GEITA GOLD MABINGWA WA JUMLA LIGI DARAJA LA KWANZA


 KLABU ya Geita Gold ambayo msimu ujao itashiriki Ligi Kuu Bara ikitokea Ligi Daraja la Kwanza leo Mei 30 imeibuka na ushindi wa bao 1-0 dhidi ya Mbeya Kwanza kwenye mchezo wa fainali Ligi Daraja la Kwanza katika mchezo uliowakutanisha washindi wa kwanza.

Mchezo wa leo uliochezwa Uwanja wa Uhuru ulikuwa na ushindani mkubwa ambapo dakika 90 ubao ulisoma Mbeya Kwanza 0-0 Geita Gold.

Iliwabidi Geita Gold chini ya Kocha Mkuu, Felix Minziro, 'Baba Isaya' ambaye amepewa tuzo ya kocha bora wasubiri mpaka dakika 30 zilizoongezwa ili kuweza kupata ushindi.

Dakika ya 110, Omary  Ramadhan alipachika bao la ushindi kwa kichwa ndani ya 18 na kuwafanya waweze kuibuka na ushindi huo muhimu. 

Timu zote mbili msimu ujao zitashiriki Ligi Kuu Bara baada ya kuongoza katika makundi ya Ligi Daraja la Kwanza.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO