Posts

Showing posts from January, 2021

SIMBA YAPELEKWA MAHAKAMANI NA RWEYEMAMU

Image
  ALIYEWAHI kuwa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, anaripotiwa kuishitaki timu hiyo mahakamani. Inadaiwa kuwa, Rweyemanu ambaye aliondolewa Simba mwaka jana baada ya Simba kupata matokeo mabaya mfululizo sasa inaripotiwa anataka kusafishwa na kulipwa fedha ambazo anaidai timu hiyo ili wamalizane vizuri. Mechi mbili mfululizo Simba iliyeyusha pointi sita ilikuwa kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.   Mwanasheria wake, John Feka, alikiri kuwepo kwa madai hayo ambayo yapo kwenye mahakama ya usuluhishi.   Feka amesema mteja wake ameitaka Simba kukanusha tuhuma zilizotolewa na timu ambazo zililenga kumchafua kwa makusudi.   “Kweli kesi ipo mahakama ya usuluhishi na kikubwa ipo kesi ya madai ya fedha ambazo ni siri. “Kesi nyingine ya tuhuma ambazo amepewa mteja wangu zilitaka kumchamfua kutokana na tuhuma alizopewa,” alisema wakili huyo. Chanzo:Championi

AUBA AMPASUA KICHWA ARTETA

Image
 PIERRE Emerick Aubameyang, nahodha wa kikosi cha Arsenal kwa sasa bado yupo karantini na haijulikani atarejea lini uwanjani jambo ambalo linampasua kichwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mikel Arteta. Raia huyo wa Gabon alitarajiwa kurejea uwanjani kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United uliokamilika kwa sare ya bila kufungana ila alikosekana ndani ya uwanja. Auba amewekwa karantini baada ya kutoka kumjulia hali mamaye ikiwa ni kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Corona ili kujua kwamba hajarudi na Corona. Kocha huyo amesema kuwa ni muhimu kwao kufuata utaratibu ambao umewekwa ili kutovunja sheria hivyo wataendelea kusubiri mpaka pale atakaporejea ndani ya uwanja. Arteta amesema kuwa:"Alikuwa amekwenda kumuona mamaye ila kwa sasa yupo karantini hivyo tunapaswa kufuata taratibu na hatuwezi kumtumia kwa sasa," .

JEMBE JIPYA YANGA LAPEWA JEZI YA MAPINDUZI, MAZOEZI YAKE NOMA

Image
  BAADA ya kutua Bongo Januari 29 na kupokelewa na shangwe kutoka kwa mashabiki na viongozi wa Yanga, Fiston Abdulazak Januari 30 alianza mazoezi rasmi na wachezaji wenzake kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara pamoja na Kombe la Shirikisho. Nyota huyo ambaye amesaini dili la miezi sita amesema kuwa amekuja kufanya kazi moja ya kufunga mabao jambo ambalo limewafanya Yanga wenyewe wampe jina la mtambo wa mabao. Habari kutoka kwenye benchi la ufundi ndani ya Yanga linaloongozwa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze raia wa Burundi na mzawa Nizar Khalifan limeeleza kuwa nyota huyo ameanza kuwaka mazoezini huku akipewa jezi namba 7. “Amekabidhiwa jezi namba 7 ambayo ilikuwa inatumika na Mapinduzi Balama.Balama yeye kwa sasa bado hajatengamaa kwani anaendelea na matibabu. “Alikuja na kutambulishwa kwa wachezaji na alianza mazoezi tayari na amekuwa akiwashangaza wachezaji wenzake kwa namna alivyo na uwezo katika umiliki wa mpira, na utoaji wa pasi. “Anaonekana kuwa mwepesi na ana

MO SALAH ATUPIA MAWILI WAKATI TIMU YAKE IKISEPA NA POINTI TATU MBELE YA WEST HAM UNITED

Image
 WEST Ham United walikubali kichapo cha mabao 3-1 dhidi ya Liverpool, mchezo wa Ligi Kuu England usiku wa kuamkia Januari 31. Mshambuliaji wa Liverpool, raia wa Misri Mohamed Salah alitupia mabao mawili dakika ya 57 na 68 na lile la tatu lilifungwa na Georginio Wijnaldum dakika ya 84. West Ham United walipata bao la kufuta machozi kupitia kwa Craig Dawson aliyepachika bao hilo dakika ya 87. Ushindi huo unaifanya Liverpool kupanda nafasi moja kutoka ile ya nne mpaka nafasi ya tatu baada ya kufikisha pointi 40 ikiwa imecheza jumla ya mechi 21 na West Ham United inabaki nafasi ya tano ikiwa na pointi 35 na imecheza jumla ya mechi 21.

GOMES AWAKAZIA MAZEMBE, ATAJA SABABU ZA SARE NA KUSEPA NA KOMBE

Image
 DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa wapinzani wao TP Mazembe walikuwa imara muda wote jambo ambalo limewafanya waambulie sare kwenye mchezo wao wa mwisho kwenye mchezo wa Simba Super Cup. Licha ya Gomes kuwakazia wababe hao kwenye soka la Afrika, TP Mazembe bado timu yake iliweza kuibuka vinara kwenye mashindano ya Simba Super Cup kwa kukusanya pointi nne huku TP Mazembe wakiwa nafasi ya tatu na pointi yao ni moja. Kwenye mashindano hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika kwenye bara la Afrika, Simba walianza kufungua kwa ushindi wa mabao 4-1 Januari 27 dhidi ya Al Hilal ambao wao ni washindi wa pili baada ya kuifunga mabao 2-1 TP Mazembe.  Mchezo wa jana,Januari 31 Simba ikiwa Uwanja wa Mkapa, ulikamilika kwa sare ya bila kufungana huku Simba ikikosa nafasi nyingi za wazi kupitia kwa kiungo wao Clatous Chama aliyekosa nafasi nne huku mshambuliaji Chris Mugalu akikosa nafasi mbili. Kuhusu sare hiyo Gomes amesema:"Haikuwa bahati yetu kwani tulikutana na upinzani m

KOCHA YANGA:TUTAFANYA VIZURI NDANI YA LIGI NA KOMBE LA SHIRIKISHO

Image
 EDEM Mortotsi kocha wa viungo wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anaamini kuwa timu hiyo italeta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na mashindano mengine ambayo watashiriki. Kocha huyo anaungana na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ni raia wa Burundi kuwanoa vinara wa Ligi Kuu Bara, wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 18.  Tayari kikosi hicho kimeanza mazoezi Januari 25 kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao ikiwa na ingizo jipya la wachezaji watatu kwenye dirisha dogo ambao ni Fiston Abdulazack, Saido Ntibanzokiza na Dickson Job. Mortotsi amesema:"Nimeona kwamba wachezaji wana morali na kila mmoja anapenda kufanya vizuri ndani ya uwanja hivyo ni mwanzo mzuri kwetu na wachezaji pia. "Imani yangu ni kwamba tutakuwa na mwendo mzuri na tutaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti," .

AZAM FC KUKIPIGA DHIDI YA TP MAZEMBE

Image
KLABU ya Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, George Lwandamina kesho itakuwa na kazi ya kusaka ushindi kwenye mchezo wa kirafiki dhidi ya Klabu ya TP Mazembe. Januari 30, Azam FC ilishinda mabao 3-1 dhidi ya KMC kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa Uwanja wa Azam Complex majira ya saa 10 jioni. Mabao ya Azam FC mawili yalifungwa na nyota wao Prince Dube na moja lilifungwa na Mudathiri Yahaya huku lile la KMC likifungwa na Lusajo Mwaikenda. Kesho Februari 2 Azam FC inatarajiwa kucheza mchezo wa kirafiki dhidi ya miamba ya Afrika, TP Mazembe ambao ni washindi wa tatu wa mashindano ya Simba Super Cup. Ofisa Habari wa Azam FC, Zakaria Thabit amesema kuwa malengo ya mchezo huo ni kuendelea kujiweka sawa kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara. Azam FC ikiwa nafasi ya tatu kwenye msimamo inatarajiwa kucheza Februari 7 na Simba ambao ni mabingwa wa Simba Super Cup, Uwanja wa Mkapa.

SIMBA MABINGWA WA SIMBA SUPER CUP, YAWASHUKURU MASHABIKI

Image
MTENDAJI Mkuu wa Simba, (CEO) Barbara Gonzalez amesema kuwa mashabiki wanastahili pongezi kwa kujitokeza kwa wingi kuwashuhudia mabingwa wapya wa Simba Super Cup, Simba kwenye mchezo wa kilele cha mashindano hayo ambayo umemalizika leo Januari 31, Uwanja wa Mkapa. Mashindano hayo ambayo yameshirikisha timu tatu ambazo ni Simba wenyeji, Al Hilal na TP Mazembe yalianza Januari 27 ambapo Simba walianza kwenye mchezo wa ufunguzi kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal. Al Hilal ilishinda mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe Januari 29 Uwanja wa Mkapa na kujikusanyia jumla ya pointi tatu huku Mazembe wakiwa na pointi mbili wakiwa nafasi ya tatu. Al Hilal ambao ni mabingwa wa pili pamoja na TP Mazembe wamepewa zawadi zao pamoja na medali Uwanja wa Mkapa. Pia kulikuwa na zawadi ya mchezaji bora ambayo imekwenda kwa Rarry Bwalya huku mfungaji bora akiwa ni Bernard Morrison mwenye mabao mawili. Luis Miquissone alikuwa mchezaji bora wa mchezo wa leo na kipa bora ametoka ndani ya Klabu y

FT:SIMBA SUPER CUP:SIMBA 0-0 TP MAZEMBE

Image
  FT: Simba 0-0 TP Mazembe  Simba inakuwa bingwa wa kwanza wa mashindano ya Simba Super Cup ambayo yalianza Januari 27, Uwanja wa Mkapa baada ya kulazimisha sare ya bila kufungana mbele ya TP Mazembe, Uwanja wa Mkapa. Inakusanya jumla ya pointi nne baada ya kushinda mbele ya Al Hilal mabao 4-1 na Al Hilal ni washindi wa pili baada ya kushinda mabao 2-1 mbele ya TP Mazembe ambao ni washindi wa tatu. Zinaongezwa dakika 2 Dakika ya 90 Chikwende anapeleka mashambulizi TP Mazembe ila mwamuzi anasema amenawa Dakika ya 88 Onyango anatolewa akiwa Kwenye machela baada ya kuchezewa faulo Dakika ya 85 Ajibu anachukua nafasi ya Chama na Mzamiru anachukua nafasi ya Lwanga Dakika ya 84 Mwapi anaonyeshwa kadi ya njano  Dakika ya 81 Duchu anaonyeshwa kadi ya njano Dakika ya 61 Chama anapaisha Dakika ya 60 Wawa anajichanganya Kwenye kuokoa Jeje anakosa nafasi ya wazi Dakika ya 57 Morrison anaingia anatoka Sheva Dakika ya 53 Chama anapiga of target akiwa nje kidogo ya lango Dakika ya 50

KIKOSI CHA TP MAZEMBE KITAKACHOANZA LEO DHIDI YA SIMBA, UWANJA WA MKAPA

Image
 KIKOSI cha TP Mazembe kitakachoanza leo dhidi ya Simba, Uwanja wa Mkapa, Simba Super Cup. Mounkoro Ibrahim Tandi Mwape Arsene Zola Kabaso Chongo Josep Ochanya Chris Kisangala Christian Koume Fred Djedeje Isaac Tshibangu Rainford Kalaba Moustapha Kouyate

YANGA WATAMBIA BENCHI LAO LA UFUNDI, YATAJA MAKOMBE INAYOHITAJI

Image
 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa benchi lao la ufundi lipo imara jambo ambalo wanaamini kwamba litawapa matokeo mazuri kwenye mechi zao za Ligi Kuu Bara pamoja na mashindano mengine. Tayari kikosi hicho kinachonolewa na Kocha Mkuu, Cedric Kaze kinaongoza ligi kikiwa nafasi ya kwanza na pointi zake kibindoni ni 44. Kimecheza jumla ya mechi 18 na hakijapoteza mchezo hata mmoja zaidi ya kushinda mechi 13 na kulazimisha sare tano ndani ya uwanja. Ofisa Uhamasishaji wa Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa wamejipanga kwa ajili ya kufanya vizuri kwenye mechi zao zote za ligi kutokana na benchi lao imara. "Tuna benchi makini la ufundi ambalo lina vijana watupu mpaka wachezaji pia asilimia kubwa ni vijana hivyo imani yetu ni kuona kwamba tunafanya vizuri. "Kikubwa ambacho kipo kwenye mpango wetu ni kupata matokeo tunahitaji kutwaa Kombe la Ligi Kuu Bara, tunahitaji Kombe la Shirisho hilo lipo wazi ni suala la muda tu," . Mikoba ya kocha msaidizi ambayo ilikuwa mikononi mwa Ju

DStv CHUPUCHUPU WALE KICHAPO KWA GLOBAL FC

Image
  UNAWEZA ukasema watasimulia waendako, mara baada ya kikosi bora na ghali cha Kampuni ya Global Group, Global FC  kuupiga mwingi dhidi ya timu ya Kampuni ya Multichoice, DStv ambao waliponea chupuchupu kula kichapo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa leo Jumapili Januari 31, 2021 Uwanja wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam (UDSM).   Mchezo huo umekamilika kwa sare ya kufungana mabao 3-3 huku DStv wakifanya kazi ya kusawazisha mabao hayo. Global FC walikuwa wa kwanza kuandika bao la uongozi kwa mpira wa kutengwa uliopigwa na nyota wa timu hiyo Saleh Ally ‘Jembe’ na kuzamishwa kimiani na mshambuliaji Abdulghafary Ally. Hadi mapumziko Global FC walitoka na mtaji wa mabao 2-1. DStv wao walipata mabao mengine mawili ya harakaharaka na kupata uongozi wa 3-2 kisha Abdulghafary akasawazisha kwa upande wa Global na kuwa 3-3 hadi dakika 90. Baada ya matokeo hayo ya sare kituko ni kwamba refa aliamua zipigwe penalti ili mshindi apatikane lakini DStv wakakataa kabisa.   Baada ya mchezo zi

MASHABIKI WA SIMBA V TP MAZEMBE WAPEWA TIKETI BURE NA SPOTI XTRA

Image
  TIMU ya Masoko kutoka Kampuni ya Global Group kambao ni wachapishaji wa magazeti namba moja kwa habari za michezo kupitia gazeti la Spoti Xtra imeingia mtaani leo Januari 31 kutoa zawadi kwa wateja wake. Ziara ya leo ilikuwa ni maeneo ya Uwanja wa Benjamin Mkapa Jijini Dar es salaam ambapo kuna tukio la mchezo wa kukata na shoka kati ya Simba dhidi ya TP Mazembe. Unatarajiwa kuchezwa mchezo wa mwisho kilele cha mashindano ya Simba Super Cup, ambap wenyeji Simba watamenyana na TP Mazembe. Mashabiki wa Simba na TP Mazembe wamepata bahati ya kupewa tiketi bure baada ya kupata nakala ya gazeti bora siku ya Jumapili la Spoti Xtra. Anthon Adam, Mkuu wa Kitengo cha Usambazaji kutoka Global Publishers amesema kuwa ni kawaida ya kampuni hiyo kurudisha fadhila kwa wasomaji wake ikiwa ni pamoja na kuwapa zawadi mbalimbali. “Hii imekuwa desturi yetu kurudisha fadhila kwa wasomaji wetu kwani wamekuwa wakituunga mkono, hivyo ni jambo jema kuwarudishia kile tunachokipata kutoka kwao, kwa k

KANE MAJANGA TUPU, HATIHATI KUUKOSA MCHEZO WA KUFUZU KOMBE LA DUNIA

Image
 HARRY Kane, mshambuliaji wa kikosi cha Tottenham imeelezwa kuwa anaweza kukaa nje ya uwanja kwa muda mrefu tofauti na ilivyoelezwa awali. Kane aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool uliochezwa Alhamisi iliyopita ambapo timu yake ilifungwa mabao 3-1. Taarifa zimekuwa zikisema kuwa mchezaji huyo anaweza kukosa mchezo wa timu ya Taifa ya England wa kufuzu Kombe la Dunia unaotarajiwa kuchezwa Machi mwaka huu 2021. Kocha Mkuu wa Tottenham, Jose Mourinho amesema kuwa ni kweli mchezaji wake ameumia ila muda ambao atakaa nje ya uwanja bado hajatambua. "Kweli Kane ameumia ila kuhusu majeraha yake na muda ambao atakosekana ni jambo ambalo linahitaji muda hivyo tusubiri na tuone," .

LUKAKU NA ZLATAN YAWAKUTA, WAPIGWA PINI ITALIA

Image
 KAMATI ya nidhamu ya Ligi Kuu ya Italia imewafungia mastaa wawili kwenye ligi hiyo, Zlatan Ibrahimovic wa AC Milan na Romelu Lukaku wa Inter Milan. Hatua hiyo imefikia baada ya mastaa hao kukorofishana kwenye mchezo wa robo fainali ya Copa Italia, Jumanne ya wiki hii wakati Inter Milan ikishinda mabao 2-1. Chama cha soka cha Italia kimewafungia wachezaji hao ambao walitaka kukinukisha ndani ya uwanja mara mbili kwenye mchezo wa michuano hiyo. Pia adhabu hiyo ni tofauti na ile ambayo Zlatan alipewa uwanjani baada ya kuonyeshwa kadi nyekundu kwa kuwa alionyeshwa jumla ya kadi mbili za njano. Lukaku ambaye alionyeshwa kadi ya njano ataukosa mchezo wa nusu fainali ya kwanza dhidi ya Juventus huku chama hicho kikiweka wazi kwamba bado hakijapitia taarifa ya mwamuzi na kama kutakuwa na makosa mengine basi adhabu hiyo inaweza kuongezeka. 

MORRISON AWEKA REKODI TATU KWA MKAPA KAMA NAMBA YA JEZI

YANGA WAZUNGUMZIA HALI ZA YACOUBA NA NTIBANZOKIZA

Image
  UONGOZI wa Yanga umesema kuwa kwa sasa maendeleo ya nyota wao watatu ambao ni majeruhi ndani ya kikosi hicho ambao ni Saido Ntibanzokiza, Yacouba Songne na Dickson Job yanaleta matumaini hivyo mashabiki wasiwe na presha. Saido ambaye ni kiungo mshambuliaji aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu Bara dhidi ya Tanzania Prisons huku Yacouba alipata maumivu kwenye mchezo wa Kombe la Mapinduzi hatua ya robo fainali dhidi ya Azam FC na Job yeye alipata maumivu ya paja akiwa kwenye kambi ya timu ya Taifa ya Tanzania.  Meneja wa Yanga, Hafidh Saleh alisema kuwa kwa sasa wachezaji wanaendelea na mazoezi huku wale wanaosumbuliwa na majeraha wakiwa na maendeleo mazuri. “Kuhusu Job huyu tayari ameanza mazoezi mepesi na wachezaji wenzake ambao wapo kambini hivyo tupo imara na nina amini kwamba mpaka ligi itakaporudi kila kitu kitakuwa sawa. “Yacouba na Saido nao pia bado hawajawa fiti ila nao maendeleo yao ni mazuri hivyo mashabiki wasiwe na mashaka kuhusu wachezaji hawa,” alisema Saleh.

ISHU YA MKUDE KUREJEA SIMBA IMEKAA NAMNA HII

Image
 JONAS Mkude, nyota wa Klabu ya Simba kwa sasa anasubiri simu ya Mtendaji Mkuu wa Simba, Barbara Gonzalez ili aweze kurejea kambini. Kiungo huyo mkabaji kipenzi cha mashabiki na viongozi wa Simba alisimamishwa ndani ya Klabu hiyo Desemba 28 kutokana na utovu wa nidhamu. Kwa mujibu wa Kamati ya Nidhamu ya Simba inayosimamiwa na Kamanda Mstaafu wa Kanda ya Dar, Seleman Kova iliweka wazi kuwa nyota huyo alikutwa na hatia ya makosa ya utovu wa nidhamu. Kutokana na suala hilo alipigwa faini ya milioni moja na kupewa karipio kali pamoja na kutakiwa kuomba msamaha kwa njia ya maandishi ikiwa tayari ameshaomba msamaha kwa njia ya maneno. Habari zinaeleza kuwa tayari ameshakamilisha kila kitu ikiwa ni pamoja na faini hivyo kwa sasa anasubiri ruhusu kutoka kwa CEO. "Tayari Mkude amemaliza kila kitu kuanzia faini mpaka kuomba msamaha kwa maandishi, ni suala la simu ya CEO kwamba kijana rudi kazini anarudi kambini," ilieleza taarifa hiyo. Chini ya Kocha Mkuu, Didier Gomes Mkude b

MTIBWA SUGAR YAANZA KUPIGIA HESABU MZUNGUKO WA PILI

Image
 HITIMANA Thiery, Kocha Mkuu wa Mtibwa Sugar amesema kuwa tayari wachezaji wa timu hiyo wamerudi kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi za Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili. Mtibwa Sugar walivunja kambi baada ya kuvuliwa ubingwa wa Kombe la Mapinduzi na Simba visiwani Zanzibar. Akizungumza na Saleh Jembe, Hitimana ambaye aliibuka ndani ya Mtibwa Sugar baada ya kufutwa kazi ndani ya Klabu ya Namungo FC amesema kuwa tayari maandalizi yameanza. "Taratibu kwa sasa tumeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zetu za Ligi Kuu Bara mzunguko wa pili na nina amini kwamba tutakuwa imara. "Ipo wazi kwamba mzunguko wa pili utakuwa na ushindani mkubwa ila mashabiki wasiwe na presha wazidi kutupa sapoti nina amini kwamba tutafanya vizuri na kila kitu kitakuwa sawa," . Kwenye msimamo wa Ligi Kuu Bara, Mtibwa Sugar ipo nafasi ya 11 baada ya kucheza jumla ya mechi 18 na kibindoni ina pointi 22.

MWISHO WA UBISHI GLOBAL FC V DStv LEO

Image
  MWISHO wa ubishi ni leo kwa mchezo wa kirafiki kati ya Global FC dhidi ya timu ya DStv mchezo unaotarajiwa kupigwa kwenye Viwanja vya Chuo Kikuu cha Dar es Salaam. Mchezo huo ambao ni maalum kwa ajili ya kudumisha uhusiano na ujamaa kati ya Kampuni ya Multichoice na Global Group ambazo zimekuwa zikishirikiana kwenye mambo mbalimbali unatarajiwa kuwa na upinzani wa aina yake kutokana na maandalizi ya timu zote mbili.   Akizungumza na Saleh Jembe, Kocha Mkuu wa Global FC, Philip Nkini amesema kuwa kikosi chake kimekamilika na wanaamini wataibuka na ushindi ndani ya dakika 90.   “ DStv waje kwa nidhamu tumefanya maandalizi kwa muda mrefu na itakuwa ni mechi yetu ya kwanza kwa ufunguzi ndani ya 2021 hivyo tutafanya jambo la kweli, mashabiki wajitokeze kwa wingi.  Nahodha wa DStv, Festo Laizer amesema: “Mpira hauchezwi mdomoni ni ndani ya uwanja,tutafanya kweli na hakuna ambacho kinashindikana tutawafunga na hawataamini,”.  

AZAM FC YAINYOOSHA KMC 3-1 AZAM COMPLEX

Image
  VIVIER Bahati,  kocha msaidizi wa Klabu ya Azam FC amesema kuwa bado vijana wake wanazidi kuimarika jambo ambalo limewafanya waibuke na ushindi wa mabao 3-1 dhidi ya KMC. Azam FC iliibuka na ushindi huo kwenye mchezo wa kirafiki uliochezwa jana Januari 29, Uwanja wa Azam Complex.  Mabao ya Azam FC mawili yalifungwa na Prince Dube na moja lilipachikwa na Mudhathir Yahya huku lile la KMC likipachikwa na Lusajo Mwaikenda aliyepachika bao hilo kwa penalti. Bahati amesema:"Ulikuwa ni mchezo mzuri na kila mchezaji alikuwa kwenye wakati mzuri jambo ambalo limetufanya tuwe katika wakati mzuri kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara ambazo zinakuja,". Ligi Kuu Bara inatarajiwa kurejea Februari 13 huku Azam FC ikiwa na kibarua cha kuanza kumaliza kiporo cha mchezo wake dhidi ya Simba. Mchezo huo wa mzunguko wa kwanza unatarajiwa kuchezwa Februari 7, Uwanja wa Mkapa.

RASHFORD:NINAJUA KWAMBA MIMI NI MWEUSI, WANAONIBAGUA SITAWAJIBU

Image
MARCUS Rashford, mshambuliaji wa Klabu ya Manchester United amesema kuwa anatambua kwamba ana rangi nyeusi anaifurahia rangi hiyo wale wanaombagua hawatendi jambo la haki na wala wasifikiri kwamba atawajibu. Nyota huyo wa Manchester United alikutana na jambo hilo kupitia mitandao ya kijamii muda mfupi baada ya timu yake kulazimisha sare ya bila kufungana dhidi ya Klabu ya Arsenal, Uwanja wa Emirates kwenye mchezo wa Ligi Kuu England. Kupitia kwenye mtandao wa kijamii wa Instagram mashabiki walianza kumshambulia Rashford kwa kutumia emoji za nyani na wengine waliweka ujumbe kwamba anapaswa kwenda maeneo ya makazi ya wanyama jambo ambalo limemuumiza nyota huyo kuhusu ubaguzi wa rangi. Mbali na Rashford mwenye miaka 23 pia suala hilo la ubaguzi wa rangi lilimtokea nyota mwenzake Axel Tuanzebe na Anthony Martial pia nyota wa Chelsea Reece James na nyota wa Klabu ya West Broms Romaine Sawyer nao pia walikutana na ubaguzi kwenye mitandao ya kijamii. Rashford kupitia tweet amesema:"

KUMBE SVEN ALIBWAGA MANYANGA KIMYAKIMYA, SIMBA HAWAKUTAKA KUACHANA NAYE

Image
UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa haukuwa na mpango wa kuachana na Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba na alibwaga manyanga Januari 7. Aliyekuwa Mtendaji Mkuu ndani ya Klabu ya Simba, Crestius Magori amesema kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba alipigiwa simu na watu kutoka sehemu aliyokuwa anakaa Sven na kuambiwa kuwa amebeba kila kitu mpaka viatu. "Hatukuwa na mpango wa kuachana na Sven ila yeye mwenyewe aliamua kuondoka na CEO aliambiwa kuwa mbona Kocha amebeba kila kitu kutoka kwa watu wa sehemu aliyokuwa anakaa, wakati huo timu ilikuwa wanajiaandaa kwenda Zanzibar, ". Sven kwa sasa yupo ndani ya Klabu ya FAR Rabat ya Morroco.

MUONEKANO WA UKURASA WA MBELE GAZETI LA SPOTI XTRA JUMAPILI

Image
  MUONEKANO wa ukurasa wa mbele Gazeti la SPOTI XTRA Jumapili 

SIMBA KUBADILI KIKOSI MBELE YA TP MAZEMBE AMBAO WATABADILI MFUMO KESHO

Image
 KUELEKEA kwenye mchezo wa kilele cha mashindano ya Simba Super Cup, kesho Januari 31, Uwanja wa Mkapa Kocha Mkuu wa Klabu ya Simba, Didier Gomes amesema kuwa atafanya mabadiliko makubwa kwenye kikosi cha kwanza. Gomes alianza kwa ushindi wa mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal Uwanja wa Mkapa, Januari 27 na kesho ana kibarua cha kusaka ushindi mbele ya TP Mazembe. TP Mazembe wanaingia uwanjani wakiwa na hasira ya kupoteza kwa kufungwa mabao 2-1 dhidi ya Al Hilal hivyo kesho utakuwa ni mchezo wa kisasi kwa TP Mazembe ambayo Mtanzania Thomas Ulimwengu anacheza. Raia huyo wa Ufaransa ambaye amerithi mikoba ya Sven Vandenbroeck ambaye amebwaga manyanga Januari 7 na kwa sasa yupo zake ndani ya FAR Rabat ya Morocco amesema kuwa anataka kuwaona wachezaji wake wote wakiwa ndani ya uwanja. "Kuelekea kwenye mchezo wetu dhidi ya TP Mazembe ninahitaji kufanya mabadiliko kwenye kikosi cha kwanza ili kuweza kuwaona wachezaji wote wakiwa ndani ya uwanja. "Kutakuwa na mabadiliko ya kikosi kwe

JKT TANZANIA KUCHEZA MECHI TATU ZA KIRAFIKI

Image
KOCHA Mkuu wa Klabu ya JKT Tanzania Abdalah Mohamed,'Bares' amesema kuwa kwa sasa kikosi hicho kinaendelea na maandalizi kwa ajili ya mechi za Ligi Kuu Bara na wanatarajia kuwa na mechi tatu za kirafiki kujiweka sawa. JKT Tanzania kwenye msimamo ipo nafasi ya 12 ikiwa imekusanya jumla ya pointi 20 baada ya kucheza jumla ya mechi 18. Akizungumza na Saleh Jembe, Bares amesema kuwa wapo vizuri kwa ajili ya mzunguko wa pili na wanaamini kwamba ushindani utakuwa mkubwa ndani ya uwanja. "Tunatajia kucheza mechi tatu za kirafiki ambazo zitaweza kutupa matokeo mazuri ndani ya uwanja na kwa kuanza ninadhani tutaanza na Mtibwa Sugar kisha nyingine mbili zitafuata. "Wachezaji wapo vizuri na kila mmoja yupo tayari kwa ajili ya mechi zetu zijazo ndani ya Ligi Kuu Bara nina amini kwamba kila kitu kitakwenda sawa.Tukimaliza mechi zetu za kirafiki nina amini tutakuwa na kitu ambacho tumekijenga," . Kwa sasa JKT Tanzania inaendelea na mazoezi bila ya nyota wake Adam Ad

MASAU BWIRE:NIOMBEENI,NIMEAMBIWA NIMEKULA CHAKULA CHENYE SUMU

Image
  OFISA Habari wa Ruvu Shooting inayoshiriki Ligi Kuu Bara amewaomba Watanzania wamuombee kwa kuwa kwa sasa hali yake haijatengamaa kwa kile ambacho ameambiwa na madaktari kuwa amekuwa chakula chenye sumu. Kupitia ukurasa wake wa Istagram Masau Bwire ameandika:Kwa siku kadhaa zilizopita, nimekuwa sipokei simu, au nikipokea nasema tu siko vizuri, siwezi kuzungumza! Wapo walionielewa, lakini wapo walioona kama ni jeuri na kiburi tu, nafanya makusudi, kwa sababu sitaki kuzungumza nao. Niwaombe radhi, wanisamehe kwa yote, lakini pia niwaaambie, na kuwahakikishia kwamba, sina kawaida hiyo ya kutopokea simu ya mtu yeyote atakayenipigia, siwezi kudharau simu ya mtu yeyote, daima namuomba Mungu, aniepushe na tabia hiyo ya kishetani ya kudharau na kutowapa ushirikiano pale wanapohitaji lolote kutoka kwangu. Kwa kweli nilikuwa katika hali ngumu, kama unavyoiona hiyo picha, ndio uhalisia wa namna nilivyokuwa, nilikamatika haswa! Baada ya vipimo vya Hospitali, wataalamu wa afya (Daktari),

KMC YAIPIGA MKWARA AZAM FC, YATAMBA KUITEMBEZEA PIRA SPANA

Image
CHRISTINA Mwagala, Ofisa Habari wa Klabu ya KMC amesema kuwa wapo tayari kwa ajili ya kuzilamba Ice Cream za wapinzani wao Azam FC kwenye mchezo wa kirafiki utakaochezwa Uwanja wa Azam Complex, saa 4:30 jioni leo Januari 30. Azam FC inayonolewa na Kocha Mkuu, Geroge Lwandamina itawakaribisha Wanakino Boys kwenye mchezo wa kirafiki ambao ni maalumu kwa ajili ya kujiweka sawa kwa ajili ya mzunguko wa pili. Christina amesema kuwa wamejipanga kwa ukamilifu kwenye mchezo wa leo kupata matokeo licha ya kwamba ni mchezo wa kirafiki. "Tupo tayari kwa ajili ya mchezo wetu dhidi ya Azam FC, tunahitaji kulamba Ice Cream na kuonyesha kwamba sisi tunaweza na tupo imara. "Mbali na kwamba ni mchezo wa kirafiki vijana wetu wapo imara na wataonyesha kwamba ile mwendo wa pira spana, pira kodi inaendelea ndani ya uwanja. "Utakuwa ni mchezo maalumu kwa ajili ya kuweza kurejea kwenye ubora wetu pale ligi itakapoanza hasa ukizingatia kwamba tunarudi kwenye ligi na tutaanza na mche

KOCHA AZAM AIPIGA HESABU ZA KUIMALIZA SIMBA

BIASHARA UNITED KAMILI GADO KWA MZUNGUKO WA PILI

Image
  UONGOZI wa Biashara United umesema kuwa kwa sasa unaendelea na mazoezi kwa ajili ya kujiweka sawa kwa timu hiyo kabla ya mechi za Ligi Kuu Bara kurejea. Timu hiyo inayonolewa na Kocha Mkuu, Francis Baraza ipo nafasi ya nne kwenye msimamo ikiwa imekusanya jumla ya pointi 29 kibindoni. Imecheza jumla ya mechi 18 huku ikishinda mechi 8,sare 5 na imepoteza jumla ya mechi 5 kwa msimu huu wa 2020/21. Akizungumza na Saleh Jembe, Ofisa Habari wa Biashara United, Idrisa Sechombo amesema kuwa mapumziko ambayo waliwapa wachezaji yamekwisha hivyo kwa sasa wameanza maandalizi ya ligi. "Tuliwapa mapumziko wachezaji wetu ila kwa sasa muda huo tayari umekwisha hivyo tumeanza maandalizi kwa ajili ya mechi zetu za ligi. "Kila kitu kipo sawa na wachezaji wameanza kuripoti kambini kwa ajili ya maandalizi ya mechi zetu. Awali tulipanga kucheza mchezo wa kirafiki na Alliance ila mchezo huo umefutwa," amesema.  

MABOSI YANGA WATAJA KAZI YA MTAMBO WA MABAO

Image
 UONGOZI wa Yanga umesema kuwa nyota wao mpya Fiston Abdulazack ambaye wamempachika jina la mtambo wa mabao amekuja kufanya kazi itakayowapa furaha wana Jangwani. Nyota huyo ametua Bongo jana, Januari 29 akitokea nchini Burundi na amesaini dili la miezi sita ambalo lina kipengele cha kuongeza mkataba. Anaungana na rafikiye, Said Ntibanzokiza ambaye alianza kazi ndani ya Yanga akiwa amefunga mabao mawili kwenye Ligi Kuu Bara. Ntibanzokiza na rai wa Burundi na alijiunga na Yanga kwenye usajili wa dirisha dogo akiwa ni mchezaji huru na alikuwa anakipiga kwenye timu ya Taifa ya Burundi. Alianza kufunga bao lake la kwanza mbele ya Dodoma Jij, Uwanja wa Sheikh Amri Abeid na alifunga bao la pili mbele ya Tanzania Prisons, Uwanja wa Nelson Mandela. Ofisa Uhamasishaji ndani ya kikosi cha Yanga, Antonio Nugaz amesema kuwa kazi yake ni kuwapa furaha wanajangwani na kutuma salamu kwa wapinzani wao. "Amekuja ndani ya Yanga kufanya kazi ya kuwapa furaha mashabiki wa Yanga ambao kwa sasa

LIVERPOOL YATAJWA KUMALIZANA NA BEKI LONG

Image
IMERIPOTIWA kuwa Klabu ya Liverpool ambao ni mabingwa watetezi wa Ligi Kuu England imemalizana na beki wa kati wa Klabu ya New York Red Bulls, Aaron Long. Hatua hiyo imefikia baada ya Liverpool kutokuwa imara upande wa ulinzi kutokana na mabeki wake wengi kuwa ni majeruhi ikiwa ni pamoja na Virgil van Dijk ambaye ni beki kisiki wa kati na Joe Gomez hawa wanatarajiwa kukaa nje msimu mzima wakitibu majeraha yao. Pia Joel Matip aliumia kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Tottenham hivyo naye anasumbuliwa na majeraha jambo ambalo linawafanya Liverpool wasiwe na chaguo zaidi ya kuhitaji saini ya beki huyo mwenye miaka 28 kwa mkopo. Jurgen Klopp, Kocha Mkuu wa Liverpool amesema kuwa watafanya jitihada ili kuweza kuwa imara katika safu ya ushambuliaji pamoja na ulinzi ambavyo vyote vinategemeana ndani ya uwanja. "Kila kitu ndani ya uwanja kinategemeana, ninaskia kwamba wanasema nisajili beki wa kati sasa hapo unaweza kujiuliza nikipata beki nitakuwa nimemaliza matatizo yote

UCHAGUZI RT KINAWAKA LEO

DUBE: KWA BEKI HUYU, SIMBA WAMEPATA JEMBE

BUMBULI HAJARIDHIKA NA MAAMUZI YA KUFUNGIWA,SIMBA WATOA NENO

Image
BAADA ya kufungiwa miaka mitatu kujihusisha na shughuli za mpira wa miguu ndani na nje ya nchi na Kamati ya Maadili ya Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Ofisa Habari wa Klabu ya Yanga, Hassan Bumbuli amesema kuwa hajaridhishwa na hukumu hiyo hivyo atawakilisha rufaa yake.   Kamati hiyo ilimpa adhabu hiyo Bumbuli  baada ya kushindwa kulipa kiasi cha Sh. 5,000,000 kama ilivyoainishwa kwenye hukumu yao iliyotolewa tarehe 28 Septemba 2020,  baada ya kiongozi huyo kukutwa na hatia.   Taarifa ya kamati hiyo ya maadili iliyotolewa, 27 Januari 2021, imeeleza kuwa adhabu ya kumfungia kiongozi huyo kwa kipindi cha miaka mitatu imetolewa chini ya cha 73(8)(a) cha mwongozo wa maadili ya TFF, toleo la 2013.   Akizungumza baada ya adhabu hiyo Bumbuli amesema kuwa hukumu hiyo imeshatoka na wameipokea ila kwa upande wake bado hakuridhika na maamuzi hayo na atakata rufaa.   “Nyundo imeshuka na tumeshaipokea na tutaijadili na uongozi wa Yanga tujue tunafanyaje, na kiufupi hatukurid

BINGWA SIMBA SUPER CUP KUSEPA NA M 15,KESHO NI SIMBA V TP MAZEMBE

Image
 UONGOZI wa  Simba umeweka wazi kuwa zawadi atakazopata bingwa wa michuano ya Simba Super Cup iliyoanza Januari 27, 2021 ni fedha taslimu shilingi milioni 15, kikombe na medali.   Ofisa Habari wa Simba, Haji Manara amesema kuwa wamepanga kutoa zawadi hiyo pamoja na kutoa burudani kwa mashabiki ambao watajitokeza kutazama mashindano hayo ambayo ni mara ya kwanza kufanyika ndani ya ardhi ya Bongo. Katika mashindano hayo ni timu tatu ambazo zinashiriki ikiwa ni Simba wenyewe ambao ni wenyeji, Al Hilal ya Sudan na TP Mazembe ya Congo. Simba ilianza mchezo wa ufunguzi Januari 27 na ilishinda mabao 4-1 dhidi ya Al Hilal na mchezo wa pili ulikuwa ni jana, Januari 29 ambapo Al Hilal ilishinda mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe. Kilele ni kesho Januari 31 ambapo Simba itacheza na TP Mazembe na mshindi atapatikana kesho, Uwanja wa Mkapa. Manara amesema baada ya mchezo wa mwisho kutakuwa na tafrija  (after party)  ambayo itafanyika ‘Kidimbwi Beach’ jijini Dar es Salaam. Na siku hiyo kutak

JOSE MOURINHO:KUKASIRIKA KWA WACHEZAJI KAWAIDA WAKIFUNGWA

Image
JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham amesema kuwa kitendo cha wachezaji wake kukasirika ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo ni jambo la kawaida kutokea hasa pale ambapo timu inakuwa imefungwa. Januari 28, Mourinho alikiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool na kukubali kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1. Habari zimeeleza kuwa wakati wa mapumziko wachezaji walikuwa wakilaumiana huku zigo kubwa la lawama akipewa beki Serge Aurier kwa kuwa alishindwa kuongeza uimara kwenye safu ya ulinzi dakika za mwisho kabla ya mapumziko na kuruhusu Liverpool kupata bao la kuongoza. Roberto Firmino alifunga bao hilo la kwanza kwa Liverpool akiwa chini ya uangalizi wa Aurier na Eric Dier ambao walikuwa kwenye safu ya ulinzi. Mourinho aliamua kumfanyia mabadiliko Aurier ambaye alikasirika na anatajwa kusepa uwanjani wakati wachezaji wenzanke wakiingia kumalizia dakika 45 za kipindi cha pili na waliokota nyavuni mabao mengine mawili. Pia inaelezwa kuwa nyot

AL HILAL YAIBAMIZA MABAO 2-1 TP MAZEMBE, SIMBA SUPER CUP

Image
 KLABU ya Al Hilal leo Januari 29 imeibuka na ushindi wa mabao 2-1 dhidi ya TP Mazembe kwenye mchezo wa Simba Super Cup uliochezwa Uwanja wa Mkapa. TP Mazembe anayocheza Mtanzania, Thomas Ulimwengu ilianza kupachika bao kupitia kwa nyota wao Moustapha Kouyate dakika ya 11. Kwa Al Hilal, dakika ya 29 Bongonga Vinny aliweka mzani sawa na kufanya ngoma kuwa 1-1 baada ya kupachika bao ambalo liliwarudisha wapinzani wao TP Mazembe katikati ya uwanja. Mpaka wanakwenda mapumziko timu zote mbili zilikuwa zimetoshana nguvu ndani ya dakika 45, kwenye mashindano ya Simba Super Cup. Mashabiki ambao walijitokeza Uwanja wa Mkapa walikuwa wachache kiasi chake na walishuhudia ushindani mkubwa ndani ya uwanja. Kipindi cha pili wachezaji wa Al Hilal waliweza kukosa umakini dakika za mwanzo kupachika bao la pili huku TP Mazembe wenyewe pia wakikosa umakini kupachika bao la pili. Ikiwa imebaki dakika moja mpira kukamilika, Al Hilal waliweza kupachika bao la pili dakika ya 89 kupitia kwa Mohamed Mu