SIMBA YAINGIA ANGA ZA UD SONGO, KULIVUTA JEMBE HILI LA KAZI
IMEFAHAMIKA kuwa, kiungo mshambuliaji wa Simba raia wa Msumbiji, Luis Miquissone, ndiye aliyetoa mapendekezo ya usajili wa kiungo mshambuliaji, Pachoio Lau Há King anayekipiga UD Songo ya nchini huko. Imeelezwa kuwa, Simba imepanga kumsajili kiungo huyo wa kimataifa raia wa Msumbiji katika kukiboresha kikosi chao kinachojiandaa na Ligi ya Mabingwa Afrika msimu wa 2020/21. Wakati Simba ikiwa katika mipango hiyo ya kumsajili nyota huyo, imepanga kuachana na kiungo wao mchezeshaji raia wa nchini Kenya, Francis Kahata ambaye mkataba wake unatarajiwa kumalizika mwishoni mwa msimu huu. Kwa mujibu wa taarifa ambazo imezipata Spoti Xtra, Simba inamtumia Luis kufanikisha usajili wa kiungo huyo wa pembeni atakayetua kuichezea timu hiyo kwenye usajili wa dirisha dogo msimu huu. Mtoa taarifa huyo alisema kuwa, Luis alimpendekeza jamaa huyo baada ya viongozi kumshirikisha kuhusu usajili wa kiungo wa kimataifa mwenye uwezo wa kutengeneza mabao akitokea pem...