YANGA YAZITAKA POINTI TATU ZA COASTAL UNION


 CEDRIC Kaze, Kocha Mkuu wa Yanga amesema kuwa mpango mkubwa kwa sasa ni kupata matokeo chanya kwenye mechi yao mbele ya Coastal Union.

Yanga ikiwa ni namba moja kwenye msimamo na pointi zake 49 ina kibarua cha kusaka pointi tatu mbele ya Coastal Union Machi 4, Uwanja wa Mkwakwani, Tanga.

Kaze amesema kuwa wachezaji wake wapo vizuri na anaamini kwamba atapata matokeo chanya kwenye mchezo huo.

"Kwa sasa tunatazama namna gani tunaweza kupata matokeo chanya kwenye mechi zijazo ndani ya Uwanja hilo ni la msingi kwetu.

"Kila kitu kitakuwa sawa mashabiki waendelee kutupa sapoti kwa kuwa ushindani ni mkubwa nasi pia tunaendelea kushindana,". 



Comments

Popular posts from this blog

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

KOCHA BIASHARA UNITED: WACHEZAJI NIMEWAPA KAZI YA KUPAMBANA NA JEZI YA NJANO

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI