CRISTIANO RONALDO APONA CORONA, SASA KAZIKAZI


 UONGOZI wa Juventus umethibitisha kuwa nyota wao Cristiano Ronaldo kwa sasa tayari ameshapona COVID -19 baada ya kubaninika na Virusi hivyo ambapo alikaa karantini kwa muda wa siku 19.


Ronaldo akiwa karantini alikosa mechi nne ndani ya kikosi chake ikiwa ni pamoja na ile dhidi ya Barcelona ya mshikaji wake Lionel Messi katika Ligi ya Mabingwa Ulaya wakati wakipoteza kwa kufungwa mabao 2-0.


Staa huyo alibainika kupata maambukizi ya Corona akiwa kwenye majukumu ya timu ya Taifa ya Ureno Oktoba 13 mwezi uliopita.

"Cristiano Ronaldo amefanyiwa vipimo kwa mara nyingine na amebainika kwamba hana Virusi vya Corona, kwa sasa anarejea kwenye timu hivyo hatajitenga tena kama ilivyokuwa awali." ilieleza taarifa hiyo.



Comments

Popular posts from this blog

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

KOCHA BIASHARA UNITED: WACHEZAJI NIMEWAPA KAZI YA KUPAMBANA NA JEZI YA NJANO

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI