MRITHI WA KAZE NI MAALUMU KWA AJILI YA CAF

 


SEBASTIAN Migne, raia wa Ufaransa anapewa nafasi kubwa ya kuwa mrithi wa mikoba ya Cedric Kaze ambaye alifutwa kazi Machi 7,2021 kutokana na kile kilichoelezwa kuwa hakuwa na mwendo mzuri.

Habari zinaeleza kuwa sababu kubwa za Migne kuletwa ni kwa ajili ya mashindano ya kimataifa yanayoandaliwa na Shirikisho la Soka Afrika, (Caf) ikiwa ni ile ya Kombe la Shirikisho na Ligi ya Mabingwa Afrika. 

Imani kubwa ya Yanga ni kwamba wana nafasi ya kushiriki mashindano hayo msimu ujao kwa kuwa wanaamini wapo kwenye nafasi ya kutwaa taji la Ligi Kuu Bara pamoja na lile la Shirikisho. 

Yanga ina pointi 50 baada ya kucheza mechi 23 wanaongoza ligi wakifuatiwa na mabingwa watetezi Simba wenye pointi 46 baada ya kucheza mechi 20.

Migne aliwahi kuwa Kocha Mkuu wa timu ya Taifa ya Kenya na timu ya Taifa ya Equatorial Guinea.

Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Kamati ya Ufundi Yanga, Dominic Albinius aliweka wazi kuwa mchakato unaendelea na atakayekuja ni kocha mwenye uzoefu.


Kwa sasa Yanga ipo mikononi mwa Juma Mwambusi ambaye ni Kaimu Kocha Mkuu wa timu hiyo ambayo imeweka kambi Kigamboni.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA