiefs ikiwa na mzigo wa mabao 4-0 ni Bocco alianzisha safari katika nyakati ngumu ila haikuwa bahati kwa Simba kwa kuwa aggregate kwa sasa inasoma Simba 3-4 Simba. Ukiachana na mchezo wa Mei 22, wakati ubao ukisoma Simba 3-0 Kaizer Chiefs na huku mabao hayo yakipachikwa dakika ya 24 na 56 huku lile la tatu likipachikwa na Clatous Chama dakika ya

MAJOGORO:TUTAPAMBANA KUPATA MATOKEO MECHI ZILIZOBAKI

Image
 NYOTA wa kikosi cha Mtibwa Sugar,Baraka Majogoro amesema kuwa watapamba akupata matokeo kwenye mechi zao zote zilizobaki ili kubaki ndani ya Ligi Kuu Bara. Chini ya Kocha Mkuu, Mohamed Badru ipo nafasi ya 11 ikiwa na pointi 34 baada ya kucheza mechi 30 na imebakiwa na mechi nne kukamilisha mzunguko wa pili utakaofunga msimu wa 2020/21 mazima. Akizungumza na Saleh Jembe, Majogoro amesema kuwa ushindani msimu huu ni mkubwa na kila timu ina presha ya kupata matokeo jambo ambalo linawafanya nao wapambane kwa hali na mali. “Kweli hatupo katika nafasi nzuri hasa ukizingatia kwamba pointi tulizo nazo pamoja na nafasi kwetu sio nzuri ambacho tutakifanya ni kupambana kushinda mechi zetu zote zilizobaki na inawezekana kikubwa mashabiki wazidi kutupa sapoti. "Ushindani ni mkubwa nasi tunapambana kupata pointi tatu kwa sasa hasa ukizingatia tupo kwenye lala salama na kila timu inahitaji pointi tatu," amesema. Majogoro. Mechi za Mtibwa Sugar ambazo zimebaki ni dhidi ya Mwadui F

SIMBA AKILI ZAKE KWA WAZEE WA MPAPASO

Image
DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anahitaji kuona wanashinda mbele ya Ruvu Shooting, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara. Kwa sasa Ruvu Shooting wao sera yao kubwa ni Mpapaso Square muasisi wake akiwa no Ofisa Habari wao Masau Bwire.   Ikumbukwe kwamba,  mchezo wa kwanza  walipocheza Uwanja wa  Uhuru, Dar, ubao ulisoma  Simba 0-1 Ruvu Shooting  jambo ambalo  limewafanya  mabingwa hao  watetezi wa  Ligi Kuu Bara  kufikiria namna  ya kulipa kisasi.   Kocha Mkuu  wa Simba,  Didier Gomes,  aliliambia Spoti  Xtra kuwa, kila  mchezo kwao  ni muhimu  kushinda ili  kufikia malengo yao  jambo linalowafanya  wawe na hesabu kali kila  wanaposhuka dimbani.   “Tuna mechi nyingi  za kucheza kwa sasa,  hivyo kila mchezo  tunaufikiria na tunajua  kwamba tukimaliza  mchezo mmoja unafuata  mwingine ambao  unakuwa mgumu zaidi,  hivyo yote tunakwenda  nayo sawa.   “Kikubwa ambacho  tunahitaji ni ushindi  kwani tayari  tumefanikisha lengo la  kwanza la kutinga hatua  ya nusu fainali ya K

MASAU BWIRE ATUMA UJUMBE HUU SIMBA, ATAMBA KUSEPA NA POINTI TATU

Image
  O FISA  Habari  wa Ruvu Shooting,  Masau Bwire,  amesema kuwa  watawakung’uta  tena wapinzani wao, Simba  watakapokutana katika  mchezo wao wa Ligi Kuu Bara  mzunguko wa pili.   Katika mchezo wa kwanza  walipokutana  Uwanja wa Uhuru,  Ruvu Shooting  ilishinda bao 1-0  ilikuwa ni zama za  Sven Vandenbroeck  ambaye alibwaga  manyanga na sasa  yupo Kocha Mkuu,  Didier Gomes.   Amesema  kuwa  wanajua  kwamba  wapinzani  wao  wanafikiria  kulipa kisasi  ila wasahau suala  hilo kwa kuwa halitatokea.   “Tunajua kwamba  Simba wanafikiria  kulipa kisasi, hilo  wasahau kwani  sisi tupo tayari  kuwapapasa,  kuwatingisha na  kuwakung’uta  kwa mara  nyingine tena na  kujidhihirisha sisi ni  zaidi. "Hakuna namna wachezaji wetu wapo imara na tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu” amesema Bwire. Mchezo huo unatarajiwa  kuchezwa Juni 3, Uwanja wa  CCM Kirumba, Mwanza. Kwenye msimamo, Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 ina pointi 37 na inakutana na

KUMBE DE GEA ALIPUUZIA MBINU, KAFUNGWA PENALTI 40

Image
KUMBE kipa namba moja wa Manchester United, David De Gea alipuuzia ushauri wa kocha wake wa makipa wa Manchester United kuhusu upigwaji wa penalti ambao mwisho wake umewafanya wafungwe na Villarreal katika fainali ya Europa League. Iko namna hii baada ya dakika 120 kukamilika, De Gea alipewa karatasi ya maelekezo ya wapigaji penalti wote wa Villarreal ikionyesha upande wanaopendelea kupiga. Lakini yeye akaipuuzia na mwisho wake hakudaka penalti hata moja kati ya 11 zote zilizama nyavuni jumlajumla. Karatasi hiyo ilipatia baadhi ya mipigo ya wapinzani na iliandaliwa na Richard Hartsis lakini mwisho wa siku haikuwa na faida kwao. Kufungwa kwa penalti hizo kunamfanya De Gea kushindwa kudaka penalti hata moja kati ya 40 ambazo amepigiwa akiwa langoni. Mara ya mwisho kwa kipa huyo kudaka penalti ilikuwa ni miaka mitano iliyopita ambapo alizuia penalti ya Lukaku Romelu zama hizo akiwa Everton kufunga katika nusu fainali ya FA Cup, Aprili 23,2016. Penalti hizo 11 alifungwa Mei 26 na k

GEITA GOLD MABINGWA WA JUMLA LIGI DARAJA LA KWANZA

Image
 KLABU ya Geita Gold ambayo msimu ujao itashiriki Ligi Kuu Bara ikitokea Ligi Daraja la Kwanza leo Mei 30 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa fainali Ligi Daraja la Kwanza katika mchezo uliowakutanisha washindi wa kwanza. Mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Uhuru ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo dakika 90 ubao ulisoma Mbeya Kwanza 0-0 Geita Gold. Iliwabidi Geita Gold chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro, 'Baba Isaya' ambaye amepewa tuzo ya kocha bora wasubiri mpaka dakika 30 zilizoongezwa ili kuweza kupata ushindi. Dakika ya 110, Omary  Ramadhan alipachika bao la ushindi kwa kichwa ndani ya 18 na kuwafanya waweze kuibuka na ushindi huo muhimu.  Timu zote mbili msimu ujao zitashiriki Ligi Kuu Bara baada ya kuongoza katika makundi ya Ligi Daraja la Kwanza.

MUKOKO WA YANGA ANASAKWA NA VIGOGO AFRIKA

AZAM KUANZA MAZOEZI KESHO

YANGA: ISHU YA MWAKALEBELA, TUNATAKA HAKI NA SI UONEVU

AZAM FC YAWAPA TANO WACHEZAJI WAKE KUITWA STARS

Image
UONGOZI wa Azam FC umewapa pongezi nyota wake watano kwa kutajwa kwenye orodha ya wachezaji wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Kikosi cha Stars kilitangazwa na Kocha Mkuu, Kim Poulsen Mei 28. Kinatarajiwa kuingia kambini Juni 5 mwaka huu ikiwa ni maandalizi ya mchezo wa kirafiki dhidi ya Malawi. Wachezaji wa Azam FC ambao wamejumuishwa kwenye kikosi ni pamoja na Mudhathir Yahya, Salum Abubakar, Bryson Raphael, Ayoub Lyanga na Idd Seleman, 'Nado'. Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa wachezaji hao wanapaswa pongezi kwa kujumuishwa kwenye kikosi hicho na wanapaswa kutimiza majukumu kwa ukamilifu.

NYOTA WATATU SIMBA WAWANIA TUZO

Image
 NYOTA watatu wa kikosi cha Simba wameingia katika kinyang'anyiro cha kusaka mchezaji bora wa mwezi Mei. Tuzo hiyo ni maalumu kwa ajili ya mashabiki kuweza kuchagua mchezaji ambaye wanaona anastahili kusepa na tuzo hiyo  kutokana na kile ambacho amekifanya katika mwezi husika. Mchezaji wa kwanza kusepa na tuzo hiyo ambayo inadhaminiwa na Emirate Aluminium Profile alikuwa ni kiungo, Luis Miquissone na kwa mwezi Aprili ni Clatous Chama alisepa na tuzo hiyo. Wachezaji ambao wanawania tuzo hiyo ni pamoja na John Bocco ambaye ni nahodha, Bernard Morrison ambaye ni kiungo na Taddeo Lwanga yeye ni mkata umeme.

SIMBA YAITAJA AZAM FC KUWA NJIA YAO KUFIKA FAINALI

Image
  B IG bosi wa Benchi la Ufundi la Simba,  Didier Gomes raia wa Ufaransa  amebainisha mapema kwamba wapinzani  wao, Azam FC ni njia ya wao kutinga Hatua ya  Fainali ya Kombe la Shirikisho (FA).   Kocha huyo ameongeza kwamba anataka kuiona  timu yake ikifanikiwa kutinga fainali ya michuano  hiyo kwa ajili ya kutimiza malengo ambayo  alijiwekea ambapo hilo haliwezi kutimia bila ya  kuwafunga Azam FC.   Simba watakutana na Azam FC kwenye nusu  fainali ya FA baada ya timu hizo kushinda mechi zao  za robo fainali za michuano hiyo. Gomes raia wa Ufaransa, amebainisha wazi  kwamba anataka kuiona Simba ikitinga fainali ya  michuano hiyo ambapo haiwezi kufanya hivyo bila  ya kuwaondosha Azam FC katika nusu fainali. “Tumefika nusu fainali, hili ndilo lengo letu  tangu mwanzo.  Niliwaambia wachezaji wangu  kwamba tunataka kufika fainali moja mwaka huu na  kushinda. “Tuna hatua moja ya kucheza ya nusu fainali,  lakini tuko kwenye mwendo mzuri na najivunia sana  wachezaji wangu wanavyoj

POCHETTINO KURUDI TENA TOTTENHAM

Image
 TOTTENHAM imeanza mazungumzo na kocha wao wa zamani, Mauriccio Pochettino ili awe sehemu ya kumshawishi nyota wao Harry Kane ambaye anahitaji kusepa ndani ya kikosi hicho. Pochettino alifundisha timu hiyo kuanzia mwaka 2014 hadi 2019 na alifukuzwa Novemba mwaka jana baada ya kuwa na msimu mbovu kisha akatua ndani ya PSG. Kwa sasa inaelezwa kuwa hana furaha ndani ya PSG na taarifa zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy anataka kuanza mchakato wa kumrejesha tena. Kocha huyo mwenye miaka 49 ameiongoza PSG kutwaa taji la French Super Cup na French Cup ila amekosa ubingwa wa Ligue 1 na timu yake ilitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na Manchester City katika nusu fainali.

YANGA WARAHISISHIWA KUMPATA MSHAMBULIAJI HUYU WA KAIZER CHIEFS

Image
 BAADA ya  Klabu ya Kaizer Chiefs  ya Afrika Kusini  kutangaza kuachana  na straika Mzambia,  Lazarous Kambole itakuwa ni njia rahisi kwa mabosi wa Jangwani, Yanga kuipata saini yake.   Katika msimu  uliopita, Yanga  ilikuwepo katika  mipango ya kumsajili  Mzambia huyo kabla  Chiefs kuingilia kati  na kumnasa kwa dau la dola  200,000 (zaidi ya Sh 459m)  akitokea Zesco United.   Yanga hivi sasa ipo  kwenye mipango ya kukisuka  kikosi chake ikiwemo safu  ya ushambuliaji ambayo  imeshindwa kuonyesha makali  inayoongozwa na Mghana  Michael Sarpong na Fiston  Abdoulrazack.   Kwa mujibu wa taarifa  ambazo imezipata Championi , kutoka Chiefs  upo uwezekano mkubwa wa  mshambuliaji huyo kuachwa  katika mipango ya klabu hiyo  baada ya kufanya vibaya katika  ligi.   Chiefs itaachana na nyota  huyo kwa lengo la kuacha nafasi  ya kumsajili mshambuliaji  mwingine mwenye uwezo  mkubwa wa kufunga mabao  zaidi ya Kambole ambaye hana  nafasi ya kudumu ya kucheza  katika kikosi cha kwanza.  

BAO LA MORRISON LIRURIDWE

Image
  M ASHABIKI wa  Simba jana  baada ya Bernard  Morrison kufunga  bao kali dhidi ya Namungo,  walilipuka kwa sauti kubwa  wakisema: “Bao la Morrison  lirudiwe, hatujaliona  vizuri.   ” Morrison alifunga bao  hilo dakika ya 87 kwa  shuti la umbali wa zaidi  ya mita 40 akimtesa kipa  wa Namungo, Jonathan  Nahimana katika ushindi  walioupata wa mabao 3-1,  mchezo uliochezwa Uwanja  wa Majaliwa, Lindi.   Simba ilitumia nguvu  nyingi kusaka pointi tatu  jana baada ya Namungo  kutangulia dakika ya 21  kupitia kwa Nzigamasabo  Styve.   Kuingia kwa bao  hilo, kukawapa zaidi  presha Simba waliokuwa  wakipambana kuhakikisha  wanazidi kujitanua kileleni  mwa msimamo wa Ligi Kuu  Bara.   Timu hizo zilienda  mapumziko, wenyeji  Namungo wakiwa mbele  kwa bao 1-0, ndipo Kocha  wa Simba, Didier Gomes,  akafanya mabadiliko.   Mambo yalibadilika  kipindi cha pili baada  ya Gomes kumtoa Rally  Bwalya, nafasi yake  ikachukuliwa na Hassan  Dilunga na Meddie Kagere  alimpisha John Bocco.   Chr

BALAMA MAPINDUZI AREJEA KAZINI SASA

Image
  B AADA ya kuwa  nje ya uwanja  kwa muda  mrefu akiuguza  majeraha ya mguu,  Kiungo Mshambuliaji  wa Yanga, Balama  Mapinduzi, kesho  Jumatatu anatarajiwa  kuanza mazoezi  maalum ya uwanjani.   Balama alivunjika  mguu akiwa mazoezini  katika maandalizi ya  mechi za Ligi Kuu Bara  msimu uliopita ambapo  hadi sasa hajaonekana  uwanjani.   Akizungumza na  Spoti Xtra,  Ofisa Habari  wa Yanga, Hassan  Bumbuli, alisema: “Kwa  mujibu wa daktari,  tayari Balama amepona  na anatarajiwa kuanza  mazoezi Jumatatu timu  ikirejea kambini.   “Alikuwa nje kwa  muda mrefu, hivyo  atakaporejea daktari  na benchi la ufundi  watakaa na kuona  watampa mazoezi yake  binafsi. “   Kwa upande wa  wachezaji wengine  ambao walikuwa  majeruhi, dokta atatoa  ripoti watakaporejea  kambini Jumatatu.” Mbali na Balama,  nyota wengine wa Yanga  ambao ni majeruhi ni  Saidi Ntibazonkiza,  Carlos Carlinhos na  Abdallah Shaibu ‘Ninja’

KOCHA NABI WA YANGA ATOA MAAGIZO MAALUMU

Image
 NASREDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amewaambia wachezaji wake kuwa wanahitaji kutwaa mataji mawili kwa msimu huu wa 2020/21 ili kufikia malengo ambayo walianza nayo mwanzo wa msimu. Mataji hayo ni pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo tayari Yanga imetinga hatua ya nusu fainali baada ya ubao wa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kusoma Mwadui 0-2 Yanga hivyo inatarajiwa kucheza na Biashara United hatua ya nusu fainali. Kwenye upande wa ligi ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 29 na ina mechi  tano mkononi kukamilisha mzungukuko wa pili. Kwa mujibu wa Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema kuwa kocha huyo raia wa Tunisia aliongea na wachezaji na kuwaambia kwamba bado wana kazi ya kufanya kutimiza malengo. “Nabi ameongea na wachezaji na kuwaambia kwamba bado kazi inaendelea na anahitaji kuona wanafanikisha lengo la kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho pamoja na ligi kwani bado mapambano yanaendelea na kazi itaendelea mpaka mwisho,” alisema

KUSHUKA DARAJA NI SUALA LISILOEPUKIKA MUHIMU KUJIPANGA

Image
 NGUVU kubwa kwa sasa kwa timu zinazoshiriki Ligi Kuu Bara ni kuona namna gani zinaweza kupata kile ambacho wanastahili mara baada ya msimu wa 2020/21 kukamilika. Mbali na Mwadui FC ambayo hesabu zimeigomea kubaki ndani ya ligi licha ya mechi zake nne mkononi bado kuna timu nyingine ambazo zitashuka pia. Ligi Daraja la Kwanza zitapanda mbili jumla huku nne zikishuka ambazo ni timu kutoka Ligi Kuu Bara na msimu ujao zitashiriki ligi hiyo ambayo nayo ushindani wake sio wa kawaida. Shirikisho la Soka Tanzania,(TFF) liliweka wazi tangu awali mpango wa kupunguza timu kutoka 18 mpaka 16 ambapo zile zitakazokuwa nafasi ya 13 na 14 zitacheza playoff. Kwa zile ambazo zitashuka zina jukumu la kujipanga upya na kufanya kazi kwa umakini katika kutimiza majukumu yao kwa sababu huku juu ushindani ni mkubwa muda wote. Nimekuwa nikiwasiliana na marafiki zangu wengi kutoka nje ya nchi ambao wanatupa pongezi nyingi kwa kuwa na maendeleo kwenye suala la mpira kwa kuwa wanaona kupitia Azam TV.