Posts

Showing posts from May, 2020

SIMBA NA YANGA YAPIGANA VIKUMBU KUPATA SAINI ZA MITAMBO HII YA MABAO

Image
BIGIRIMAMA Blaise na Relliants Lusajo ni mitambo ya kucheka na nyavu inaotajwa kuingia anga za Klabu ya Yanga na Simba ambazo zina mpango wa kuboresha vikosi vyao msimu ujao. Nyota hawa wawili ni mitambo ya kutengeneza mabao ndani ya Namungo FC iliyo chini ya Kocha Mkuu Hitimana Thiery, raia wa Rwanda. Kwa ujumla wametupia jumla ya mabao 21 kati ya mabao 34, Blaise ametupia mabao 10 na Lusajo ametupia mabao 11 akiwa ni kinara ndani ya klabu hiyo. Akizungumza na Saleh Jembe, Lusajo amesema kuwa hana tatizo la kucheza timu ya Yanga ama Simba iwapo utaratibu utafuatwa atasaini.  "Ukiwa mchezaji hauchagui kambi, hivyo ikiwa Yanga ama Simba watahitaji saini yangu sina tatizo nao nitasaini iwapo utaratibu utafuatwa, kikubwa kwangu ni kucheza," amesema. Blaise amesema kuwa amekuwa akiskia habari hizo ila hajapata taarifa rasmi. Hassan Bumbuli, Ofisa Habari wa Yanga amesema kuwa hawezi kuzungumza kuhusu masuala ya usajili kwa sasa kwani wakati bado ila kinachofanyika ni

JADON SANCHO AFUNGA HAT TRICK YAKE YA KWANZA, ATUMA UJUMBE KUHUSU GEORGE FLOYD

Image
JADON Sancho, ameungana na dunia kiujumla kutetea haki ya George Floyd ambaye inaripotiwa kuwa aliuawa na Polisi mweupe wa Marekani kwa sababu za kiubaguzi wa rangi kwa kuwa yeye ni mweusi, mjini Minneapolis. Jana, Mei 31, Sancho alifunga hat trick take ya kwanza ndani ya Borussia Dortmund, wakati wakiinyoosha mabao 6-1 Padernborn kwenye mchezo wa Bundesliga. Muda wa kushangilia mshambulijaji huyo alionyesha fulana yenye maneno ya kuhitaji kuona haki ya Floyd inapatikana. Sancho alipachika mabao hayo dakika ya 57,74 na 90+2 huku mengine yalifungwa na Thorgan Hazard dakika ya 54, Achraf Hakimi ambaye ni beki dakika ya 85 naye aliungana na Sancho kwa kuonyesha t shirt yenye ujumbe sawa na Sancho, Marcel Schmelzer dakika ya 89 alipachika bao huku lile la Paderborn likipachikwa kwa penalti na Uwe Hunembeier dakika ya 72. Ushindi huo unaifanya Dortmund kufikisha pointi 60 ikiwa nafasi ya pili ikiachwa kwa pointi 7 na vinara ambao ni Bayern Munich wenye pointi 67 huku Paderborn iki

MUONEKANO WA UKURASA WA NYUMA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU

Image
MUONEKANO wa ukurasa wa nyuma gazeti la Championi Jumatatu, lipo mtaani jipatie nakala yako

SIMBA YATAJA SABABU YA KUTWAA UBINGWA WA LIGI KUU BARA

Image
FRANCIS Kahata, kiungo mshambuliaji wa Simba amesema kuwa ana matumaini makubwa ya Klabu yake kuchukua ubingwa kutokana na nafasi ambayo wapo kwa sasa. Simba ipo nafasi ya kwanza kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 28 kibindoni ina pointi 71. Tangu Machi 17 hakukuwa na shughuli za michezo baada ya kusimamishwa kutokana na janga la Virusi vya Corona. Serikali imeruhusu masuala ya michezo kuanza leo Juni Mosi huku ratiba ikieleza kuwa mechi za Ligi Kuu Bara, Ligi Daraja la Kwanza na la Pili zitaanza Juni 13. Kahata amesema:"Kuna ushindani mkubwa ambao upo lakini kwa kuwa tulikuwa sehemu nzuri imani ya kufanya vema ipo na nafasi ya kutwaa ubingwa pia. "Wachezaji tulikuwa tunafanya mazoezi wakati wa mapumziko yalisyosababishwa na Corona,tumerejea tutaendelea pale ambapo tuliishia," amesema. Kahata ni miongoni mwa nyota wa Simba ambao walisepa Bongo na kurejea kwao Kenya, alirejea Mei 31 na kuungana na wachezaji wenzake ambao waliripoti kambini Mei

RAIS WA AWAMU YA NNE, KIKWETE AKUMBUSHIA MAJARIBIO MAKUBWA YA MABADILIKO YALIYOPITA YANGA

Image
RAIS wa awamu ya nne ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Jakaya Kikwete amesema kuwa mataminio ya mabadiliko ndani ya Yanga ni safari a tatu kufanyika. Kikwete ameyasema hayo katika hafla ya kutiliana saini ya kuanza safari ya mabadiliko kati ya Yanga, GSM na La Liga ambayo imefanyika jana Hotel ya Serena na kurushwa moja kwa moja kupitia Azam TV na you tube chane ya Yanga. Kikwete amesema:- "Matamanio ya mabadiliko katika Klabu ya Yanga katika mfumo wa uendeshaji ni ya muda mrefu. Tunakumbuka wakati wa katibu George Mpondela (Castro) alikuja na mapendekezo ya Yanga Kampuni. "Jaribio kubwa, la pili ni wakati wa mwenyekiti Yusuph Manji alipokuja na dhana ya kukodisha, katika majaribio makubwa hili ni la tatu kwa kumbukumbu zangu, mengine yalikua ya katiba tu"amesema, Mwenyekiti wa Klabu ya Yanga, Mshindo Msolla amesema kuwa baada ya kutiliana saini ya makubaliano ni hatua ya kwanza kuelekea kwenye mabadiliko ambayo ni ndoto ya muda mrefu. Injinia, Hersi Said Mwakil

NYOTA MPYA YANGA BADO KIDOGO ASAINI,NDANI YA GAZETI LA CHAMPIONI JUMATATU

Image
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele gazeti la Championi Jumatatu lipo mtaani jipatie nakala yako na nafasi ya kushinda ndinga mpya ni yako 

GSM:TUNATAKA KUACHA ALAMA YANGA, SEVILLA WATATUNGAZIA NCHI, MKATABA WASAINIWA

Image
INJINIA Hersi Said,Mkurugenzi wa Uwekezaji GSM amesema kuwa mpango mkubwa wa kuwa wadhamini ndani ya Klabu ya Yanga ni kuona kwamba siku watakayoondoka wanaacha alama ndani ya Yanga. Hayo ameyazungumza leo kwenye ukumbi wa Serena kwenye hafla ya utiliaji saini kati ya Yanga, La Liga na GSM kuelekea safari ya mabadiliko ambapo mgeni rasmi ni Rais mstaafu wa awamu ya nne.Jakaya Kikwete.  "Tuna historia ya wadhamini wengi wa Yanga ambao waliwekeza kwa muda siku walipoondoka Yanga iliyumba, sisi hatuna mpango huo tunataka siku tutakayoondoka tuache alama ndani ya Yanga, tuache thamani ili Yanga isimame kwa miguu yake miwili. "Pia La Liga, kupitia Klabu ya Sevilla ya Hispania ni sehemu ya kuitangaza Tanzania kupitia utalii, mafanikio makubwa klabu yetu itapata iwapo tutaweza kushirikiana nao vizuri tutapata nafasi kubwa sana ya kuitangaza nchi yetu," amesema.  Tayari mkataba wa kuanza safari ya kuelekea kwenye safari ya mabadiliko umeshasainiwa ambapo Mshindo Msolla amb

SIMBA YATAJA SABABU YA MECHI ZAO 10 KUWA NGUMU

Image
JOHN Bocco, nahodha wa Simba amesema kuwa wana kazi kubwa ya kupambana kwenye mechi 10 kutokana na wapinzani wao kujipanga kupata matokeo. Simba imecheza mechi 28 za Ligi Kuu Bara kibindoni imejikusanyia pointi 71 na imefunga mabao 63 na imefungwa jumla ya mabao 15. Ligi Kuu inatarajiwa kuanza kutimua vumbi Juni 13 baada ya Serikali kuruhusu masuala ya michezo ambayo yalisimamishwa Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona. Bocco amesema:"Tuna kazi ngumu na kubwa kupambana kutafuta matokeo kwani mechi zetu nyingi zina ushindani mkubwa, ukizingatia kwamba kila timu inajua inahitaji nini. "Timu ambazo zinashuka ni nyingi nasi tunatakiwa tupambane ili kushinda haitakuwa kazi rahisi lakini tunaamini kwamba kwa kuwa tumeanza mazoezi basi tutafanya kazi," amesema. Simba ilianza mazoezi Mei 27 baada ya wachezaji kuripoti kambini rasmi.

YANGA: TUPO MIKONO SALAMA HATUJAKOSEA NJIA

Image
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mchakato wao wa mabadiliko ni ndoto yao ya muda mrefu hivyo wanaamini kwamba itafanikiwa bila mashaka yoyote yale kwa kuwa inasimamiwa na watu sahihi. Yanga leo inaendelea safari ya mabadiliko ambapo ipo kwenye mchakato wa kutiliana saini na Kampuni ya La Liga ya Hispania pamoja na GSM. Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mfumo ambao wanaufuata ni njia sahihi kufikia mafanikio yalipo. "Tupo sahihi na tunajua kile ambacho tunakifanya kikubwa tu mashabiki wawe pamoja nasi watupe sapoti katika kile ambacho tunakifanya kwani hatujakosea njia tupo mikono ya watu salama," amesema. Tukio hilo la makubaliano linarushwa leo moja kwa moja kutoka Serena Hotel kupitia Azam TV na Yanga TV.

MASHINE ILIYOINGIA SIMBA YAAHIDI UBINGWA,YANGA KUMEPAMBA MOTO, KESHO NDANI YA CHAMPIONI JUMATATU

Image
KESHO ndani ya Championi Jumatatu, usipange kukosa kupata nakala yako.

VIDEO:MASHARTI YALIYOTOLEWA NA SERIKALI KUHUSU MICHEZO

Image

VIDEO:PENALTI ZA MARCO MZUMBE NA SAID KATUNDU JR ZAWAPA USHINDI WASIOOA

Image

RATIBA YA MECHI ZILIZOBAKI KUTOLEWA KESHO

Image
BODI ya Ligi Tanzania imetoa taarifa kuwa ratiba ya mechi ambazo zilipangwa kutolewa leo itatolewa kesho Jumatatu, saa 4:00 asubuhi.

WAANDISHI WA HABARI WA TIMU YA WASIOOA WAWAFUNGA WALIOOA KWA PENALTI

Image
WAANDISHI wa Habari  Walioa wamepoteza kwa kufungwa kwa penalti 4-1 kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Wasioa uliochezwa leo Uwanja wa Chuo cha Sheria Ubungo baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana mabao 2-2.   Ibrahim Mohamed aliwatanguliza walioa kwa mabao yake mawili ya kipindi cha kwanza, kabla ya Abdulghafary Ally mwandishi wa gazeti la Championi alisawazisha bao moja kipindi hichohicho cha kwanza. Juma Ayo alifunga bao la pili kwa wasioa kipindi cha pili na kufanya ubao usomeke 2-2 na matokeo yakabaki hivyo hadi filimbi ya mwisho ya mwamuzi wa kati Heri Sasii inapulizwa.   Baada ya ushindi huo kocha wa wasioa FC, Wilson Oruma alisema: “Tulikua na kila sababu ya kushinda katika huu mchezo, kwa sababu moja kubwa tu, soka linachezwa na vijana, wazee kazi yao ni kuoga maji ya moto, kwahiyo kazi wanayo watafute kwa kujificha.” Kwa upande wa kocha wa walioa, Thabit Zakaria, (Zaka za Kazi), alisema: “Tumekubali kufungwa, lakini siku zote penati hazina mwenyewe, tul

SERIKALI YATOA MUONGOZO RASMI UTAKAOTUMIKA KWENYE MASUALA YA MICHEZO

Image
SERIKALI leo, Mei 31 imetoa mwongozo wa kufuata katika michezo ya ligi kuu za soka nchini ambazo zinatarajiwa kuanza Juni Mosi, 2020. Katibu Mkuu Wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo na MsemajI Mkuu wa Serikali, Dr. Hassan Abbas amesema kuwa ni muhimu kuzingatia na kwa yoyote atakayekiuka taratibu hizo hatua kali zitachukuliwa dhidi yake.

SASA MECHI KUPIGWA KAMA KAWAIDA, NYUMBANI NA UGENINI, VITUO HAKUNA

Image
RASMI sasa mechi zote zitachezwa kwa mtindo wa nyumbani na ugenini bila kuwepo vituo kama ambavyo awali ilielekezwa. Dr. Hassan Abass, Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni, Sanaa na Michezo amesema kuwa suala hilo limezingatia maoni ya Wizara ya Afya pamoja na wadau mbalimbali wa masuala ya michezo. "Serikali imeridhia mfumo wa michezo ya soka uchezwe kama ilivyokuwa ukifanyika awali, yaani kwa mfumo wa nyumbani na ugenini, kabla ya Virusi vya Corona. "Awali ilipangwa ichezwa kwa vituo na ilitokana na kuwepo kwa Virusi vya Corona lakini kwa kuwa hali inazidi kuwa shwari na Serikali imeridhia kuwe na mechi za nyumbani na ugenini kwa kila mechi ili kutoa burudani na furaha iendelee vilevile. "Jambo la msingi ni kuona kwamba utaratibu unafuatwa ikiwa ni pamoja na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona kwani licha ya kwamba hali imekuwa shwari lakini ni lazima kuchukua tahadhari,". Vituo ambavyo vilipangwa awali ilikuwa ni kwa Ligi Kuu Bara na Kombe

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

Image
DR.Hassan Abbas,Katibu Mkuu wa Wizara ya Habari, Utamaduni. Sanaa na Michezo amesema kuwa kuanzia ligi itakapoanza mashabiki ni ruksa kwenda viwanjani lakini kwa kuzingatia muongozo ambao umetolewa na Serikali. Awali baada ya Serikali kuruhusu kuanza kwa masuala ya michezo ifikapo Juni Mosi, ilitolewa taarifa kwamba mashabiki watakaoruhisiwa kwenda uwanjani ni 20 ambapo kila timu ingetoa mashabiki 10 na hii ilitokana na kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.  Leo, Mei 31, kwenye mkutano wa Waandishi wa Habari, uliofanyika Ukumbi wa Kimataifa wa Mwalimu Julius Kambarage Nyerere, Dr. Abbas amesema: "Serikali  imeridhia mashabiki watakaotaka kwenda uwanjani wanaruhusiwa kwenda kama utaratibu ulivyokuwa awali, kabla ya Virusi vya Corona, pia nyingine zitaonyeshwa ‘live’ kama kawaida, lakini lazima wafuate muongozo na kuchukua tahadhari dhidi ya Corona.  “ Kila uwanja, shabiki atapimwa joto na kwa upande wa mechi kubwa ambazo zitahusisha mashabiki wengi na kuleta changamot

YANGA YAPANGA KUSHTUA LEO BONGO NA LA LIGA

Image
UONGOZI wa Yanga umesema kuwa leo Mei 31 utashtua Bongo kutokana na yale watakayojadili wakati wa kukamilisha mchakato wa kutiliana saini mkataba wa kuelekea kwenye safari ya mabadiliko sambambana na La Liga pamoja na GSM . Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kwa wana imani kubwa ya kufika safari yao ya mabadiliko salama. “Tupo vizuri na tunapambana kuelekea kwenye safari ya mabadiliko, Mei 31 itakuwa ni hatua ya kutiliana saini kati ya Yanga, GSM na La Liga kutoka Hispania hivyo ni fursa kwa mashabiki kufuatilia kwa umakini na kuona mambo ambayo yatajadiliwa.  “Tumekuwa kwenye maandalizi kwa muda mrefu na hatimaye Mei 31 tutashtua wengi na kuanza ile safari ambayo tulikuwa tukiizungumzia kila siku, mambo yamekuwa mengi ila tunapambana ili kuweka kila kitu sawa. “Nina amini wengi wanahitaji kujua kutakuwa na kitu gani ila ukweli ni kwamba kutakuwa na vitu vingi ambavyo kwa sasa siwezi kuweka hadharani ila wasubiri kwan

DAH! KUMBE AZAM FC NDIO WAMEPANIA NAMNA HII....

Image
Kocha Msaidizi wa Azam FC, Vivier Bahati, amesema kuwa watafanya mazoezi mfululizo bila kupumzika ili kukifanya kikosi hicho kurudi kwenye ubora wake kabla ya kuanza mbio za kumalizia michezo 10 ya Ligi Kuu Bara waliyobaki nayo. Vivier raia wa Burundi, alisema ameridhishwa na namna ambavyo wachezaji wake wameanza mazoezi, hali inayoonyesha kuwa kila mchezaji alifuata vizuri program yake, ingawa bado kuna tatizo dogo la utimamu na nguvu kwenye miguu jambo ambalo linahitaji muda kidogo kuliweka sawa. Tangu Jumatano ya wiki hii, Azam FC walianza mazoezi wakijiwinda na michezo iliyosalia ambapo mbali na Ligi Kuu Bara wanaposhika nafasi ya pili, pia wana kibarua cha kucheza na Simba katika mechi ya robo fainali ya Kombe la FA. "Wengi wanaonekana kukosa nguvu za miguu kwa sababu wamekaa muda mrefu bila kucheza mpira, ila tumetenga siku 12 za kufanya kazi ngumu ambazo hizo zitawafanya wote wawe fiti na kufanya vizuri uwanjani. "Tunafanya mazoezi maalumu kwa ajili ya kuka

LUC EYMAEL ANAAMINI KAGERA SUGAR WALA SI TATIZO

Image
Kocha Mkuu wa Yanga, Luc Eymael, ametuma ujumbe mzito kwa wapinzani wake Kagera Sugar ambao watacheza nao katika robo fainali ya Kombe la FA akiwaambia analihitaji kombe hilo kwa nguvu zote, hivyo atawafunga tu. Kocha huyo amesema kwamba kile kilichotokea kwenye mechi ya Ligi Kuu Bara ambapo Yanga ilifungwa 3-0, hakitajirudia kwa sababu ya kulihitaji kombe hilo ili kupata nafasi ya kushiriki michuano ya kimataifa msimu ujao. Yanga na Kagera Sugar watapambana katika hatua ya robo fainali ya Kombe la FA ambapo mechi za hatua hiyo zimepangwa kupigwa kati ya Juni 27 na 28, mwaka huu jijini Dar. Eymael amesema uzuri ni kwamba atakuwepo katika mechi hiyo na ana uhakika wa kuiongoza timu yake kushinda kutokana na mipango yake ya kuelekea kuchukua ubingwa huo. “Nimepata taarifa za mechi hiyo na nimeona tumepangwa kucheza na Kagera Sugar. Najua katika mechi ya kwanza walitufunga lakini safari hii hawatusumbui, tutawafunga. “Ujue hili kombe ndiyo nafasi kwetu sisi kucheza kimataif

HIVI HAPA VIGONGO 10 VYA RUVU SHOOTING

Image
IKIWA imecheza mechi 28 Ruvu Shooting inayobebwa na serea ya 'Kupapasa Square' ipo nafasi ya 11 na kibindoni ina pointi 39. Imebakiza mechi zake 10 kukamilisha mzunguko wa pili msimu wa 2019/20 hizi hapa za Ruvu Shooting :-Simba SC KMC Ndanda Namungo Kagera Sugar Biashara United Mwadui FC Singida United Lipuli Mtibwa Sugar

MASHABIKI SASA KUPATA FURSA YA KUONA UHONDO WA FAINALI KOMBE LA FA

Image
IMEELEZWA kuwa fainali ya mchezo wa Kombe la FA inayotarajiwa kuchezwa Agosti Mosi, Uwanja wa Wembley itahudhuriwa na idadi ya mashabiki 20,000. Kwa sasa viongozi wanapambana kuona namna gani wanaweza kupata kibali hicho ili kupata kibali cha kuwa na mashabiki katika fainali hizo kutokana na janga la Virusi vya Corona kutibua mipango mingi katika soka. Ripoti zinaeleza kuwa moja ya kigezo ambacho kinatakiwa ili kupata kibali hicho ni pamoja na kupungua kwa maambukizi ya Virusi vya Corona mpaka kufikia asilimia 0.5 kwa muda ambao fainali itakaribia kupigwa. Hesabu kubwa ni kuwagawa mashabiki 20,000, ambapo kila upande utakuwa na mashabiki 10,000. Msimu huu zimebaki timu nane ndani ya FA ambapo Leicester City wao watamenyana na Chelsea, Newcastle United dhidi ya Manchester City, Sheffield United itamenyana na Arsenal huku Norwich itakutana na Manchester United hatua ya robo fainali. Kwa sasa imekuwa ngumu pia kwa mashabiki wa Premier kuona uhondo wa mechi zinazotarajiwa kuanza

MROMANIA WA AZAM FC KUANZA SAFARI YAKE NA GARI

Image
ARSTICA Cioaba, Kocha Mkuu wa Azam FC anatarajiwa kurejea muda wowote kuanzia sasa baada ya kibali cha kuja Bongo kupatikana na ataanza kwa usafiri wa gari mpaka nchi jirani na Ujerumani kabla ya kukwea pipa kuja Bongo. Kocha huyo kwa sasa yupo nchini Romania ambapo aliibukia huko baada ya masuala ya michezo kusimamishwa Machi 17 imekuwa ngumu kurudi mapema baada ya mipaka kufungwa. Ofisa Habari wa Azam FC, Thabit Zakaria amesema kuwa mpango wa kupata kibali kwa Cioaba umefanikiwa kinachosubiriwa ni siku ya kuja nchini. "Tayari kibali cha Cioba kuja nchini kimepatikana kwani sheria ya Romania alipo imekuwa ngumu kidogo, kocha atasafiri kwa basi kutoka hadi nchi jirani ya Ujerumani ambako ndege zimeanza kuruka. 'Muda wowote kuanzia sasa tuna uhakika wa kumpata Cioaba ndani ya Azam FC ili arejee kuendelea majukumu yake," amesema. Azam FC imeanza mazoezi chini ya Kocha Msaidizi,  Bahati Vivier huku ikiendelea kuchukua tahadhari dhidi ya Virusi vya Corona.

LIVERPOOL YAINGIA ANGA ZA ADAMA, MWILI JUMBA

Image
JURGEN Klopp,  Kocha Mkuu wa Liverpool yupo kwenye hesabu za kuinasa saini ya winga mwili jumba na mwenye kasi anayekipiga ndani ya Wolves, Adama Traore. Taarifa zinaeleza kuwa Kocha huyo anataka kuwapunguzia presha mastaa wake watatu wa mbele ambao ni Firmino,  Mo Salah na Sadio Mane. Kwa mujibu wa The Sun, Klopp amemuweka katika kipaumbele chake cha kwanza cha usajili winga huyo mwenye miguvu na thamani yake inatajwa kuwa milioni 60. Raia huyo wa Hispania amekuwa katika kiwango bora ndani ya Wolves msimu huu, mocha wake Nuno Espirito Santo amekuwa akimtumia zaidi pembeni.

ALLIANCE FC WAIPIGIA HESABU NDEFU NAMUNGO

Image
KESSY Mziray, Kocha Mkuu wa Klabu ya Alliance School amesema kuwa wameanza kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa hatua ya robo fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC. Mchezo huo unatarajiwa kucheza kati ya Juni 27/28 mwaka huu na mshindi atatinga hatua ya robo fainali. Mziray amesema kuwa anaamini Namungo ni timu bora na ina ushindani katika ligi hivyo mchezo utakuwa m mgumu na wenye ushindani.  "Nimekuwa na timu kwa muda mfupi nina  amini watafanya vizuri kwani inawezekana kupata matokeo chanya Kwenye mechi ngumu,". Bingwa mtetezi wa Shirikisho ni Azam FC.

KAGERA SUGAR YALIPIGIA HESABU KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
UONGOZI wa Kagera Sugar unesema kuwa utapambana kwa nguvu zote ili kusepa na Kombe la Shirikisho msimu huu ili waiwakikishe nchi kwenye michuano ya kimataifa. Kagera Sugar ilitinga hatua ya robo fainali kwa kuitungua KMC penalti 2-0 baada ya dakika 90 kukamilika kwa sare ya kufungana 1-1 itakutana na Yanga hatua ya nusu fainali kati ya Juni 27/28. Kocha Mkuu wa Kagera Sugar, Mecky Mexime amesema kuwa mipango yao ni kutwaa Kombe la Shirikisho ili wafikie hatua ya kuwa wa kimataifa. "Ninaiheshimu Yanga ambayo tumepangwa nayo kucheza baada ya droo ila kikubwa ambacho tunakihitaji ni Kombe la la Shirikisho ili tuwakilishe nchi kimataifa," amesema. Kwa sasa Kagera Sugar imeanza mazoezi kujiaanda kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara ambayo ilisimama tangu Machi 17 kutokana na janga la Virusi vya Corona na inatarajiwa kuanza Juni 13.

NAMUNGO:TUMEUKUMBUKA MPIRA

Image
ADAM Oseja, mlinda mlango namba mbili wa kikosi cha Namungo FC kilicho chini ya Kocha Mkuu, Hitimana Thiery amesema kuwa anafurahia kurejea kwa mechi za ushindani kwa kuwa walikuwa wameukumbuka mpira. Shughuli za michezo zilisimamishwa tangu Machi 17 na Serikali kutokana na janga la Virusi vya Corona ila kwa sasa Serikali imesema kuwa mambo yanaweza kuendelea huku tahadhari ikichukuliwa kuanzia Juni Mosi. Bodi ya Ligi Ligi Tanzania iliyo chini ya Shirikisho la Soka Tanzania (TFF) imesema kuwa masuala ya michezo yataanza Juni 13,2020. Akizungumza na Saleh Jembe, Oseja amesema kuwa muda mrefu walikaa bila kucheza mechi za ushindani jambo lililowafanya waukumbuke mpira. "Tulikaa muda mrefu bila kucheza ila sababu kubwa ilikuwa ni janga la Virusi vya Corona hatukuwa na namna ya kufanya, kwa kuwa mambo yanarejea tumefurahi tuliukumbuka mpira," amesema.

JEMBE LILILOTUA USIKU WA LEO SIMBA KUUNGANA NA WENZAKE MAZOEZINI

Image
FRANCIS Kahata, kiungo mshambuliaji wa Simba amerejea Bongo akitokea Kenya usiku wa kuamkia leo ataungana na wachezaji wenzake kwenye mazoezi ya leo yatakayofanyika kwenye uwanja wao uliopo Bunju. Kiungo huyo alikwama nchini Kenya baada ya mipaka kufungwa kutokana na janga la Virusi vya Corona jambo lililopelekea ugumu wa safari yake. Wachezaji wa Simba walianza mazoezi Mei 27 mara baada ya kuripoti kambini na kuanza mazoezi kwa ajili ya kujiandaa na mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho. Kiungo huyo ametupia mabao manne na kutoa pasi sita za mabao ndani ya Simba iliyofunga mabao 63.

MORRISON ATIKISA YANGA,NDANI YA SPOTIXTRA JUMAPILI

Image
MUONEKANO wa ukurasa wa mbele Gazeti la SPOTIXTRA Jumapili lipo mtaani usipange kukosa jipatie nakala yako jero kama jero.

TUSIJISAHAULISHE CORONA BADO IPO, KILICHOBAKI TUMALIZE MSIMU HUKU TUKICHUKUA TAHADHARI

Image
KUNAPOTOKEA tatizo lolote unaomba msaada na ukija huwezi kuchagua ni yupi anakuletea huo msaada. Unachotaka wewe ni kulitatua hilo tatizo lako ili maisha mengine yaendelee kama kawaida. Kuna wakati tunasema si wakati wa kuchagua kitu lazima ukubali na kile kinachotokea kwa wakati ule na hiyo haina namna. Tumekaa hapa kwa zaidi ya miezi miwili bila kucheza mpira wowote au hata kufanya mazoezi tukalalamika sana kuwa tunakumbuka mpira. Hali haikuwa nzuri wakati ule kutokana na janga la ugonjwa wa Corona na kweli wote tulikubali na tulipambana. Sasa hali imeanza kuwa shwali na kwa kuanzia Serikali imerejesha soka lianze kuchezwa kabla ya michezo mingine ili kuweza kuona itakuwaje kabla ya kuanza kwa michezo mingine. Sasa baada ya Serikali kuruhusu soka lichezwe kwa vituo viwili yaani Dar es salaam na Mwanza tayari watu wameanza kutoa maneno maneno kibao. Serikali imefanya kama ni msaada tu ili kumalizia msimu huu wa ligi sasa mnataka kuipangia kama mnavyotaka nyie. Hivi s

KIKOSI KAZI CHA KELVIN YONDANI WA YANGA KINA BALAA, WAWILI WA SIMBA NDANI

Image
HIKI ndicho kikosi cha kwanza cha mkongwe ndani ya Klabu ya Yanga anayekipiga pia ndani ya timu ya Taifa ya Tanzania Kelvin Yondani. Naye pia anaamini anastahili kuwa ndani ya kikosi hichi kutokana na uwezo wake, amewavuta wawili kutoka Simba namna hii:- Kipa-Metacha Mnata wa Yang. Beki wa kulia-Juma Abdul wa Yanga. Beki wa kushoto-Mohamed Hussein wa Simba. Beki wa kati-Bakari Mwamnyeto wa Coastal Union. Beki wa kati-Kelvin Yondan wa Yanga. Kiungo mkabaji-Papy Tshishimbi wa Yanga. Winga wa kulia-Mapinduzi Balama wa Yanga. Kiungo wa Kati- Haruna Niyonzima wa Yanga. Mshambuliaji-Ditram Nchimbi wa Yanga. Mshambuliaji-John Bocco wa Simba. Winga wa kushoto-Bernard Morrison wa Yanga.

AZAM FC IPO KAMILI GADOGADO

Image
MATAJIRI wa Dar es Salaam, Azam FC wameanza mazoezi kwa ajili ya kujiaandaa kumalizia vigongo vyao 10 ndani ya Ligi Kuu Bara pamoja na kutetea taji la Kombe la Shirikisho. Azam FC ilitwaa taji hilo msimu wa 2019 kwenye fainali iliyochezwa Lindi, ilikuwa dhidi ya Lipuli FC ya Iringa. Bao pekee la ushindi lilifungwa na Obrey Chirwa aliyeipoteza Lipuli mazima wakati huo ikiwa chini ya Seleman Matola ambaye kwa sasa anakinoa kikosi cha Simba. Mechi yao ya hatua ya robo fainali ndani ya Kombe la Shirikisho ni dhidi ya Simba. Ofisa Habari wa Azam FC, Zaka Zakazi amesema kuwa wanapo tayari kwa ajili ya ushindani hawana mashaka yoyote.