BREAKING: YANGA WATHIBITISHA KUACHANA NA CARINHOS
BREAKING: Yanga wamethibitisha kuvunja mkataba na kiungo wao Carlos Carlinhos raia wa Angola ambaye alikuwa nje ya uwanja kwa muda akitibu majeraha yake ambayo aliyapata kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Tanzania Prisons.
Taarifa rasmi iliyotolewa na Yanga imeeleza kuwa wamefikia makubaliano ya kusitisha mkataba wake kwa pande zote mbili kukaa chini.
Pia Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu, Nassredine Nabi imemshukuru kiungo huyo kwa huduma yake ndani ya Yanga.
Comments
Post a Comment