SIMBA KUIFUNGULIA YANGA KESI SITA MAHAKAMANI,HAWA HAPA WATAJWA




 OFISA Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa kuna kesi zaidi ya sita ambazo zitapelekwa mahakamani zikiwahusu watani zao wa jadi Yanga.

Hivi karibuni, Makamu Mwenyekiti wa Yanga, Fredrick Mwakalebela aliweka hadharani kwamba wana mpango wa kumshitaki Manara ikiwa hataomba msamaha kwa kile alichoeleza kuwa aliharibu nembo ya timu hiyo kwa kuandika ujumbe usio na mantiki kwenye ukurasa wake wa Instagram.

Mkutano huo ulifanyika Februari 19,2021 mbele ya Waandishi wa Habari.



Ujumbe huo ulihusu jezi ya Yanga jambo ambalo Mwakalebela aliweka wazi kwamba lilishusha mauzo ya jezi. Kutokana na jambo hilo walitoa siku 14 ili aombe radhi na akishindwa kufanya hivyo watachukua hatua.

Manara amesema:"Siwezi kuomba msamaha kwa hilo hata nikipewa siku milioni, siwezi kwa jambo gani hasa, tena kesi kama hizo ninazipenda sana waache tu tuone itakuaje.

"Sasa nami ninasema kwamba hata wao tuna kesi nao, kuna kesi zaidi ya 6 zinawahusu tunaongea na mwanasheria wetu aweke mambo sawa hivi kunzia sasa na mambo yakikamilika kila kitu kitakuwa wazi.

"Zipo kama sita hivi ipo ya huyo Mwakalebela,(Fredrick) huyo Bumbuli,(Hassan Bumbuli) na wengine wengi hivyo wao wameanza nasi tunafuata hatuna mashaka tupo imara," amesema.

Bumbuli ni Ofisa Habari wa Yanga ambapo alifungiwa kujihusisha na soka kwa muda wa miaka mitatu na Shirikisho la Soka Tanzania, (TFF) baada ya kukata rufaa amerejeshwa kazini rasmi.




Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA