POCHETTINO KURUDI TENA TOTTENHAM


 TOTTENHAM imeanza mazungumzo na kocha wao wa zamani, Mauriccio Pochettino ili awe sehemu ya kumshawishi nyota wao Harry Kane ambaye anahitaji kusepa ndani ya kikosi hicho.

Pochettino alifundisha timu hiyo kuanzia mwaka 2014 hadi 2019 na alifukuzwa Novemba mwaka jana baada ya kuwa na msimu mbovu kisha akatua ndani ya PSG.

Kwa sasa inaelezwa kuwa hana furaha ndani ya PSG na taarifa zinaeleza kuwa Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy anataka kuanza mchakato wa kumrejesha tena.

Kocha huyo mwenye miaka 49 ameiongoza PSG kutwaa taji la French Super Cup na French Cup ila amekosa ubingwa wa Ligue 1 na timu yake ilitolewa kwenye Ligi ya Mabingwa Ulaya na Manchester City katika nusu fainali.



Comments

Popular posts from this blog

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

KOCHA BIASHARA UNITED: WACHEZAJI NIMEWAPA KAZI YA KUPAMBANA NA JEZI YA NJANO

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI