MTAMBO WA MABAO NDANI YA SIMBA WAINGIA ANGA ZA NORWAY

 


JUNIOR Lokosa, mshambuliaji mpya ndani ya kikosi cha Simba anatajwa kuwa kwenye hesabu za timu moja ya nchini Norway ambayo inahitaji huduma yake.

Ikiwa chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes, Lokosa bado hajapata nafasi ya kuanza kikosi cha kwanza kwenye mechi 8 ambazo Gomes ameziongoza msimu wa 2020/21.

Habari zinaeleza kuwa bado Gomes hajaelewa uwezo wake hivyo itakuwa rahisi kwa raia huyo wa Nigeria mwenye miaka 27 kusepa mazima ndani ya kikosi hicho baada ya kusaini dili la miezi sita.

Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wachezaji ambao wamesajiliwa na Simba huwa inawachukua muda kuingia kikosi cha kwanza hivyo wale ambao wanambeza Lokosa wataona uwezo wake.

"Lokosa ni moja ya wachezaji wazuri na ataingia kwenye mfumo hivi karibuni hivyo kama kuna watu ambao wanambeza basi wasubiri pale atakapojibu ndani ya Simba.

"Kuhusu biashara ya wachezaji tunajua kwamba wachezaji wanahitajika na wapo mawakala ambao wanahitaji huduma zao hapo sasa ni suala la dau kuangalia namna itakavyokuwa," .



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA