YANGA: TUPO MIKONO SALAMA HATUJAKOSEA NJIA


UONGOZI wa Yanga umesema kuwa mchakato wao wa mabadiliko ni ndoto yao ya muda mrefu hivyo wanaamini kwamba itafanikiwa bila mashaka yoyote yale kwa kuwa inasimamiwa na watu sahihi.

Yanga leo inaendelea safari ya mabadiliko ambapo ipo kwenye mchakato wa kutiliana saini na Kampuni ya La Liga ya Hispania pamoja na GSM.

Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa mfumo ambao wanaufuata ni njia sahihi kufikia mafanikio yalipo.

"Tupo sahihi na tunajua kile ambacho tunakifanya kikubwa tu mashabiki wawe pamoja nasi watupe sapoti katika kile ambacho tunakifanya kwani hatujakosea njia tupo mikono ya watu salama," amesema.

Tukio hilo la makubaliano linarushwa leo moja kwa moja kutoka Serena Hotel kupitia Azam TV na Yanga TV.


Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO