KOCHA YANGA:TUTAFANYA VIZURI NDANI YA LIGI NA KOMBE LA SHIRIKISHO


 EDEM Mortotsi kocha wa viungo wa Klabu ya Yanga amesema kuwa anaamini kuwa timu hiyo italeta ushindani ndani ya Ligi Kuu Bara, Kombe la Shirikisho pamoja na mashindano mengine ambayo watashiriki.

Kocha huyo anaungana na Kocha Mkuu, Cedric Kaze ambaye ni raia wa Burundi kuwanoa vinara wa Ligi Kuu Bara, wakiwa na pointi 44 baada ya kucheza mechi 18.

 Tayari kikosi hicho kimeanza mazoezi Januari 25 kwa ajili ya maandalizi ya mechi zao ikiwa na ingizo jipya la wachezaji watatu kwenye dirisha dogo ambao ni Fiston Abdulazack, Saido Ntibanzokiza na Dickson Job.

Mortotsi amesema:"Nimeona kwamba wachezaji wana morali na kila mmoja anapenda kufanya vizuri ndani ya uwanja hivyo ni mwanzo mzuri kwetu na wachezaji pia.

"Imani yangu ni kwamba tutakuwa na mwendo mzuri na tutaweza kufikia malengo ambayo tumejiwekea hivyo mashabiki wazidi kutupa sapoti," .





Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO