SIMBA AKILI ZAKE KWA WAZEE WA MPAPASO


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anahitaji kuona wanashinda mbele ya Ruvu Shooting, kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara.

Kwa sasa Ruvu Shooting wao sera yao kubwa ni Mpapaso Square muasisi wake akiwa no Ofisa Habari wao Masau Bwire.

 

Ikumbukwe kwamba, mchezo wa kwanza walipocheza Uwanja wa Uhuru, Dar, ubao ulisoma Simba 0-1 Ruvu Shooting jambo ambalo limewafanya mabingwa hao watetezi wa Ligi Kuu Bara kufikiria namna ya kulipa kisasi.

 

Kocha Mkuu wa Simba, Didier Gomes, aliliambia Spoti Xtra kuwa, kila mchezo kwao ni muhimu kushinda ili kufikia malengo yao jambo linalowafanya wawe na hesabu kali kila wanaposhuka dimbani.

 

“Tuna mechi nyingi za kucheza kwa sasa, hivyo kila mchezo tunaufikiria na tunajua kwamba tukimaliza mchezo mmoja unafuata mwingine ambao unakuwa mgumu zaidi, hivyo yote tunakwenda nayo sawa.

 

“Kikubwa ambacho tunahitaji ni ushindi kwani tayari tumefanikisha lengo la kwanza la kutinga hatua ya nusu fainali ya Kombe la Shirikisho la Azam, kinachofuata ni mechi zetu ambazo zipo ndani ya ligi, mashabiki watupe sapoti,” alisema Gomes.

 

Juni 3, mwaka huu, Ruvu Shooting itakuwa mwenyeji wa Simba kwenye Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza ukiwa ni mchezo wa Ligi Kuu Bara.


Simba inaongoza ligi ikiwa na pointi 64 baada ya kucheza jumla ya 26 inakutana na Ruvu Shooting yenye pointi 37 baada ya kucheza jumla ya mechi 29. 



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA