BEKI SIMBA ABADILISHIWA MAJUKUMU


 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba alimbadilishia majukumu beki wake wa kati, Kenedy Juma kwenye mchezo wa Kombe la Shirikisho, Uwanja wa Mkapa kwa kumpa mikoba ya Shomari Kapombe.


Keneddy ambaye aliibuka ndani ya Simba akitokea Singida United ni miongoni mwa mabeki ambao jina lake lipo kwenye orodha ya nyota walioitwa timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars.


Juzi wakati African Lyon 0-3 Simba, alipewa mikoba ya kumwaga maji ambapo alionekana akiimudu kazi hiyo huku akitumia nguvu kubwa kuwazuia nyota wa African Sports kupita upande wake.


Gomes amesema kuwa lengo la kufanya mabadiliko kwenye kikosi chake ni kuweza kuwapa nafasi wale ambao hawachezi mara kwa mara pamoja na kuwapa mapumziko wachezaji wengine.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA KUBADILI KIKOSI MBELE YA TP MAZEMBE AMBAO WATABADILI MFUMO KESHO

SIMBA YAJIFUA LEO SUMBAWANGA KUELEKEA MCHEZO WA FAINALI KOMBE LA SHIRIKISHO

MCHEZO MZIMA WA YANGA KUINYOOSHA AIGLE NOIR KWA MKAPA ULICHEZWA HIVI