MASAU BWIRE ATUMA UJUMBE HUU SIMBA, ATAMBA KUSEPA NA POINTI TATU


 OFISA Habari wa Ruvu Shooting, Masau Bwire, amesema kuwa watawakung’uta tena wapinzani wao, Simba watakapokutana katika mchezo wao wa Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili.

 

Katika mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Uhuru, Ruvu Shooting ilishinda bao 1-0 ilikuwa ni zama za Sven Vandenbroeck ambaye alibwaga manyanga na sasa yupo Kocha Mkuu, Didier Gomes.

 

Amesema kuwa wanajua kwamba wapinzani wao wanafikiria kulipa kisasi ila wasahau suala hilo kwa kuwa halitatokea.

 

“Tunajua kwamba Simba wanafikiria kulipa kisasi, hilo wasahau kwani sisi tupo tayari kuwapapasa, kuwatingisha na kuwakung’uta kwa mara nyingine tena na kujidhihirisha sisi ni zaidi.


"Hakuna namna wachezaji wetu wapo imara na tupo tayari kwa ajili ya mchezo huo ambacho tunahitaji ni pointi tatu muhimu” amesema Bwire.


Mchezo huo unatarajiwa kuchezwa Juni 3, Uwanja wa CCM Kirumba, Mwanza.


Kwenye msimamo, Ruvu Shooting ipo nafasi ya 10 ina pointi 37 na inakutana na Simba iliyo nafasi ya kwanza na pointi 64.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO