KOCHA NABI WA YANGA ATOA MAAGIZO MAALUMU


 NASREDINE Nabi, Kocha Mkuu wa Yanga amewaambia wachezaji wake kuwa wanahitaji kutwaa mataji mawili kwa msimu huu wa 2020/21 ili kufikia malengo ambayo walianza nayo mwanzo wa msimu.


Mataji hayo ni pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo tayari Yanga imetinga hatua ya nusu fainali baada ya ubao wa Uwanja wa Kambarage, Shinyanga kusoma Mwadui 0-2 Yanga hivyo inatarajiwa kucheza na Biashara United hatua ya nusu fainali.


Kwenye upande wa ligi ipo nafasi ya pili ikiwa na pointi 61 baada ya kucheza mechi 29 na ina mechi  tano mkononi kukamilisha mzungukuko wa pili.


Kwa mujibu wa Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz alisema kuwa kocha huyo raia wa Tunisia aliongea na wachezaji na kuwaambia kwamba bado wana kazi ya kufanya kutimiza malengo.


“Nabi ameongea na wachezaji na kuwaambia kwamba bado kazi inaendelea na anahitaji kuona wanafanikisha lengo la kufanya vizuri kwenye Kombe la Shirikisho pamoja na ligi kwani bado mapambano yanaendelea na kazi itaendelea mpaka mwisho,” alisema Nugaz.


Makombe yote mawili ambayo wanapigia hesabu Yanga yapo mikononi mwa watani zao wa jadi Simba ambao nao walibainisha kwamba wanahitaji mataji yao.




Comments

Popular posts from this blog

SIMBA KUBADILI KIKOSI MBELE YA TP MAZEMBE AMBAO WATABADILI MFUMO KESHO

SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUINYOOSHA AIGLE NOIR KWA MKAPA ULICHEZWA HIVI