Posts

Showing posts from March, 2021

MAJEMBE HAYA YA KAZI YAMPA JEURI KOCHA YANGA

Image
  K OCHA Mkuu wa  Yanga, Juma  Mwambusi,  amesema kuwa  kama atawapata  wachezaji wake  wote waliokwenda  kuzitumikia timu  zao za taifa wakiwa  salama akiwemo staa  Saido Ntibazonkiza  na Mukoko Tonombe  basi anaamini  wataisaidia timu hiyo  katika michezo yao  inayofuata ya ligi.   Wachezaji wa Yanga  ambao walikwenda  kuzitumikia timu zao  za taifa ni pamoja na  Saido Ntibazonkiza  (Burundi), Tonombe  Mukoko (Congo)  na Haruna Niyonzima  (Rwanda), Feisal Salum,  Bakari Mwamnyeto na  Deus Kaseke wote kutoka  Tanzania. Mwambusi amesema kuwa,  hali ya kikosi chake  kilichopo kambini ipo sawa  kwa wachezaji  waliosalia  kambini huku  akisema kuwa  ana matumaini  na wachezaji  walioenda  kuzitumikia  timu za taifa  wakiwemo Saido,  Mukoko Tonombe. Anaamini kuwa ikiwa  watarejea  wakiwa   wataisadia Yanga  katika michezo inayofuata  ya Kombe la Shirikisho na  ligi kuu.   “Hali ya wachezaji wetu  kambini ni nzuri, wachezaji  wanaonyesha kufurahia  mazoezi, wanajituma tayari  kwa

NAMUNGO FC KAMILI GADO KUVAANA NA NKANA FC KWA MKAPA

Image
UONGOZI wa Namungo FC  umesema kuwa upo tayari kwa ajili ya mchezo  wao wa Kombe la  Shirikisho Afrika dhidi ya  Nkana ya Zambia.   Mchezo huo wa tatu  kwa timu hizo unatarajiwa  kupigwa kesho  Ijumaa, Aprili 2 katika Uwanja wa  Mkapa, Dar es Salaam.   Kwenye msimamo wa  kundi D la michuano hiyo,  Namungo inakamata nafasi  ya tatu baada ya kupoteza  michezo miwili ya kwanza.  Walifungwa bao  1-0 ugenini dhidi ya Raja  Casablanca ya Morocco na  kukubali kipigo cha mabao  2-0 nyumbani dhidi ya  Pyramids FC ya Misri.   Ofisa Habari wa Namungo,  Kindamba Namlia amesema:  “Maandalizi yapo vizuri na tunatambua kwamba tuna kazi ya kufanya Aprili 2 mbele ya Nkana FC.   “Kila kitu kinakwenda sawa na wachezaji wana morali kubwa ya kwa ajili ya kutafuta ushindi. Tupo nyumbani na tutatumia nafasi ya kuwa nyumbani kufanya vizuri,". Miongoni mwa nyota ambao wapo tayari kwa mchezo huo ni pamoja na Stephen Sey, Sixtus Sabilo, Shiza Kichuya, Humud.

SIMBA YAFUNGUKIA ISHU YA UTATA WA KAULI YA MO NA SportPesa

Image
  MJUMBE wa bodi ya Wakurugenzi wa Kampuni ya Klabu ya Simba, Mulami Ng’ambi amefafanua ujumbe wa mkurugenzi wake wa bodi, Mohammed Dewji baada ya kutwit na kueleza hisia zake juu ya uwekezaji wa mkataba mpya wa Klabu ya Manchester United na kuhusisha Simba na mkataba wa SportPesa. MO aliandika:- “Man Utd italipwa kiasi cha pauni milioni 305 ambazo ni sawa na Shilingi Bilioni 700 za kitanzania kwa miaka mitano kutoka kwa (Team Viewer). Simba ya Tanzania haipati hata asilimia moja ya hiyo pesa kutoka kwa wadhamini SportPesa (Asilimia moja ya hiyo pesa ni kiasi cha Bilioni 7 za kitanzania).”     Mulami amesema:-”Watu hawakumuelewa Mo Dewji.  Alichokimaanisha Mohamed Dewji alikuwa anamaanisha kwamba, hela ambayo ipo au inawekezwa kwenye mpira kama udhamini bado ni kidogo sana kulinganisha na nchi nyingine ambazo zinapata udhamini.     ”Nafikiri alisema Simba haipati asilimia moja ya udhamini ambayo Manchester United wanaipata katika mkataba mpya ambao wameisaini hivi karibuni. M

GAUCHO ATAJA SABABU ZA KUPOKEA KICHAPO CHA MABAO 6-0

Image
NAHODHA wa Twiga Stars, Mwanahamisi Omary ‘Gaucho’ baada ya kuanza vibaya kwenye mchezo wake wa kwanza katika Ligi Kuu nchini Morocco amesema kuwa ni matokeo mabaya ambayo watayafanyia kazi.  Ilikuwa ni kwenye mchezo wake wa kwanza akivaa uzi wa Chabab Atlas Khenifira Feminin alishuhudia timu yake ikipokea zigo la mabao 6-0 na AS-Far wakiwa ugenini. Gaucho ambaye alicheza dakika zote 90 amesema sababu ya kuchapwa sita kwenye huo ni kutokana na golikipa wao namba moja Chaimae Chawni kupigwa kadi nyekundu dakika za mapema, lakini pia wapinzani wao hao walipata penalti mbili za haraka haraka. Nyota huyo ambaye ni Mtanzania alikuwa akicheza timu ya Simba Queens alipewa jukumu la kuongoza mashambulizi kwenye timu hiyo akisaidiana na Rania Kostani na Nouhaila Oubail, wakitumia mfumo wa 4-3-3 kama ambao alikuwa anacheza akiwa na Simba, lakini dakika 90 ziliisha wakiwa vichwa chini. Gaucho amesema: “Mpira una matokeo matatu, kwahiyo sisi tulipata matokeo hayo baada ya dakika 90. Kikub

ORODHA YA NCHI AMBAZO ZIMEFUZU AFCON

Image
NCHI ambazo zimefunzu kushiriki Afcon ambayo itafanyika nchini Cameroon 2021 ambapo Tanzania imeishia hatua ya makundi kwa kukusanya pointi 7 ikiwa kundi J. Kwa ukanda wa Afrika mashariki timu zimekwama kutusua ambapo Kenya, Uganda, Rwanda, Burundi zimeishia hatua ya makundi. Hizi hapa:- Senegal.  Tunisia. Algeria.  Mali.  Burkina Faso.  Guinea.  Comoros.  Gambia.  Gabon. Misri. Ghana.  Equatorial Guinea.  Zimbabwe. Morocco. Ivory Coast. Nigeria.  Sudan. Malawi. Mauritania.  Ethiopia. Guinea-Bissau. Cape Verde. Sierra Leone. 

CHEKI MECHI ZA SIMBA NDANI YA APRILI KWENYE LIGI KUU BARA

Image
KIKOSI cha Simba kinachonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes kina mechi zake nne kwa mwezi Aprili kusaka pointi tatu muhimu katika Ligi Kuu Bara. Kwenye msimamo kipo nafasi ya kwanza na pointi zake ni 46 baada ya kucheza mechi 20. Ratiba yake ambayo imetolewa leo Machi 31 itaanza Aprili14 ni Simba v Mtibwa Sugar, Uwanja wa Mkapa. Mwadui FC v Simba itakuwa Aprili 18, Uwanja wa Kambarage. Kagera Sugar v Simba itakuwa ni Aprili 21, Uwanja wa Kaitaba. Gwambina v Simba ni Aprili 24, Uwanja wa Gwambina Complex. Simba v Dodoma Jiji itakuwa ni Aprili 27, Uwanja wa Mkapa.

RATIBA YA MECHI ZA YANGA LIGI KUU BARA APRILI

Image
KIKOSI cha Yanga kina kibarua cha kusaka pointi tatu kwenye mechi zake nne kwa mwezi Aprili baada ya leo Machi 31 ratiba kutoka. Hizi hapa ni mechi nne za vinara wa Ligi Kuu Bara wenye pointi 50 baada ya kucheza jumla ya mechi 23 namna hii:- Yanga dhidi ya KMC, Uwanja wa Mkapa itakuwa ni Aprili 10. Yanga dhidi ya Biashara United, itakuwa ni Aprili 17, Uwanja wa Mkapa. Yanga dhidi ya Gwambina, Aprili 20, Uwanja wa Mkapa Yanga dhidi ya Azam FC, Uwanja wa Mkapa, Aprili 25.

VURUGU ZA LIGI KUU BARA NI MPAKA JULAI BADALA YA KUISHA JUNI

Image
 ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania, (TPLB) amesema kuwa msimu wa 2020/21 utakamilika Julai tofauti na awali ambapo ulitarajiwa kukamilika Juni. Mabadiliko hayo ya muda wa ligi kukamilika yametokana na kutokea kwa msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli ambaye alitangulia mbele za haki Machi 17. Kutokana na msiba huo ambao ni mkubwa kwa Tanzania na Afrika kiujumla kulikuwa na siku 21 za maombolze ambazo zinaendelea mpaka wakati huu na zinatarajiwa kukamilika Aprili 7. Kasongo amesema:" Awali ligi yetu ya Tanzania Bara ilipaswa kumalizika tarehe 12 mwezi wa sita lakini kulingana na mabadiliko ligi itaisha tarehe 11 mwezi wa saba. "Hii inatokana na kuwa na mabadiliko ambayo yamefanyika kwenye ligi kuendena na siku 21 ambazo ni za maombolezo," . Leo TBLB imetoa ratiba ambayo inaonyesha kwamba Ligi Kuu Tanzania Bara pamoja na mechi za Kombe la Shirikisho zitarejea kuanzia Aprili 8. Kwa timu ambazo zitaangukia kucheza Playoff 2

SIMBA HATA HAWAJUI ALIPO MSHAMBULIAJI WAO LOKOSA

Image
  KOCHA Mkuu wa Klabu ya Simba, Didier Gomes amesema kuwa hajui alipo mshambuliaji wake Lokosa Junior. Junior raia wa Nigeria alisajiliwa na Simba kwa dili la miezi 6 na sababu kubwa ya usajili wake ni kwa ajili ya mashindano ya Ligi ya Mabingwa Afrika. Akiwa ndani ya kikosi cha Simba hajaweza kuonekana kwenye mechi ya ushindani ambapo Simba ikiwa imecheza mechi nne za Ligi ya Mabingwa Afrika hatua ya makundi hajacheza mchezo hata mmoja. Nafasi yake ya ushambuliaji amekuwa akianza Chris Mugalu pamoja na Meddie Kagere ambaye mechi nyingi amekuwa akianzia benchi huku John Bocco taratibu akirejea kwenye ubora wake. Katika mazoezi ya Simba ambayo yanaendelea kwenye viwanja vya Simba Mo Arena vilivyoppo Bunju, Lokosa hajaonekana mazoezini huku habari zikieleza kuwa amevunjiwa mkataba wake na mabosi hao wa mtaa wa Msimbazi. Kuhusu Lokosa, Gomes amesema:"Sijui kwa kweli kuhusu huyo, ila siwezi kulizungumzia jambo hilo ila ukweli ni kwamba sijamuona muda mrefu kwenye eneo la mazoe

UKANDA WA AFRIKA MASHARIKI MAJANGA MATUPU AFCON

Image
  UKANDA wa Afrika Mashariki mambo yamekuwa magumu kwenye mechi za kuwania kukata tiketi ya kufuzu kushiriki Michuano ya Mataifa ya Afrika, (Afcon) kwa timu nyingi kuangukia pua. Sare ya bila kufungana ndani ya dakika 90 dhidi ya Cameroon inaifanya timu ya Taifa ya Rwanda nayo pia kuishia hatua ya makundi. Ni Cameroon na Cape Verde wamekata tiketi ya kushiriki Afcon nchini Cameroon baada ya kuwa nafasi mbili za juu ambapo mwenyeji Cameroon ana pointi 11 huku Cape Verde akiwa na pointi 10. Rwanda ipo nafasi ya 3 na pointi zao ni 6 huku nafasi ya nne ikiwa mikononi mwa Msumbiji wenye pointi 4 baada ya kucheza jumla ya mechi 6. Tanzania pia imeishia hatua ya makundi na pointi zake ni 7 katika kundi J ipo nafasi ya tatu ambapo ni Tunisia wenye pointi 16 na Equatorial Guinea wenye pointi 9 wamepenya mpaka Cameroon.  Burundi katika kundi E wapo nafasi ya tatu na pointi zao ni 5 huku Morocco yenye pointi 14 na Mauritania wenye pointi 9 wakitusua mpaka Cameroon.  Kenya katika kundi G

BODI YA LIGI YATAJA SIKU YA MECHI ZA LIGI KUU BARA PAMOJA NA KOMBE LA SHIRIKISHO KUANZA

Image
ALMAS Kasongo, Mtendaji Mkuu wa Bodi ya Ligi Tanzania,(TPLB) amesema kuwa Ligi Kuu Tanzania Bara inatarajia kuendelea Aprili 8 baada ya kutimiza siku 21 za maombolezo. Ligi ilisimama kwa muda kutokana na msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, Hayati John Joseph Magufuli ambapo zilitolewa siku 21 za maombolezo. Magufuli alitangulia mbele za haki Machi 17 jambo lilipolekea Serikali kutoa siku 21 za maombolezo ambazo bado zinaendelea kwa sasa. Kasongo amesema:- "Ukitazama ratiba yetu ile ya awali ambayo tuliitoa kwa vilabu ilikuwa inaonyesha kwamba tarehe 3-4 Machi, michezo ya Kombe la Shirikisho, tarehe 6-8 Machi tulikuwa tunarejea kwenye mechi za ligi. "Kutokana na msiba tafsiri yake ni kwamba ile michezo ya Shirikisho na ile ya ligi nayo inakuwa haipo kwa sababu tupo kwenye maombolezo ya siku 21. "Kumbuka kwamba siku 21 zinaisha tarehe 7 ambapo kulikuwa na mchezo wa ligi, tarehe 6 kulikuwa na mchezo wa ligi na tarehe 3-4 kulikuwa na mchezo wa Kombe la Shirikish

KOCHA BIASHARA UNITED KUANZA KUONGEZA MAKALI YA WASHAMBULIAJI

Image
 KOCHA Mkuu wa timu ya Kagera Sugar, Francis Baraza amesema kuwa kazi ya kwanza atakayoanza nayo kwa sasa ni kushughulika na safu ya ushambuliaji ili irejeshe makali yake. Baraza amechukua mikoba ya Mecky Maxime ambaye alifutwa kazi kutokana na mwendo mbovu wa timu yake na mchezo wa mwisho kukaa benchi ilikuwa mbele ya Azam FC ambapo ubao wa Kaitaba ulisoma Kagera Sugar 1-2 Azam FC. Kwa sasa Maxime yupo huru ambapo amekuwa akitajwa kuibukia Biashara United kuchukua mikoba ya Baraza. Akizungumza na Saleh Jembe, Baraza amesema kuwa amewatazama washambuliaji wake walivyo na ameona ni lazima aanze nao ili kuongeza kasi kwenye ushambuliaji. "Ili timu ipate ushindi ni lazima ifunge na ufungaji unaanzia kwa washambuliaji pamoja na viungo ambao kazi yao ni kutengeneza nafasi za kufunga kwa washambuliaji. "Kikubwa ambacho nina amini kwamba kinawezekana ni kupata matokeo katika mechi zetu hivyo mashabiki watupe sapoti bila kuwa na mashaka nasi," . Kagera Sugar kwenye msima

USHINDI WA MABAO 14 WA TIMU YA TAIFA JAPAN WAWEKA REKODI

Image
  TIMU ya Taifa ya Japan, imeweka rekodi ya kupata ushindi mkubwa ambao haujawahi kutokea ndani ya dakika 90 katika harakati za kuwania kufuzu Kombe la Dunia. Ushindi wa mabao 14-0 dhidi ya Mongolia walioupata Jumanne ya Machi 30 unawafanya wawe kwenye rekodi hiyo tamu huku wakiwa na nafasi ya kufuzu kushiriki Kombe la Dunia kwa mara ya 7. Walikuwa hawajacheza tangu Novemba 2019 kutokana na janga la Virusi vya Corona.  Mchezo huo uliochezwa Uwanja wa Fuku-Ari dakika 90 wapinzani wa Japan walikamilisha bila kupiga shuti hata moja lililolenga lango huku Japan ikipiga jumla ya mashuti 25 ambayo yalilenga lango la wapinzani hao  Matokeo hayo yanaifanya Japan kuwa nafasi ya kwanza katika kundi F na pointi zao ni 15 baada ya kucheza mechi 5 huku Mongolia ikiwa nafasi ya tano na pointi zao ni 3 baada ya kucheza mechi 7. Mshambuliaji wa Southampton ambaye yupo huko kwa mkopo akitokea Klabu ya Liverpool, Takumi Minamino alifungulia mvua ya mabao dk 13 kwenye mchezo huo. Kazi ikaendela k

KOCHA WA TIMU YA TAIFA YA BEACH SOCCER HAJARIDHISHWA NA USHINDI WA MABAO 8-3

Image
  BONIPHACE Pawasa, Kocha Mkuu wa timu ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer) amesema kuwa hajaridhishwa na ushindi wa mabao 8-3 walioupata dhidi ya Burundi. Mchezo huo ambao uliokuwa na ushindani mkubwa ulichezwa jana, Machi 30  ulikuwa ni maalumu kwa ajili ya kuwania tiketi ya kufuzu Afcon uliochezwa kwenye fukwe za Coco Beach, Dar. Pawasa amesema kuwa kwa namna ambavyo walijiandaa aliamini kwamba wangepata ushindi mkubwa zaidi ya huo ili kuongeza hali ya kujiamini kwa vijana wake. "Tulifanya maandalizi makubwa na mazuri jambo ambalo lilitupa matumaini kwamba tungepata ushindi mkubwa zaidi ya huu ambao tumeupata. "Kwa kuwa kuna makosa ambayo tumeyaona tutayafanyia kazi ili wakati ujao tuweze kupata matokeo mazuri zaidi ya hapa. "Ninawapongeza vijana kwa kazi ambayo wameifanya pamoja na sapoti ya mashabiki ambao wamekuwa wakitupa nguvu sisi kufanya vizuri,". Mchezo mwingine wa marudio dhidi ya Burundi unatarajiwa kuchezwa Aprili 3,2021

MICHAEL SARPONG ANAPENDA KUFUNGA

Image
  MICHAEL Sarpong, mshambuliaji wa Klabu ya Yanga amesema kuwa kitu ambacho anakipenda kukifanya akiwa uwanjani ni kufunga mabao kwa ajili ya timu yake. Nyota huyo raia wa Ghana ni ingizo jipya ndani ya kikosi cha Yanga kilicho chini ya Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi aliyechukua mikoba ya Cedric Kaze aliyefutwa kazi Machi 7. Aliibuka Yanga akitokea Klabu ya Rayon Sports ya Rwanda na kusaini dili la miaka miwili kuwatumikia Wanajangwani. Yanga ikiwa imetupia jumla ya mabao 36  kwenye Ligi Kuu Bara baada ya kucheza mechi 23 amehusika katika mabao matano ambapo amefunga mabao manne na kutoa pasi moja ya bao. Sarpong amesema:-"Nikiwa uwanjani ninapenda kufunga na kuipa ushindi timu yangu hakuna jambo jingine ambalo huwa ninapenda. Ikitokea nikashindwa basi nitatengeneza nafasi kwa mwenzangu. "Ukweli ni kwamba mashabiki wanapenda kuona timu ikishinda hilo ninalijua hata mwalimu pia amekuwa akituambia suala hilo, imani yangu nitafanya hivyo katika mechi zetu zijazo,"

MFARANSA WA SIMBA AFICHUA KINACHOWABEBA KIMATAIFA

Image
DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kikubwa ambacho kinawapa nguvu ya kuamini kwamba watapata matokeo mbele ya AS Vita ni pamoja na hali ya kujiamini na maandalizi mazuri. Kikosi cha Simba kinatarajiwa kumenyana na AS Vita kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika unaotarajiwa kuchezwa Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.   Mfaransa huyo ameongeza kwamba kuchukulia siriazi na kujiamini katika mechi zao ndiyo kitu ambacho kimekuwa kikiwabeba na kuifanya timu hiyo kutopoteza mechi yoyote hadi sasa katika Ligi ya Mabingwa Afrika.   Simba ni vinara wa Kundi A la Ligi ya Mabingwa Afrika watakuwa uwanjani kupambana na Vita katika mechi ambayo Simba wakitoa sare tu watajihakikishia nafasi ya kwenda hatua ya robo fainali, lakini Vita wanahitaji ushindi tu ili wafufue matumaini yao ya kutinga robo fainali.    Gomes  amesema kwamba kila mechi ambayo wamekuwa wakiicheza katika hatua hiyo wamekuwa wakiamini kwamba wanaweza kupata matokeo na hiyo imekuwa msaada mkubwa kwao.   "Mchezo

MANCHESTER UNITED YATAJWA KUISAKA SAINI YA ARGUERO

Image
BAADA ya mshambuliaji wa bora wa muda wote ndani ya Klabu ya Manchester City, Sergio Arguero kuripotiwa kwamba anaodoka ndani ya kikosi hicho msimu huu mkataba wake utakapoisha, Klabu ya Manchester United inapewa nafasi ya kupata saini yake. Arguero ndani ya Etihad ameshamalizana na mabosi wake na kupitia kikao ambacho walikaa pamoja na Kocha Mkuu wa timu hiyo Pep Guardiola na mabosi wa timu hiyo iliwapa nafasi mabosi wake kutangaza kwamba hatakuwa pamoja nao msimu ujao. City waliweka wazi Machi 29 kwamba hawatakuwa na nyota huyo ambaye amedumu kikosini hapo kwa muda wa misimu 10 akiwa na rekodi ya kucheka na nyavu mara 257 katika michuano yote na mkataba wake unameguka Juni, mwaka huu. Kwa mujibu wa Foot Mercato imeripoti kwamba raia huyo wa Argentina ana ofa nyingi mkononi ikiwa ni pamoja na ile ya kutoka kwa Manchester United.

AS VITA WAPINZANI WA SIMBA KIMATAIFA WAANZA KUMWAGA SABABU KIBAO

Image
  ZIKIWA zimesalia siku chache kufikia siku ya mtanange kati ya Simba na AS Vita, Kocha Mkuu wa AS Vita kutoka nchini DR Congo, Florent Ibenge ameweka wazi kuwa ratiba yake ya sasa si rafiki kwa klabu hiyo kuelekea mchezo wao dhidi ya Simba. Ibenge ukiachana na kuwa kocha wa AS Vita, pia ni kocha mkuu wa kikosi cha timu ya taifa ya Congo ambapo Jumatatu aliongoza taifa la Congo katika mchezo wao wa mwisho wa kufuzu michuano ya mataifa ya Afrika dhidi ya Gambia. Kwenye mchezo huo Ibenge alishuhudia kikosi chake kikishinda bao 1-0 ila kilikwama kufuzu Afcon nchini Cameroon kwa kuwa kipo nafasi ya tatu.   Ibenge amesema kuwa ratiba ya mechi za timu za taifa na michuano ya Ligi ya Mabingwa imebana sana kiasi cha kukosa siku za kutosha kwake kukiandaa kikosi cha AS Vita kuelekea mchezo wao unaofuata wa michuano ya Ligi ya Mabingwa dhidi ya Simba.     “Ratiba si rafiki kwetu, nadhani hii ni kwa klabu nyingi zinazoshiriki Ligi ya Mabingwa, ukiangalia mechi za timu za taifa na ile

EYMAEL: KUIFUNGA SIMBA MBELE YA JPM NI KUMBUKUMBU KWANGU NA WACHEZAJI

Image
 LUC Eymael, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2019/20 amesema kuwa moja ya kitu ambacho anakikumbuka muda wote ni ushindi wake mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa. Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkaa, Machi 8,2020 na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Simba. Bao pekee ambalo alilishuhudia pia aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli lilipachikwa kimiani na Bernard Morrison na kuwafanya Simba ayeyushe pointi tatu. Kwa sasa baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki Machi 17,2021 Samia Suluhu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa katiba ambapo awali alikuwa ni makamu wa JPM. Leo Machi 30, Samia amemchagua Philip Mpango awe Makamu wa Rais wa Tanzania ambapo jina lake limepitishwa na Wabunge kwa asilimia 100. Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael ambaye kwa sasa yupo Ubelgiji amesema kuwa anakumbuka mchezo huo kwa namna ambavyo Magufuli aliweza kuhudhuria na timu yake ilishinda jambo ambalo halifutiki

AS VITA : TUNAIFUNGA SIMBA TUKIJA TANZANIA

Image
  M SHAMBULIAJI wa  AS Vita, Ducapel  Moloko, amewapiga  mkwara mzito  Simba kwa kusema  kuwa watachukua alama tatu  watakapokutana uwanjani  Jumamosi hii.   Kauli hiyo ameitoa zikiwa zimebaki  siku chache kabla timu hizo  hazijavaana kwenye mechi ya hatua  ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika  itakayochezwa wikiendi hii kwenye  Uwanja wa Mkapa, Dar.  Moloko amesema kuwa,  wamejipanga kuchukua ushindi kwa  Simba ili kutengeneza nafasi ya kufuzu  hatua ya makundi. “Sisi tumejiandaa na tutaifunga  Simba ikiwa nyumbani kwao na alama  zote tutazichukua, subiri tuje mtauona  moto wetu,” alisema mshambuliaji  huyo.   Katika michuano hiyo, Simba ndiyo  vinara wa Kundi A wakiwa na pointi  10, wakifuatiwa na Al Ahly yenye  saba, huku AS Vita ikijikusanyia pointi  nne na Al Merrikh moja.  Timu zote  zimecheza mechi nne zikibakiwa na  mbili kukamilisha hatua hiyo kabla ya  kwenda robo fainali ambapo Simba inahitaji pointi moja ili kuweza kutinga hatua hiyo.

AZAM FC WAANZA KULIFUKUZIA JAMBO LAO

Image
  THABIT Zakaria, Ofisa Habari wa Azam FC amesema kuwa muda wa mapumziko kwa wachezaji wa timu hiyo umekwisha hivyo wanarejea mazoezi kuanza kazi ya kulikimbizia jambo lao waliloanza nalo mwanzoni mwa msimu wa 2020/21. Wachezaji wa Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina walipewa mapumziko kutokana na maombolezo ya msiba wa aliyekuwa Rais wa awamu ya tano, John Pombe Magufuli kilichotokea Machi 17. Akizungumza na Saleh Jembe, Zakaria amesema kuwa tayari muda ambao waliwapa wachezaji kwa ajili ya mapumziko umekwisha hivyo wamerejea kuanza kufanya mazoezi. “Tupo salama na tunahitaji kutimiza jambo letu. Kwa sasa tumeanza mazoezi kwa kuwa muda ambao tulitoa kwa ajili ya mapumziko kwa wachezaji umekwisha,” amesema. Kwenye msimamo wa ligi, Azam FC ipo nafasi ya tatu ikiwa imecheza jumla ya mechi 24 ina pointi 44 kibindoni kinara ni Yanga mwenye pointi 50 baada ya kucheza mechi 23.

VIDEO: MFARANSA WA SIMBA GOMES AZITAKA POINTI TATU ZA AS VITA

Image
KOCHA Mkuu wa Simba, Didier Gomes, raia wa Ufaransa amesema kuwa maandalizi ambayo wanayafanya kwa sasa kwa ajili ya mchezo wao wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya AS Vita ya Congo yanakwenda vizuri na wana amini kwamba watapata matokeo chanya.  Simba inaendelea na mazoezi kwenye Viwanja vya Simba Mo Arena ambapo wanatarajiwa kucheza na AS Vita, Aprili 3, Uwanja wa Mkapa.  Gomes amesema kuwa anahitaji kushinda kwenye mchezo huo ili kupata pointi tatu muhimu.  

MAPINDUZI BALAMA, DICKSON JOB KAMILI GADO KWA KAZI YANGA

Image
  KAIMU Kocha Mkuu wa Yanga, Juma Mwambusi amesema kuwa maendeleo ya nyota wake ambao walikuwa wakisumbuliwa na majeraha ikiwa ni pamoja na Mapinduzi Balama, Dickson Job yamezidi kuimarika. Job alikuwa anasumbuliwa na majeraha ya nyama za paja ambayo aliyapata kwenye timu ya taifa ya Tanzania, Taifa Stars ila kwa sasa amerejea kwenye ubora wake na kuanza mazoezi. Balama alikuwa nje kwa muda mrefu akitibu majeraha ya kisigino aliyoyapata msimu wa 2019/20 aliyoyapata kwenye mazoezi ya maandalizi ya mchezo wa Ligi Kuu Bara ilikuwa dhidi ya Ndanda FC. Tayari naye ameanza kupewa program maalumu ambayo itaweza kumrejesha uwanjani kuendelea na majukumu yake. Mwambusi amesema:"Kila mchezaji anaonekana kuwa na furaha na taratibu wale ambao hawakuwa fiti wanarudi, Mapinduzi Balama amepewa program maalum huku wachezaji wengine wakiwa wameanza mazoezi. "Fiston naye kwa sasa anaendelea vizuri ni jambo jema kwetu na tunaamini wale wengine ambao hawajawa kwenye ubora wataimarika,&qu

AS VITA: YAPIGA HESABU KUIFUNGA SIMBA KWA MKAPA

Image
  FLORENT Ibenge, Kocha Mkuu wa AS Vita amesema kuwa watapambana kupata matokeo chanya kwenye mchezo wao dhidi ya Simba ili waweze kutimiza malengo ya kutinga hatua ya robo fainali kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. AS Vita inakumbuka kwamba ilipokutana na Simba mchezo wa kwanza wa Ligi ya Mabingwa Afrika ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba. Bao lililowapa Simba pointi tatu lilifungwa na Chris Mugalu kwa mkwaju wa penalti na kuwafanya wasepe ugenini wakiwa kifua mbele. Kwenye msimamo wa kundi A, AS Vita ina pointi nne huku Simba ikiwa na pointi 10 inaongoza kundi inafuatiwa na Al Ahly nafasi ya pili yenye pointi 7. Imekuwa ikipata matokeo ugenini AS Vita kwa kuwa pointi zote nne ilikusanya ugenini ilishinda mbele ya Al Merrikh inayoshika nafasi ya nne na pointi moja na ililazimisha sare mbele ya Al Ahly. Ibenge amesema:"Tunahitaji kushinda mchezo wetu ujao wa Ligi ya Mabingwa Afrika kwa sababu uhitaji wetu ni kuona kwamba tunaweza kutinga hatua ya robo fainali. "Wapinzani w

KOCHA MPYA YANGA ATOA NENO LA MATUMAINI

Image
BAADA ya kupewa dili la miezi mitatu kuinoa Klabu ya yanga, kocha mpya wa makipa  Razak Siwa amesema kuwa anaamini atafanya kazi kwa ushirikiano mkubwa na wachezaji pamoja na benchi la ufundi. Kocha huyo raia wa Kenya alitambulishwa rasmi jana, Machi 29 na tayari ameanza kazi ya kukinoa kikosi hicho kinachosimamiwa na Kaimu Kocha Mkuu, Juma Mwambusi. Mwambusi amechukua mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7,2021 kutokana na matokeo mabovu kwa mujibu wa mabosi wa Yanga ambapo mzunguko wa pili kwenye mechi 6 alishinda moja na kuambulia kichapo moja huku nne akiambulia sare. Nizar Khalfan ambaye alikuwa msaidizi wake naye alifutwa kazi huku kocha wa makipa Niyonkuru raia wa Burundi naye akichimbishwa na nafasi yake imechukuliwa na Siwa. Siwa amesema:"Nimefurahi kuwa hapa na nitatoa ushirikiano mkubwa na kila mchezaji pamoja na uongozi kiujumla," .

ORODHA YA WACHEZAJI WA SIMBA WALIOANZA MAZOEZI KUWAVUTIA KASI AS VITA

TIMU YA TAIFA KAZINI LEO KUWANIA KUFUZU AFCON

Image
  TIMU ya taifa ya Tanzania ya Soka la Ufukweni, (Beach Soccer), inayonolewa na Kocha Mkuu Boniphace Pawasa leo itakuwa na kazi ya kusaka ushindi dhidi ya timu ya taifa ya Burundi. Mchezo huu ni maalumu kwa ajili ya kufuzu AFCON kwa timu za Beach Soccer ambapo mechi zote mbili zitachezwa Dar. Akizungumza na Saleh Jembe, Pawasa amesema kuwa wanachosubiri kwa sasa ni muda wa kuingia uwanjani kukamilisha kazi ambayo wameifanya kwa muda mrefu. “Kwa sasa tunasubiri muda wa kuingia uwanjani kumaliza kazi ambayo tumeifanya kwa muda mrefu. Tupo tayari kupata matokeo na imani yetu hatutawaangusha Watanzania vijana wanaonekana wana kitu kikubwa. “Kile ambacho ninawapa vijana wanaonekana kuelewa na kukifanyia kazi, nimewaambia kwamba wanapaswa wajiamini katika kusaka ushindi, hivyo ninawaamini katika hilo hawatakosea,” amesema. Mchezo wa leo utachezwa katika uwanja uliopo kwenye fukwe ya Coco Beach majira ya saa 10:00 jioni.

VIDEO: SIMBA WAPIGA MAZOEZI KWENYE MVUA, WASHINDA MABAO 2-1

Image
MASTAA wa Simba inayonolewa na Kocha Mkuu, Didier Gomes wameanza mazoezi kwenye Uwanja wa Simba Mo Arena uliopo maeneo ya Bunju, jana Machi 29, walifanya mazoezi hayo licha ya mvua kunyesha na walicheza mchezo wa kujipima nguvu na Simba B ambapo Simba ilishinda mabao 2-1.  Haya ni maandalizi kwa ajili ya mechi za kimataifa pamoja na Kombe la Shirikisho ambapo Aprili 4 itakuwa na mchezo wa kimataifa dhidi ya AS Vita utakaochezwa Uwanja wa Mkapa.  

MSHAMBULIAJI WA MILIONI 30 ATUMIA DAKIKA 278 KUFUNGA BAO MOJA YANGA

Image
  NYOTA wa Yanga, Wazir Junior ambaye ni ingizo jipya kutoka Klabu ya Mbao FC ambaye alisaini dili la miaka miwili kwa dau la milioni 30 ametumia dakika 278 kupachika bao moja la ushindi kwenye mechi zake zote za ushindani alizocheza. Mbele ya KMC wakati Yanga ikishinda mabao 2-1, Uwanja wa CCM Kirumba zama za Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7 aliyeyusha dakika 81 na alifunga bao lake la kwanza. Mechi yake ya pili ilikuwa mbele ya Biashara United wakati Yanga ikishinda bao 1-0 Uwanja wa Karume, alitumia dakika 60 wakati Yanga ikilazimisha sare ya bila kufungana na Gwambina, Uwanja wa Gwambina Complex alitumia dakika 58. Wakati Yanga ikichezeshwa pira gwaride Uwanja wa Nelson Mandela na ubao kusoma Tanzania Prisons 1-1 Yanga alitumia dakika 13. Uwanja wa Amaan kwenye Kombe la Mapinduzi alitumia dakika 57 wakati Yanga ikilazimisha sare ya bila kufungana na Jamhuri na mchezo wa fainali mbele ya Simba alitumia dakika 7 ubao ulisoma 0-0. Mchezo wake wa mwisho mbele ya Polisi Ta

RATIBA YA SIMBA APRILI NI MOTO, CHEKI VIGONGO VILIVYO

Image
  DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa kikosi cha Simba ana kazi ya kufanya ndani ya Aprili kukiongoza kikosi chake kusaka pointi tatu kwenye mechi zake 6 ambazo ni dakika 540 za moto. Mechi hizo ni dhidi ya AS Vita Club Aprili 3, mchezo wa kwanza walipokutana nchini DR Congo, ubao ulisoma AS Vita 0-1 Simba, Al Ahly ya Misri Aprili 9, mchezo wa kwanza ubao ulisoma Simba 1-0 Al Ahly, hizi mbili ni dakika 180 za kwenye Ligi ya Mabingwa Afrika. Kwa upande wa Ligi Kuu Bara atakuwa na kazi mbele ya Kagera Sugar, Aprili 14, Uwanja wa Kaitaba na mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja Wa Uhuru ubao ulisoma Simba 2-0 Kagera Sugar. Pia ana kazi mbele ya Dodoma Jiji ni Aprili 18, mchezo wa kwanza Uwanja wa Jamhuri, Dodoma Simba ilishinda mabao 2-1, Coastal Union ni Aprili 25 mchezo wa kwanza walipokutana Uwanja wa Sheikh Amri Abeid, Simba ilishinda kwa mabao 7-0.  Funga kazi kwa Gomes itakuwa ni Aprili 28 dhidi ya Mtibwa Sugar ambapo Simba ilipokutana kwenye mchezo wa kwanza Uwanja wa Jamhuri, Morogo

MRITHI WA KAZE NI MAALUMU KWA AJILI YA CAF

Image
  SEBASTIAN Migne, raia wa Ufaransa anapewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7,2021 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na mwendo mzuri. Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa za Migne kuletwa ni kwa ajili ya mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) ikiwa ni ile ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika.  Imani kubwa ya Yanga ni kwamba wana nafasi ya kushiriki mashindano hayo msimu ujao kwa kuwa wanaamini wapo kwenye nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara pamoja na lile la Shirikisho.  Yanga ina pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 wanaongoza ligi wakifuatiwa na mabingwa watetezi Simba wenye pointi 46 baada ya kucheza mechi 20. Migne aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Kenya na timu ya Taifa ya Equatorial Guinea. Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Yanga, Dominic Albinius aliweka wazi kuwa mchakato unaendelea na atakayekuja ni kocha mwenye uzoefu. Kwa sasa Yanga ipo mik

MTAMBO WA MABAO SERGIO AGUERO ANASEPA MANCHESTER CITY MAZIMA

Image
  SERGIO Aguero, mshambuliaji wa Manchester City ataondoka mwishoni mwa msimu huu baada ya mabosi wa timu yake kuweka wazi suala hilo kwa kuwa hatuongezewa mkataba. Arguero alijiunga  na Manchester City akitokea Klabu ya Atletico Madrid kwa dau la pauni milioni 35 na anapewa nafasi ya kunyanyua taji la tano la Ligi Kuu England kwa kuwa amenyanyua mataji manne, FA taji moja, League Cup mara tano. Nyota huyo mwenye miaka 32 amekuwa imara uwanjani akifunga jumla ya mabao 257 kwenye mashindano yote akiwa amecheza jumla ya mechi 384 anatajwa kuwekwa kwenye rada za Barcelona na Inter Milan ambao wanahitaji saini yake. Mkataba wa raia huyo wa Argentina unameguka msimu huu. Mchezo wake wa kwanza ndani ya City ilikuwa dhidi ya Swansea, Uwanja wa Etihad wakati ubao ulisoma Manchester City 4-0 Swansea. Anaingia kwenye orodha ya wafungaji bora wa muda wote ndani ya City akifuatiwa na Eric Brook ambaye ana mabao 177, Tommy Johnson ana mabao 166. Anaongoza pia kwa kufunga hat trick akiwa nazo