EYMAEL: KUIFUNGA SIMBA MBELE YA JPM NI KUMBUKUMBU KWANGU NA WACHEZAJI


 LUC Eymael, aliyekuwa Kocha Mkuu wa Yanga msimu wa 2019/20 amesema kuwa moja ya kitu ambacho anakikumbuka muda wote ni ushindi wake mbele ya Simba kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara uliochezwa Uwanja wa Mkapa.

Mchezo huo ulichezwa Uwanja wa Mkaa, Machi 8,2020 na baada ya dakika 90 ubao ulisoma Yanga 1-0 Simba.

Bao pekee ambalo alilishuhudia pia aliyekuwa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, John Pombe Magufuli lilipachikwa kimiani na Bernard Morrison na kuwafanya Simba ayeyushe pointi tatu.

Kwa sasa baada ya Magufuli kutangulia mbele za haki Machi 17,2021 Samia Suluhu ni Rais wa Jamhuri ya Muungano kwa mujibu wa katiba ambapo awali alikuwa ni makamu wa JPM. Leo Machi 30, Samia amemchagua Philip Mpango awe Makamu wa Rais wa Tanzania ambapo jina lake limepitishwa na Wabunge kwa asilimia 100.

Akizungumza na Saleh Jembe, Eymael ambaye kwa sasa yupo Ubelgiji amesema kuwa anakumbuka mchezo huo kwa namna ambavyo Magufuli aliweza kuhudhuria na timu yake ilishinda jambo ambalo halifutiki kwake.

"Nakumbuka kwamba nilipokuwa nikifundisha Yanga niliwafunga Simba mbele ya Rais JPM, alikuwa ni kiongozi shupavu na mpenda haki kwa kuwa ametangulia mbele za haki hakuna namna ninamuombea apumzike kwa amani.

"Ushindi wetu mbele yake ilikuwa ni furaha hivyo bado itabaki kuwa alama kwangu pamoja na wachezaji ambao walianza siku hiyo, na kwenye maisha yangu ya kazi Tanzania ule ni mchezo ambao nilipenda kiwango cha wachezaji wangu," .



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA