JOSE MOURINHO:KUKASIRIKA KWA WACHEZAJI KAWAIDA WAKIFUNGWA


JOSE Mourinho, Kocha Mkuu wa Klabu ya Tottenham amesema kuwa kitendo cha wachezaji wake kukasirika ndani ya vyumba vya kubadilishia nguo ni jambo la kawaida kutokea hasa pale ambapo timu inakuwa imefungwa.

Januari 28, Mourinho alikiongoza kikosi chake kwenye mchezo wa Ligi Kuu England dhidi ya Liverpool na kukubali kupoteza kwa kufungwa mabao 3-1.

Habari zimeeleza kuwa wakati wa mapumziko wachezaji walikuwa wakilaumiana huku zigo kubwa la lawama akipewa beki Serge Aurier kwa kuwa alishindwa kuongeza uimara kwenye safu ya ulinzi dakika za mwisho kabla ya mapumziko na kuruhusu Liverpool kupata bao la kuongoza.

Roberto Firmino alifunga bao hilo la kwanza kwa Liverpool akiwa chini ya uangalizi wa Aurier na Eric Dier ambao walikuwa kwenye safu ya ulinzi.

Mourinho aliamua kumfanyia mabadiliko Aurier ambaye alikasirika na anatajwa kusepa uwanjani wakati wachezaji wenzanke wakiingia kumalizia dakika 45 za kipindi cha pili na waliokota nyavuni mabao mengine mawili.

Pia inaelezwa kuwa nyota huyo inaweza kuwa ngumu kwake kubaki ndani ya kikosi hicho kwa kuwa amebakiza dili la miezi 18 kumaliza mkataba wake ndani ya timu hiyo.

 Jose Mourinho kuhusu kumtoa beki huyo amesema:-"Ulikuwa ni wakati mgumu na hali ambayo walikuwa nayo wachezaji na ilikuwa ni ngumu kuweza kukubali suala la kupoteza.

"Ni ngumu kukubali asili hasa ya kufungwa mabao ila huwezi kuzuia namna ambavyo inatokea ndani ya uwanja hasa pale ambapo unapata nafasi ndani ya dakika moja. Ni kweli ni hali ya wachezaji hawakuwa na furaha hivyo ni jambo la kawaida," .



Comments

Popular posts from this blog

SIMBA NA YANGA MSIBEBE MATOKEO UWANJANI

FT: VPL:SIMBA 4-0 IHEFU

WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA