ALLIANCE FC WAIPIGIA HESABU NDEFU NAMUNGO

KESSY Mziray, Kocha Mkuu wa Klabu ya Alliance School amesema kuwa wameanza kufanya maandalizi kwa ajili ya mchezo wao wa hatua ya robo fainali wa Kombe la Shirikisho dhidi ya Namungo FC.

Mchezo huo unatarajiwa kucheza kati ya Juni 27/28 mwaka huu na mshindi atatinga hatua ya robo fainali.

Mziray amesema kuwa anaamini Namungo ni timu bora na ina ushindani katika ligi hivyo mchezo utakuwa m mgumu na wenye ushindani.

 "Nimekuwa na timu kwa muda mfupi nina  amini watafanya vizuri kwani inawezekana kupata matokeo chanya Kwenye mechi ngumu,". Bingwa mtetezi wa Shirikisho ni Azam FC.


Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO