YANGA YAPANGA KUSHTUA LEO BONGO NA LA LIGA



UONGOZI wa Yanga umesema kuwa leo Mei 31 utashtua Bongo kutokana na yale watakayojadili wakati wa kukamilisha mchakato wa kutiliana saini mkataba wa kuelekea kwenye safari ya mabadiliko sambambana na La Liga pamoja na GSM .
Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji na Msemaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kwa wana imani kubwa ya kufika safari yao ya mabadiliko salama.
“Tupo vizuri na tunapambana kuelekea kwenye safari ya mabadiliko, Mei 31 itakuwa ni hatua ya kutiliana saini kati ya Yanga, GSM na La Liga kutoka Hispania hivyo ni fursa kwa mashabiki kufuatilia kwa umakini na kuona mambo ambayo yatajadiliwa.
 “Tumekuwa kwenye maandalizi kwa muda mrefu na hatimaye Mei 31 tutashtua wengi na kuanza ile safari ambayo tulikuwa tukiizungumzia kila siku, mambo yamekuwa mengi ila tunapambana ili kuweka kila kitu sawa.
“Nina amini wengi wanahitaji kujua kutakuwa na kitu gani ila ukweli ni kwamba kutakuwa na vitu vingi ambavyo kwa sasa siwezi kuweka hadharani ila wasubiri kwani kila kitu kitarushwa ndani ya Azam TV na chaneli yetu ya Yanga TV,” alisema Nugaz.
Tukio hilo la kishtoria limepangwa kufanyika leo,Mei 31 Hoteli ya Serena iliyopo jijini Dar es Salaam na inatarajiwa kuhudhuriwa na baadhi ya Wabunge wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.


Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA