AUBA AMPASUA KICHWA ARTETA


 PIERRE Emerick Aubameyang, nahodha wa kikosi cha Arsenal kwa sasa bado yupo karantini na haijulikani atarejea lini uwanjani jambo ambalo linampasua kichwa Kocha Mkuu wa kikosi hicho, Mikel Arteta.

Raia huyo wa Gabon alitarajiwa kurejea uwanjani kwenye mchezo wao wa Ligi Kuu England dhidi ya Manchester United uliokamilika kwa sare ya bila kufungana ila alikosekana ndani ya uwanja.

Auba amewekwa karantini baada ya kutoka kumjulia hali mamaye ikiwa ni kuchukua tahadhari dhidi ya janga la Corona ili kujua kwamba hajarudi na Corona.

Kocha huyo amesema kuwa ni muhimu kwao kufuata utaratibu ambao umewekwa ili kutovunja sheria hivyo wataendelea kusubiri mpaka pale atakaporejea ndani ya uwanja.

Arteta amesema kuwa:"Alikuwa amekwenda kumuona mamaye ila kwa sasa yupo karantini hivyo tunapaswa kufuata taratibu na hatuwezi kumtumia kwa sasa," .



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO