SVEN ATAJA SABABU YA KUMPA MAJUKU YA USHAMBULIAJI AJIBU


SVEN Vandenbroeck Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa hakuwa na chaguo la kufanya ndani ya uwanja zaidi ya kumtumia Ibrahim Ajibu kuwa mshambuliaji kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Ruvu Shooting wakati wakipoteza kwa kufungwa bao 1-0.


Oktoba 26, Simba ilipokea kichapo cha pili mfululizo ikiwa ni cha pili mfululizo kwa msimu wa 2020/21 baada ya kuanza kufungwa bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons.


Kwenye mchezo huo Ajibu alipewa jukumu la kusaka ushindi kwa timu yake akilishwa mipira na Luis Miqussone ambaye ana jumla ya pasi tano na bao moja ndani ya ligi.


Sven amesema:"Sikuwa na jambo la kufanya kwa kuwa washambuliaji wangu wengi walikuwa ni ni majeruhi hivyo sikuwa na chaguo zaidi ya kumtumia Ajibu kwenye mchezo wetu dhidi ya Ruvu Shooting."


Ajibu kwenye mchezo huo alipiga jumla ya mashuti manne ambayo hayakulenga lango.


Simba ambao ni mabingwa watetezi kwa sasa wanajiandaa na mchezo wa ligi dhidi ya Mwadui FC utakaochezwa kesho, Oktoba 31 Uwanja wa Uhuru.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA