KUMBE SVEN ALIBWAGA MANYANGA KIMYAKIMYA, SIMBA HAWAKUTAKA KUACHANA NAYE




UONGOZI wa Klabu ya Simba umesema kuwa haukuwa na mpango wa kuachana na Sven Vandenbroeck ambaye alikuwa Kocha Mkuu wa Simba na alibwaga manyanga Januari 7.


Aliyekuwa Mtendaji Mkuu ndani ya Klabu ya Simba, Crestius Magori amesema kuwa Mtendaji Mkuu wa Simba alipigiwa simu na watu kutoka sehemu aliyokuwa anakaa Sven na kuambiwa kuwa amebeba kila kitu mpaka viatu.


"Hatukuwa na mpango wa kuachana na Sven ila yeye mwenyewe aliamua kuondoka na CEO aliambiwa kuwa mbona Kocha amebeba kila kitu kutoka kwa watu wa sehemu aliyokuwa anakaa, wakati huo timu ilikuwa wanajiaandaa kwenda Zanzibar, ".


Sven kwa sasa yupo ndani ya Klabu ya FAR Rabat ya Morroco.



Comments

Popular posts from this blog

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

KOCHA BIASHARA UNITED: WACHEZAJI NIMEWAPA KAZI YA KUPAMBANA NA JEZI YA NJANO

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI