SIMBA YAPELEKWA MAHAKAMANI NA RWEYEMAMU


 ALIYEWAHI kuwa Meneja wa Simba, Patrick Rweyemamu, anaripotiwa kuishitaki timu hiyo mahakamani.

Inadaiwa kuwa, Rweyemanu ambaye aliondolewa Simba mwaka jana baada ya Simba kupata matokeo mabaya mfululizo sasa inaripotiwa anataka kusafishwa na kulipwa fedha ambazo anaidai timu hiyo ili wamalizane vizuri.

Mechi mbili mfululizo Simba iliyeyusha pointi sita ilikuwa kwa kukubali kichapo cha bao 1-0 dhidi ya Tanzania Prisons na bao 1-0 dhidi ya Ruvu Shooting.

 

Mwanasheria wake, John Feka, alikiri kuwepo kwa madai hayo ambayo yapo kwenye mahakama ya usuluhishi.

 

Feka amesema mteja wake ameitaka Simba kukanusha tuhuma zilizotolewa na timu ambazo zililenga kumchafua kwa makusudi.


 

“Kweli kesi ipo mahakama ya usuluhishi na kikubwa ipo kesi ya madai ya fedha ambazo ni siri.


“Kesi nyingine ya tuhuma ambazo amepewa mteja wangu zilitaka kumchamfua kutokana na tuhuma alizopewa,” alisema wakili huyo.


Chanzo:Championi



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO