YANGA YAIFUATA BIASHARA UNITED

 


KIKOSI cha Yanga leo Oktoba 30 kimeondoka Mwanza kwenda Musoma kwa ajili ya mchezo wa Ligi Kuu Bara unaotarajiwa kuchezwa kesho, Oktoba 31.


Mchezo huo utachezwa Uwanja wa Karume, Mara utakuwa ni wa nane kwa Yanga huku ukiwa ni wa tisa kwa Biashara United.


Timu zote mbili zipo ndani ya tano bora jambo linalomaanisha kwamba zote kwa msimu wa 2020/21 zipo vizuri na zitapambana kupata matokeo ndani ya uwanja.


Biashara United ambao ni wenyeji wapo nafasi ya tatu na kibindoni wamekusanya pointi 16 Yanga wapo nafasi ya pili wakiwa na pointi 19.


Kwa mujibu wa Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh amesema kuwa wachezaji wote wapo fiti isipokuwa nyota wao Haruna Niyonzima ana sumbuliwa na malaria.


Kocha wa Biashara United, Francis Baraza amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya mchezo huo wa kesho.



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO