BIASHARA UNITED V YANGA, NGOMA NI NZITO, CHEKI REKODI ZAO
IKIWA imepanda Ligi Kuu Bara msimu wa 2018/19 Biashara United leo inakutana na Yanga mara ya tano uwanjani huku rekodi zikiwa ngumu kwa Yanga kupata ushindi Uwanja wa Karume.
Mechi nne ambazo wamecheza, jumla mabao matano yamekusanywa ambapo Yanga imefunga mabao matatu na Biashara United imefunga mabao mawili.
Yanga imeshinda mechi mbili na zote ilikuwa nyumbani, Uwanja wa Mkapa huku Biashara United ikishinda mchezo mmoja, wamelazimisha sare moja ilikuwa Uwanja wa Karume.
Kwa misimu miwili Yanga haijapata ushindi ndani ya Uwanja wa Karume zaidi ya kuambulia sare ya bila kufungana msimu wa 2019/20 hivyo leo itapambana kuvunja rekodi hiyo.
Matoke yao yalikuwa namna hii:-2018/19,Yanga 2-1 Biashara United, Biashara United 1-0 Yanga
.
2019/20
Yanga 1-0 Biashara United.
Biashara United 0-0 Yanga.
Comments
Post a Comment