Posts

Showing posts from February, 2021

DISMAS TEN WA YANGA AMTAJA HAJI MANARA WA SIMBA KUWA MSEMAJI BORA

Image
  OFISA Habari wa zamani wa Klabu ya Yanga, Dismas Ten amesema kuwa kwake yeye ndani ya ardhi ya Tanzania Ofisa Habari bora kwenye vilabu vya soka Tanzania ni Hassan Bumbuli wa Yanga na Idrissa Bandari wa Ndanda FC.   Ten amewahi kuwa Ofisa Habari wa Mbeya City na ndani ya Yanga amepitia nafasi mbalimbali ikiwa ni pamoja na Kaimu Katibu. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram amesema kuwa kuna tofaiyi kubwa kati ya Ofisa Habari na Msemaji hivyo kwake msemaji bora ni Haji Manara ambaye ni Ofisa Habari wa Simba. "Linapokuja suala la kuongeza, kuzungumza hakuna kama Haji Manara yeye ni msemaji kweli.   "Ipo tofauti kati ya Ofisa Habari na msemaji,".

TUCHEL AWAPA TANO WACHEZAJI WAKE,UNITED WALILIA PENALTI

Image
 THOMAS Tuchel, Kocha Mkuu wa Chelsea amesema kuwa pointi moja waliyopata mbele ya Manchester United,  Uwanja wa Stamford Bridge si haba kwa kuwa wachezaji walipambana kusaka ushindi. Mchezo huo uliochezwa usiku wa kuamkia leo ulikuwa na ushindani mkubwa huku Manchester United wakilalamika kwamba walinyimwa penalti ya wazi kwenye mchezo huo uliokamika ubao kusoma 0-0.  Mwamuzi wa kati Stuart Attwell aliikataa ambapo ilionekana nyota wa Chelsea Callum Hudson-Odoi akiugusa mpira huo walipokuwa wakipambana na Mason Greenwod na uliwagusa wote wawili kwenye mikono walipokuwa ndani ya 18. Matokeo hayo yanaifanya Chelsea kufikisha jumla ya pointi 44 ikiwa nafasi ya 5 huku United ikibaki nafasi ya pili na pointi 50. Kinara ni Manchester City mwenye pointi 62.

SIMBA YATUMA UJUMBE HUU KWA JKT TANZANIA

Image
 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa anatambua mchezo wa leo dhidi ya JKT Tanzania utakuwa na ushindani mkubwa ila amewaambia wachezaji wake wanapaswa kupambana ili kupata pointi tatu. Mchezo wa kwanza uliochezwa Uwanja wa Jamhuri, Dodoma, ubao ulisoma JKT Tanzania 0-4 Simba baada ya dakika 90. Huku bao la kwanza la Luis Miquissone akiwa nje ya 18 likiwa ni moja ya bao bora na kushangilia kwa kuwafuata mashabiki kulimponza nyota huyo ambapo alionyeshwa kadi ya njano. Gomes amesema:"Utakuwa mchezo mgumu ila tunahitaji pointi tatu muhimu,".

YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA COASTAL UNION

Image
 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mpango mkubwa kwa sasa ni kupata matokeo chanya kwenye mechi yao mbele ya Coastal Union. Yanga ikiwa ni namba moja kwenye msimamo na pointi zake 49 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union Machi 4, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga. Kaze amesema kuwa wachezaji wake wapo vizuri na anaamini kwamba atapata matokeo chanya kwenye mchezo huo. "Kwa sasa tunatazama namna gani tunaweza kupata matokeo chanya kwenye mechi zijazo ndani ya Uwanja hilo ni la msingi kwetu. "Kila kitu kitakuwa sawa mashabiki waendelee kutupa sapoti kwa kuwa ushindani ni mkubwa nasi pia tunaendelea kushindana,". 

MWAMBUSI ATANGAZA KUREJEA YANGA

GOMES ASUKA MIPANGO YA KUIPINDUA YANGA

MASHINE MPYA YA YANGA KAMILI GADO KUANZA KAZI

KILICHOMWONDOA BOCCO SIMBA HIKI HAPA

Image
IMEBAINIKA kuwa kilichokuwa kikimsumbua nahodha wa klabu ya Simba, John Raphael Bocco si majeraha kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali bali ni magonjwa mengine ya kiafya. Bocco anayekamatia nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora msimu huu akiwa na mabao nane, juzi Ijumaa alirejea kwa mara ya kwanza uwanjani kuichezea Simba kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya African Lyon hii ni baada ya kukosekana tangu Januari 6, mwaka huu. Akizungumzia hali ya nahodha huyo, Meneja wa kikosi cha Simba, Abbas Ally amesema, Bocco  sasa yuko fiti kwa ajili ya kuendelea kukisaidia kikosi chake kupata matokeo uwanjani. “Nahodha wetu Bocco amerejea tayari kikosini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, na kukosekana kwake uwanjani kwa muda wote uliopita hakukuwa na uhusiano wowote na majeraha, bali ni changamoto nyingine za kiafya za kawaida,"

JEMBE LA SIMBA LATUA GHANA

MRUNDI WA YANGA AMPA KAZE MABAO 14

Image
  KIM Poulsen, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars amesema kuwa rekodi za wachezaji alizopewa na makocha wa timu zao pamoja na maoni ya makocha yamempa nafasi ya kuteua kikosi hicho. Miongoni mwa majina ambayo yalimvutia ni pamoja na mshambuliaji wa Yanga Ditram Nchimbi ambaye yupo chini ya Kocha Mkuu, Cedric Kaze akiwa amehusika kwenye pasi mbili za mabao. Yanga imetoa jumla ya wachezaji nane kikosi cha Stars ambapo wamehusika kwenye mabao 14 kati ya 34 baada ya kucheza jumla ya mechi 21. Mbali na huyo kutoka Yanga pia yupo kipa namba moja Metacha Mnata, Bakari Nondo Mwamnyeto yeye ni beki wa kati ametupia bao moja ndani ya ligi  ingizo jipya ndani ya Yanga,  Dickson Job ni beki wa kati ila majeraha yamemfanya awe nje.  Yassin Mustapha yeye ni beki wa pembeni, Feisal Salum ‘Fei Toto’, yeye ni kiungo mkabaji ametupia bao moja. Farid Mussa yeye ni kiungo mshambuliaji ametoa jumla ya pasi tatu za mabao.  Deus kaseke yeye ni kiungo ndani ya kikosi cha Yanga am

BARBARA: UWEKEZAJI WA KWELI UNALETA MAFANIKIO KWENYE SOKA

Image
  MTENDAJI Mkuu wa Simba, mwanadada Barbara Gonzalez amefunguka kuwa jambo pekee ambalo linaweza kuleta mafanikio kwenye soka ni uwekezaji wa kweli.   Barbara alieleza kuwa mpira wa sasa unahitaji uwekeze fedha ya kutosha kwenye nyanja mbalimbali ikiwemo kwenye kununua wachezaji na kufanya maandalizi ya kina kwenye kila mchezo na mashindano makubwa kwa madogo.   Akizungumza kwa namna ambavyo Simba wanatisha msimu huu hasa kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, Barbara alifunguka: - “Ukiwekeza kwenye soka unafanikiwa kirahisi kabisa bila hata wasiwasi. Hakuna ujanjaujanja kwenye soka. “Ili uweze kufanya vizuri kwenye mashindano ya kimataifa lazima uwe na kikosi chenye wachezaji bora na kocha mwenye viwango vikubwa, ndicho ambacho sisi tunafanya, tumewekeza fedha kwa wachezaji na tunapata mafanikio.” Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika, ikiwa ipo hatua ya makundi, Simba inaongoza ligi ikiwa nafasi ya kwanza na pointi 6. Imecheza mechi mbili na kufunga jumla ya mabao mawili ilikuwa mbele

WAZIR JUNIOR AJIPA MATUMAINI YA KUFANYA VIZURI YANGA

Image
 WAZIR Junior mshambuliaji wa Yanga amesema kuwa anachopitia kwa sasa ni suala la muda ana amini kwamba atapata nafasi ya kucheza. Kwenye usajili wa dirisha dogo, timu zaidi ya tano ikiwa ni pamoja na KMC, Coastal Union, Gwambina na Namungo zilikuwa zinahitaji huduma yake kwa mkopo ia dili lake libuma baada ya Kocha Mkuu,Cedric Kaze kuhitaji huduma yake. Junior ambaye ni ingizo jipya kutoka Klabu ya Mbao FC bado hajawa na nafasi kikosi cha kwanza zaidi ya kujenga ushkaji na benchi. Nyota huyo amesema:"Ilikuwa niondoke wakati ule wa dirisha dogo ila mwalimu alitaka nibaki hivyo nina amini kwamba bado nina nafasi ya kufanya vizuri. "Kikubwa ni kuendelea kupambana ili kuwa bora kwa kuwa ushindani ni mkubwa na kila kitu nina amini kwamba kila kitu kitakuwa sawa,". Ndani ya Yanga ametupia bao moja ilikuwa mbele ya KMC wakati Yanga ikishinda 2-1.

BEKI SIMBA ABADILISHIWA MAJUKUMU

Image
  DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba alimbadilishia majukumu beki wake wa kati, Kenedy Juma kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Mkapa kwa kumpa mikoba ya Shomari Kapombe. Keneddy ambaye aliibuka ndani ya Simba akitokea Singida United ni miongoni mwa mabeki ambao jina lake lipo kwenye orodha ya nyota walioitwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars. Juzi wakati African Lyon 0-3 Simba, alipewa mikoba ya kumwaga maji ambapo alionekana akiimudu kazi hiyo huku akitumia nguvu kubwa kuwazuia nyota wa African Sports kupita upande wake. Gomes amesema kuwa lengo la kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake ni kuweza kuwapa nafasi wale ambao hawachezi mara kwa mara pamoja na kuwapa mapumziko wachezaji wengine.

YANGA YAMPIGIA HESABU NDEFU MTAMBO WA MABAO MZAWA

Image
MESHACK Abraham, mshambuliaji wa kikosi cha Gwambina FC anatajwa kuwekwa kwenye rada za mabosi wa Yanga ili kuweza kuona uwezo wake kwenye mechi za ushindani. Nyota huyo ambaye jina lake limetajwa na Kocha Mkuu, wa timu ya Taifa ya Tanzania, Kim Poulsen kwenye orodha ya  wachezaji watakaongia kambini Machi 8 kujiandaa na mechi za kufuzu Afcon alikuwa kwenye hesabu za kutua kikosini hapo ila dili lake likabuma. Kwa sasa Yanga inapambana kurejea kwenye ubora huku ikiwa imekosa washambuliaji wenye uwezo wa kuwa na mwendelezo mzuri ndani ya uwanja, ambapo kwenye mechi 21 imefunga jumla ya mabao 34 na kinara ni winga Deus Kaseke mwenye mabao 6. Michael Sarpong na Yacouba Songne ambao ni washambuliaji hawa wametupia mabao manne kila mmoja huku nyota Ditram Nchimbi akiwa ametengeneza pasi mbili za mabao. Habari kutoka ndani ya Gwambina zimeeleza kuwa Yanga wanampigia hesabu nyota huyo. "Yanga inahitaji huduma ya Abrahm ila kwa sasa itakuwa ngumu kwa kuwa dirisha la usajili l

JURGEN KLOPP ATAJWA KUIBUKIA TIMU YA TAIFA YA UJERUMANI

Image
IMEELEZWA kuwa Klabu ya Liverpool ipo kwenye mpango wa kuachana na kocha wao Jurgen Klopp katika nafasi hiyo kutokana na kuamini kwamba anaweza kupata dili la kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani. Jina la Steven Gerrad linatajwa kuwa kwenye orodha ya makocha ambao wanapewa nafasi ya kuchukua mikoba ya Klopp ambaye anapambana kutetea taji la Ligi Kuu England ambalo alitwaa msimu uliopita. Pia kuna mashaka kuwa huenda Klopp akapewa kibarua cha kuinoa timu ya taifa ya Ujerumani ambayo ipo mikononi mwa Joachim Low. Habari zinaelezwa kuwa Klopp anatazamwa kwa ukaribu na chama cha soka cha Ujerumani, (DFP) na wana mpango wa kufanya naye mazungumzo hivi karibuni ili aweze kuibuka ndani ya timu ya taifa. Low amefanya kazi na timu ya taifa ya Ujerumani kwa muda wa miaka 15 na 2014 aliweza kukiongoza kikosi hicho kutwaa Kombe la Dunia ila hakuweza kutetea taji hilo 2018 hivyo anahitaji kujiweka kando akihofia kufutwa kazi jumlajumla.

LEO NI VITA YA KIBABE LIGI KUU ENGLAND, CHELSEA V MANCHESTER UNITED

Image
 UWANJA wa Stamford Bridge leo Februari 28 majira ya saa 1:30 utachezwa mchezo mkali wa Ligi Kuu England ambao unatarajiwa kuwa mkali mwanzo mwisho. Ni Thomas Tuchel Kocha Mkuu wa Chelsea ambaye atamkaribisha ndugu yake Ole Gunnar Solskjaer wa Manchester United. Tambo kwa makocha wote wawili zimetawala ambapo kila mmoja ameweka wazi kwamba anahitaji pointi tatu muhimu. Kocha wa Chelsea amesema:"Kwenye kila mchezo kwetu tunahitaji ushindi na tuna amini kwamba na washindani wetu wanahitaji ushindi hivyo tutapambana muda wote,". Kocha wa Manchester United Ole amesema:"Ni ngumu kusema kwamba hatuhitaji ushindi ndani ya uwanja, tutapambana ili kupata matokeo mazuri,". Tuchel atakosa huduma ya beki mkongwe, Thiago Silva huku United wao nyota wao Paul Pogba, Edinson Cavani hawa ni majeruhi.  Kwenye msimamo Chelsea ipo nafasi ya tano na pointi zake ni 43 inakutana na United iliyo nafasi ya pili na pointi zake 49.

IBRAHIM AJIBU AAMBIWA AONGEZE JUHUDI NDANI YA UWANJA

Image
  DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kiungo wake mshambuliaji Ibrahim Ajibu ana kazi ya kuongeza juhudi akiwa mazoezini pamoja na uwanjani ili kuwa bora. Ndani ya Simba ambayo imecheza jumla ya mechi 8 chini ya Gomes baada ya kurithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye kwa sasa yupo Morocco, kocha huyo ameongoza kwenye mechi nane. Katika mechi hizo ni mechi moja Ajibu alianza kikosi cha kwanza ilikuwa ni mbele ya African Lyon ambapo Simba ilishinda mabao 3-0, Uwanja wa Mkapa. Mabao mawili yalifungwa na Ajibu na bao moja lilifungwa na Perfect Chikwende kwa pasi ya Miraji Athuman. Kuhusu Ajibu, Gomes amesema:"Ni moja kati ya wachezaji wazuri ila anapaswa kuongeza juhudi zaidi ili awe bora kila wakati na kupata namba kikosi cha kwanza. "Huwa ninamuona mazoezini anafanya kazi nzuri na ninaamini kwamba akizidi kukazana zaidi atakuwa bora na atafikia malengo ambayo anayo na ya timu kiujumla," . 

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUTINGA 16 BORA ULIKUWA NAMNA HII

Image
  FISTON Abdol Razack nyota mpya wa Yanga jana alifunga bao lake la kwanza ndani ya timu hiyo ambalo liliipa nafasi ya kusonga mbele hatua ya 16 bora kwenye mashindano ya Kombe la Shirikisho. Bao hilo alipachika kwa penalti dakika ya 40 baada ya mpira kumfuata kwenye mkono nyota wa Ken Gold wakati Yanga walipokuwa wakifanya mashambulizi. Jitihada za Yanga kuongeza bao la pili ndani ya dakika tano zilikwama baada ya Adam John, kipa wa Ken Gold kuwa kisiki kwa nyota wengi wa Yanga ambao walikuwa wakifanya majaribio kusaka ushindi. Ni Fei Toto dakika 16 alipaisha mpira akiwa nje kidogo ya lango huku Fiston naye akionekana kukosa utulivu ndani ya eneo la 18. Kipindi cha pili Ken Gold waliongeza juhudi kuweza kutafuta ushindi ila walikwama kumfunga Faroukh Shikalo ambaye aliweza kuokoa hatari. Nyota Carlos Carlinhos alitumia dakika 14 ndani ya Uwanja wa Uhuru ambapo alifanya jaribio moja na kupiga kona mbili kabla ya kuonyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja kutokana na kitendo chake

SIMBA KUIFUNGULIA YANGA KESI SITA MAHAKAMANI,HAWA HAPA WATAJWA

Image
 OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuna kesi zaidi ya sita ambazo zitapelekwa mahakamani zikiwahusu watani zao wa jadi Yanga. Hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliweka hadharani kwamba wana mpango wa kumshitaki Manara ikiwa hataomba msamaha kwa kile alichoeleza kuwa aliharibu nembo ya timu hiyo kwa kuandika ujumbe usio na mantiki kwenye ukurasa wake wa Instagram. Mkutano huo ulifanyika Februari 19,2021 mbele ya Waandishi wa Habari. Ujumbe huo ulihusu jezi ya Yanga jambo ambalo Mwakalebela aliweka wazi kwamba lilishusha mauzo ya jezi. Kutokana na jambo hilo walitoa siku 14 ili aombe radhi na akishindwa kufanya hivyo watachukua hatua. Manara amesema:"Siwezi kuomba msamaha kwa hilo hata nikipewa siku milioni, siwezi kwa jambo gani hasa, tena kesi kama hizo ninazipenda sana waache tu tuone itakuaje. "Sasa nami ninasema kwamba hata wao tuna kesi nao, kuna kesi zaidi ya 6 zinawahusu tunaongea na mwanasheria wetu aweke mambo sa

MTIBWA SUGAR WATAJA SABABU ZA KUWA NA MWENDO WA KINYONGA

Image
KOCHA Mkuu wa Mtibwa Sugar, Hitimana Thiery amesema kuwa kinachowasumbua wachezaji wake kwa sasa kushindwa kupata matokeo chanya ndani ya uwanja ni kutokuwa fiti kwa ajili ya kupambana. Mtibwa Sugar kwenye Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora imefungashiwa virago na JKT Tanzania ikiwa Uwanja wao wa nyumbani, Jamhuri,Morogoro. Dakika 90 zilikamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2 kisha ngoma ilipofika hatua ya mikwaju ya penalti, Mtibwa Sugar 4-5 JKT Tanzania. Kwenye Ligi Kuu Bara pia mwendo wake ni wa kinyonga, ikiwa imecheza jumla ya mechi19 ipo nafasi ya 12 na pointi zake ni 23. Hitimana amesema:"Bado wachezaji hawajawa fiti katika mapambano ndani ya uwanja jambo ambalo linafanya tunapoteza mechi zetu. "Ila haina maana kwamba hili tatizo litadumu hapana muda wake umekwisha ndio maana tunapambana ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja. "Kila kitu kinawezekana na ni muda wetu wa kurejea kwenye ubora wetu hivyo mashabiki waendelee kutupa sapoti kila kitu kitak

KADI NYEKUNDU YAMUIBUA MUANGOLA WA YANGA, BEKI AFUNGUKA NGUMI ALIYOPIGWA

Image
KIUNGO wa Yanga, Carlos Carlinhos amesema kuwa anasikitika kwa kuonyeshwa kadi nyekundu kwenye mchezo wao wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora uliochezwa Uwanja wa Uhuru. Jana, Februari 27 wakati Yanga ikishinda bao 1-0 dhidi ya Ken Gold FC ya Mbeya, Carlinhos alionyeshwa kadi nyekundu dakika ya 80. Aliingia uwanjani dakika ya 66 na alikutana na adhabu hiyo baada ya kumpiga ngumi ya chemba beki wa Ken Gold, Boniface Mwanjonde. Nyota huyo raia wa Angola amesema kuwa anasikitika kwa alichokifanya kwa kuwa hakutarajia jambo ambalo linampa presha. "Ninasikitika kwa kadi nyekundu ambayo nimepata hivyo sina la kusema zaidi ya kuomba msamaha kwa kile ambacho kimetokea,". Kwa upande wake beki Mwanjonde amesema kuwa alikutana na ngumi hiyo ya mbavu baada ya kumziba njia raia huyo wa Angola. "Ilikuwa ni ngumi ya mbavu baada ya kumzidi spidi yeye alikuja mwilini hapo niliweza kumziba njia na mpira ulitoka nje. "Wakati tunarudi uwanjani akaja akanipiga ngumi ya mbav

DUBE AIPELEKA AZAM FC MIKONONI MWA POLISI

Image
  PRINCE Dube, mshambuliaji namba moja ndani ya kikosi cha Azam FC amefanikiwa kutimiza majukumu yake kwa uzuri na kuipeleka timu hiyo hatua ya 16 bora Kombe la Shirikisho.  Bao lake la ushindi dakika ya 45+1, Uwanja wa Azam Complex limetosha kuwafungashia virago Mbuni FC ambao walikamilisha dakika 90 bila kuweka mzani sawa. Ushindi huo wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina unaifanya Azam FC kuungana na Kagera Sugar, Simba, Yanga ambazo zimetinga hatua ya 16 bora. Mchezo wake wa raundi ya tano watakutana na Polisi Tanzania inayonolewa na Kocha Mkuu, Hamsini Malale  Uwanja wa Azam Complex. Azam FC imeweka wazi kwamba malengo makubwa ni kupata ushindi kwenye mechi zao zilizobaki na kuweza kutwaa mataji ambayo wanayapambania. Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema:"Malengo ni kuona kwamba tunapata matokeo chanya kwenye mechi zetu ambazo tutacheza na kuweza kutwaa mataji,".

MCHEZO WA KIMATAIFA DHIDI YA AL MERRIKH WAMFIKIRISHA GOMES

Image
 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba amesema kuwa mchezo wake ujao dhidi ya Al Merrikh utakuwa mgumu tofauti na wengi wanavyofikiria. Kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika Simba ikiwa ipo kundi A ipo nafasi ya kwanza na ina pointi sita, mechi zake zote mbili imeshinda. Ilianza kushinda ugenini mbele ya AS Vita 0-1 Simba kisha ikashinda bao 1-0 dhidi ya Al Ahly, Uwanja wa Mkapa. Mchezo wake unaofuata wa Ligi ya Mabingwa Afrika itakuwa Machi 5, ugenini nchini Sudani, timu hiyo ilikuwa mikononi mwa Gomes kabla ya kuibukia ndani ya Simba Januari 24 kuchukua mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye yupo zake Morocco. Gomes amesema:"Kuhusu hilo tuna muda mwingi wa kufikiria juu ya mechi ijayo, itakuwa mechi ngumu kwa sababu naijua hiyo timu. Lakini kwa sasa nadhani tunatakiwa kutojipa mawazo sana kuhusiana na mechi hiyo inayokuja. "Wachezaji wanajua kwamba tunahitaji ushindi ila inahitaji muda na tutapambana ili kupata matokeo chanya ndani ya uwanja, kikubwa sapoti pamoja na umaki

YANGA KUPELEKWA FIFA NA SIBOMANA,KISA MKWANJA

Image
PATRICK Sibomana ameibuka na kudai yupo kwenye mpango wa kuifungulia mashitaka Klabu ya Yanga kwenye Shirikisho la Soka la Kimataifa (Fifa), kwa kile alichokieleza kuwa, ukiukwaji wa makubaliano ya malipo ya stahiki zake.   Hii inakuja ikiwa ni siku chache baada ya Fifa kuitaka Yanga kumlipa aliyekuwa mshambuliaji wa timu hiyo, Amissi Tambwe.   Sibomana ambaye ni mshambuliaji aliichezea Yanga kwa msimu uliopita kabla ya kuachwa mwishoni mwa msimu huo. Nyota huyo anayeumia zaidi mguu wa kushoto amesema: “Tulikubaliana kwamba Yanga wanilipe fedha zangu za usajili ambazo zilibaki kiasi cha dola 10,000 (Sh mil 23).   “Kwa kuwa niliishi nao vizuri na nilijua timu ilikuwa haina fedha, tulipanga wanilipe kwanza fedha ya miezi mitatu pamoja na fedha ya usajili ambayo jumla yake ni dola 16,000 (Sh mil 36.9) ambayo nilikatwa  hadi kufikia dola 14,500 (Sh mil 33.4). “Tukakubaliana kwamba wangenilipa Oktoba 30, mwaka jana ambapo walinipatia dola 3,000 (Sh mil 6.9) ikabaki dola 11,500

YANGA YATINGA 16 BORA, NGUMI YAMPONZA MUANGOLA ALIMWA KADI NYEKUNDU

Image
 LICHA ya kumaliza dakika 90 wakiwa pungufu, leo Februari 27, Uwanja wa Uhuru kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Ken Gold bado waliweza kulinda ushindi wao wa bao 1-0 walilolipata. Ni Fiston Abdulazack, ingizo jipya ndani ya Yanga ambaye alipachika bao la ushindi dakika ya 40 kwa mkwaju wa penalti uliomshinda kipa wa Ken Gold, Adam John. Bao hilo lilidumu hadi kipindi cha pili licha ya nyota wa Ken Gold kupambana kuweza kuweka usawa kwenye mchezo huo uliokuwa na ushindani mkubwa. Jitihada zao zilikwama kwenye mikono ya kipa Faroukh Shikalo ambaye alianza kikosi cha kwanza. Dakika ya 80 kiungo Carlos Carlinhos, raia wa Angola alionyeshwa kadi nyekundu ya moja kwa moja baada ya kumpiga ngumi mchezaji wa Ken Gold jambo lililopelekea mwamuzi kumuonyesha kadi hiyo. Inakuwa ni kadi ya kwanza kwa nyota huyo wa Yanga mwenye mabao matatu ndani ya Ligi Kuu Bara na aliingia akitoka benchi kuchukua nafasi ya mshambuliaji Ditram Nchimbi. Ushindi huo unaifanya Yanga itin

MAJEMBE HAYA MATATU YAANZA KAZI RASMI NDANI YA SIMBA

Image
 MABINGWA watetezi wa Ligi Kuu Bara na Kombe la Shirikisho ndani ya ardhi ya Tanzania, Simba wamerejesha tabasamu lao upya baada ya majembe yao matatu ya kazi kurejea rasmi kweye kikosi hicho. Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, jana Februari 26 ubao ulisoma African Lyon 0-3 Simba kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho hatua ya 32 bora na kuwafanya waweze kutinga hatua ya 16 bora. Kwenye mchezo huo majembe mawili ambayo yalikuwa nje kwa muda mrefu kutokana na sababu mbalimbali yalianza rasmi kwenye kikosi kazi. John Bocco ambaye alikuwa ni majeruhi na Jonas Mkude ambaye alisimamishwa kutokana na nidhamu. Hawa wote walicheza ambapo Mkude, kiungo mkabaji yeye aliyeyusha dakika zote 90 huku Bocco akitokea benchi kipindi cha pili na kucheza kwa mara kwanza mbele ya Gomes. Leo Februari, Patrik Rweyemamu ambaye alisimamishwa na mabosi wa Simba kwa kile kilichoelezwa kuwa ni hujuma baada ya kufungwa mechi mbili mfululizo amerejeshwa kikosini. Rweyemamu alisimamishwa na Simba na n

FA:YANGA 1-0 KEN GOLD

Image
  FT: Yanga 1-0 Ken Gold  Mpira umekamilika Uwanja wa uhuru kwa Yanga kuibuka na ushindi wa bao 1-0 mbele ya Ken Gold. Ushindi huo unaifanya Yanga isonge mbele hatua ya 16 bora ya Kombe la Shirikisho. Dakika 90 Niyonzima anafanya jaribio jepesi linaokolewa na kipa wa Ken Gold  Dakika ya 88 Fiston anatoka anaingia anaingia Sarpong  Dakika ya 80 Carinhos anaonyeshwa kadi nyekundu Dakika ya 79 Carinhos anampiga ngumi mchezaji wa Ken Gold  Dakika ya 78 Niyonzima anafanya jaribio linaokolewa na kipa wa Ken Gold  Dakika ya 70 Yanga wanapata kona inapigwa na Carinhos  Dakika ya 69 Shikalo anaokoa jaribio la Ken Gold  Dakika ya 67 Carinhos anafanya jaribio linaokolewa na kipa wa Ken Gold  Dakika ya 66 Carinhos anaingia anatoka Nchimbi  Dakika ya 63  Ken Gold wanapoteza nafasi ya wazi ndani ya 18 Dakika ya 61 Fiston anakosa nafasi ndani ya 18 Dakika ya 59 Haruna anaingia anatoka Kaseke Dakika ya 59 Yanga wanapata kona ya 10 Dakika ya 53 Fiston anakosa nafasi ya wazi Dakik

RASMI KIKOSI CHA YANGA KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA KENGOLD

Image
 LEO Februari 27 Yanga itakuwa na kibarua cha kusaka ushindi mbele ya Kengold ya Mbeya ambayo nayo pia inahitaji ushindi kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni. Hiki hapa kikosi rasmi cha Yanga kitakachoanza kusaka tiketi ya kutinga hatua ya 16 bora kwa kuwa leo ni hatua ya 32 bora:- Faroukh Shikalo Paul Godfrey Yassin Mustapha Juma Makapu Bakari Mwamnyeto Farid Mussa Zawadi Mauya Feisal Salum Fiston  Deus Kaseke  Ditram Nchimbi Hawa ni wa akiba Metacha Adeyum Lamine Niyonzima Carlos Sarpong Yacouba Songne

MTAMBO WA MABAO NDANI YA SIMBA WAINGIA ANGA ZA NORWAY

Image
  JUNIOR Lokosa, mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Simba anatajwa kuwa kwenye hesabu za timu moja ya nchini Norway ambayo inahitaji huduma yake. Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, Lokosa bado hajapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwenye mechi 8 ambazo Gomes ameziongoza msimu wa 2020/21. Habari zinaeleza kuwa bado Gomes hajaelewa uwezo wake hivyo itakuwa rahisi kwa raia huyo wa Nigeria mwenye miaka 27 kusepa mazima ndani ya kikosi hicho baada ya kusaini dili la miezi sita. Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji ambao wamesajiliwa na Simba huwa inawachukua muda kuingia kikosi cha kwanza hivyo wale ambao wanambeza Lokosa wataona uwezo wake. "Lokosa ni moja ya wachezaji wazuri na ataingia kwenye mfumo hivi karibuni hivyo kama kuna watu ambao wanambeza basi wasubiri pale atakapojibu ndani ya Simba. "Kuhusu biashara ya wachezaji tunajua kwamba wachezaji wanahitajika na wapo mawakala ambao wanahitaji huduma zao hapo sasa ni suala la dau kua

AZAM FC:MBUNI HATUWAJUI ILA TUTAPAMBANA

Image
 BRUCE Kangwa, nahodha msaidizi wa kikosi cha Azam FC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo wa leo wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Mbuni FC utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex. Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya Mbuni ili iweze kutinga hatua ya 16 bora. Akizungumza na Saleh Jembe Kangwa amesema kuwa wapo tayari na wanaamini watafanya vizuri ndani ya dakika 90 licha ya kutuwajua aina ya uchezaji wao ndani ya uwanja. "Kiujumla wachezaji wapo tayari na kila kitu kuhusu maandalizi kipo sawa hivyo mashabiki watupe sapoti ndani ya uwanja. "Wapinzani wetu kiukweli hatuwajui namna ambavyo wanacheza ila tutacheza nao kama fainali kwa kuwa tunajua kwamba timu ndogo zinatoa timu kubwa hilo tunalijua tutapambana ili tusipate matatizo,". Jana kikosi hicho kilifanya mazoezi ya mwisho ndani ya Uwanja wa Azam Complex huku kipa wao Martin Kingonya akionyesha uwezo na huenda akaanza leo mbele ya Mbuni FC.

KIKOSI CHA YANGA KINACHOTARAJIWA KUANZA LEO DHIDI YA KENGOLD YA MBEYA

Image
LEO Yanga inayonolewa na Kocha Mkuu Cedric Kaze ina kazi ya kusaka ushindi mbele ya kikosi cha Kengold ya Mbeya, Uwanja wa Uhuru. mchezo huo ni wa hatua ya 32 bora ambapo atakayepoteza anafungashiwa virago mazima ndani ya Kombe la Shirikisho linalotetewa na watani zao wa jadi Simba. Hiki hapa kikosi cha Yanga kinachotarajiwa kuwanza leo Uwanja wa Uhuru namna hii:- Faroukh Shikalo Shomari Kibwana Yassin Mustapha Lamine Moro Bakari Mwamnyeto Farid Mussa Tuisila Kisida Feisal Salum Wazir Junior Deus Kaseke  Ditram Nchimbi

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO

Image
RAHEEM Kangezi,'Zamuda' Mwenyekiti wa Klabu ya African Lyon na mmiliki wa timu hiyo amesema kuwa wamefanya mambo mengi kwa ajili ya Simba ikiwa ni pamoja na logo mpya ya timu hiyo pamoja na mpango wa Visit Tanzania. Zamuda amesema kuwa ikiwa wanasema kwamba anapiga porojo hilo sio kweli kwa kuwa anamheshimu kila mtu ikiwa ni pamoja Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara. Jana timu yake ilipoteza kwa kufungwa 0-3 dhidi ya Simba huku akiweka wazi kwamba kuna vitu aliahidiwa kulipwa na bosi wa timu yao ila havijafanyika mpaka sasa.  "Tunafanya vitu vingi sana ndani ya Simba kwa kuwa ile Visit Tanzania imetoka kwetu na muulize Barbra (Gonzalez) akuonyeshe email ambayo nilimtumia pia logo mpya ya Simba imetoka kwetu. "Tuna wachezaji ndani ya ligi zaidi ya 50, Miraji Athuman ametoka kwetu, kuna Mwenyekiti wa Mashindano wa Yanga ametoka kwetu na kocha msaidizi pia ametoka kwetu. "Bajeti yetu sio kubwa lakini ni tofauti kidogo kwa kuwa ninawalipa wachezaji na ninasafi

SARPONG AYEYUSHA DAKIKA 426 BILA KUCHEKA NA NYAVU BONGO

Image
  GUU la Michael Sarpong, mshambuliaji wa Yanga,inayonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze limekwama Uwanja wa Mkapa kwa muda wa dakika 426 bila kucheka na nyavu. Bao la kwanza Sarpong aliwafunga Tanzania Prisons, Uwanja wa Mkapa, bao la pili aliwatungua Biashara United, Uwanja wa Karume. Bao tatu aliwatungua Simba kwa mkwaju wa penalti, Uwanja wa Mkapa. Bao la nne aliwatungua Ruvu Shooting, Uwanja wa Mkapa ilikuwa Desemba 6.  Baada ya hapo amecheza jumla ya mechi sita ndani ya ligi zote hajafunga zaidi ya kutoa pasi moja za mabao. Hivyo mshambuliaji huyo amehusika kwenye mabao matano kati ya 33 yaliyofungwa na timu hiyo akiwa amefunga manne na pasi moja ya bao. Hizi hapa za kwenye ligi:-Mwadui 0-5 Yanga alitumia dakika 90,Yanga 3-1 Dodoma Jiji alitumia dakika 45,Tanzania Prisons 1-1 Yanga alitumia dakika 90,Mbeya City 1-1 Yanga alitumia dakika 90,Yanga 3-3 Kagera Sugar alitumia dakika 45, Yanga 1-0 Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa dakika 66. Sarpong amesema kuwa anaamini mashabik

MCHEZO MZIMA SIMBA WALIVYOWATULIZA AFRICAN LYON KWA MKAPA

Image
  MABINGWA watetezi wa Kombe la Shirikisho ndani ya ardhi ya Bongo, Simba jana wameibuka na ushindi wa mabao 2-0 dhidi ya African Lyon. Kwenye mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Mkapa, Didier Gomes, Kocha Mkuu wa Simba alishuhudia mabao mawili yakipachikwa na kiungo wake mshambuliaji Ibrahim Ajibu. Ajibu ikiwa ni mchezo wake wa kwanza kuanza kikosi cha kwanza kwenye mechi zote 8 ambazo Gomes ameongoza kikosi hicho ambapo ni mbili za Ligi ya Mabingwa Afrika, mechi tatu za ligi,mechi mbili za Simba Super Cup na mechi moja ya Kombe la Shirikisho. Mabao yote alipachika ndani ya 18 kipindi cha kwanza ambapo dakika ya  9 alipachika kwa kichwa baada ya kipa wa African Lyon Bwanaheri Abdallah kutema mpira wa kona uliokutana na kichwa cha Ajibu. Bao la pili ilikuwa dakika ya 43 baada ya kipa tena kutema shuti kali lililopigwa na Rarry Bwalya likakutana na mguu wa kulia wa Ajibu na kuwafanya Simba kushinda kwa mabao hayo. Ni Meddie Kagere atajutia nafasi ya penalti aliyopewa dakika ya 20 kup

CHELSEA, MANCHESTER CITY NA UNITED ZAPIGA HESABU SAINI YA JAHKEELE

Image
KINDA Jahkeele Marshall-Rutty anatajwa kuziingiza vitani klabu kubwa duniani ambazo zinahitaji saini yake ikiwa ni pamoja na Chelsea, Manchester United, Manchester City ambazo zinapata ushindani pia kutoka Bayern Munich na Juventus. Nyota huyo anayekipiga ndani ya Klabu ya Toronto mkononi ana tuzo ya kuwa mchezaji bora ndani ya timu hiyo ambayo aliitwaa Oktoba,2020 yeye ni mshambuliaji na ana miaka 16. Aliletwa duniani Juni 2004 amekuwa akitajwa kuwa ni bora awapo ndani ya uwanja jambo ambalo limezifanya timu nyigi duniani kubwa kumfuatilia kwa ukaribu ili kuwa naye katika timu zao kwa ajili ya wakati ujao. Imeripotiwa kuwa Kocha Mkuu wa Manchester City, Pep Guardiola anahitaji kuwa naye ndani ya kikosi chake kwa kuwa anakubali uwezo wake jambo ambalo litampa changamoto ni ushindani kutoka timu nyingine ambazo zinahitaji saini yake. Kinda huyo raia wa Canada amesema kuwa anachotazama kwa sasa ni kuona anafika hatua ya mafanikio ambayo anayatarajia bila kujali amevunja rekodi ya