KILICHOMWONDOA BOCCO SIMBA HIKI HAPA


IMEBAINIKA kuwa kilichokuwa kikimsumbua nahodha wa klabu ya Simba, John Raphael Bocco si majeraha kama ilivyokuwa ikiripotiwa hapo awali bali ni magonjwa mengine ya kiafya.

Bocco anayekamatia nafasi ya pili kwenye chati ya wafungaji bora msimu huu akiwa na mabao nane, juzi Ijumaa alirejea kwa mara ya kwanza uwanjani kuichezea Simba kwenye mchezo wa kombe la FA dhidi ya African Lyon hii ni baada ya kukosekana tangu Januari 6, mwaka huu.

Akizungumzia hali ya nahodha huyo, Meneja wa kikosi cha Simba, Abbas Ally amesema, Bocco  sasa yuko fiti kwa ajili ya kuendelea kukisaidia kikosi chake kupata matokeo uwanjani.

“Nahodha wetu Bocco amerejea tayari kikosini baada ya kuwa nje ya uwanja kwa muda mrefu, na kukosekana kwake uwanjani kwa muda wote uliopita hakukuwa na uhusiano wowote na majeraha, bali ni changamoto nyingine za kiafya za kawaida,"



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO