KUWAONA MASTAA WA SIMBA V MWADUI BUKU TANO TU


 KESHO Oktoba 31, Simba itakuwa na kazi ya kumenyana na Klabu ya Mwadui FC kwenye mchezo wa Ligi huku viingilio ikiwa ni buku 5,(5,000). 


Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Uhuru saa 10:00 jioni na unatarajiwa kuwa na ushindani mkubwa kwa timu zote mbili kutokana na matokeo ya timu hizo mbili.


Mwadui FC imetoka kupoteza kwa kufungwa mabao 6-1 dhidi ya JKT Tanzania Uwanja wa Mwadui Complex na Simba imetoka kupoteza kwa kufungwa bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting, Uwanja wa Uhuru.


Ikiwa ni buku 5 kwa mzunguko  VIP B ni shilingi 10,000 na 15,000 kwa VIP A. Kiingilio hicho kitatoa fursa kwa mashabiki kuona uwezo wa nyota wazawa ndani ya Simba inayoongozwa na John Bocco pamoja na uwezo wa kipa namba moja wa Mwadui FC, mzawa Mussa Mbissa.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO