SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI
PRESHA kubwa kwa sasa ni kuelekea mchezo wa Ligi Kuu Bara kati ya Simba na Yanga unaotarajiwa kuchezwa Julai 3, Uwanja wa Mkapa kutokana na watani hawa wa jadi kuwa kwenye vita ya kusaka pointi tatu. Kikubwa ni kwamba mashabiki wanahitaji kuona mpira ukichezwa huku ile presha sijui ya timu moja haitaleta timu ikitakiwa kufutwa kwa kuwa timu yenyewe inayotajwa kuwa haitapeleka timu haijatoa taarifa rasmi. Jambo la msingi kuelekea kwenye mchezo huo kwa sasa kwa Shirikisho la Soka Tanzania ni kuangalia namna gani ratiba yao itakuwa na kuwasiliana pia na Serikali yasije kutokea yale ya Mei 8 ngoma ikabadilishwa wakati mashabiki wapo uwanjani. Kila kitu kipangwe vizuri na utaratibu uwekwe kwa kuwa nimeona kwa sasa tayari taarifa kuhusu zile tiketi na namna ya kuweza kuingia uwanjani zikiwa zimewekwa wazi. Kikubwa ambacho kinahitajika kwa mashabiki ambao watajitokeza Uwanja wa Mkapa kuacha kubeba matokeo uwanjani na kuendelea kufanya maandalizi yao kwa hesabu ili kupata pointi tatu.
Comments
Post a Comment