AS VITA : TUNAIFUNGA SIMBA TUKIJA TANZANIA

 


MSHAMBULIAJI wa AS Vita, Ducapel Moloko, amewapiga mkwara mzito Simba kwa kusema kuwa watachukua alama tatu watakapokutana uwanjani Jumamosi hii.

 

Kauli hiyo ameitoa zikiwa zimebaki siku chache kabla timu hizo hazijavaana kwenye mechi ya hatua ya makundi ya Ligi ya Mabingwa Afrika itakayochezwa wikiendi hii kwenye Uwanja wa Mkapa, Dar.


 Moloko amesema kuwa, wamejipanga kuchukua ushindi kwa Simba ili kutengeneza nafasi ya kufuzu hatua ya makundi.


“Sisi tumejiandaa na tutaifunga Simba ikiwa nyumbani kwao na alama zote tutazichukua, subiri tuje mtauona moto wetu,” alisema mshambuliaji huyo.

 

Katika michuano hiyo, Simba ndiyo vinara wa Kundi A wakiwa na pointi 10, wakifuatiwa na Al Ahly yenye saba, huku AS Vita ikijikusanyia pointi nne na Al Merrikh moja.


 Timu zote zimecheza mechi nne zikibakiwa na mbili kukamilisha hatua hiyo kabla ya kwenda robo fainali ambapo Simba inahitaji pointi moja ili kuweza kutinga hatua hiyo.



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA