WAMEANZA NA MAJANGA MSIMU MPYA WA 2021/22, SIMBA WANAWEZA KUKOSA UBINGWA
IKIWA Simba watakuwa kwenye mwendo huu ndani ya msimu wa 2021/22 kengele ya hatari inawaka kwenye kichwa cha Kocha Mkuu, Didier Gomes kwa kuwa kutakuwa na hatihati ya kuachia ubingwa kwa wapinzani wao pamoja na kushindwa kufurukuta kwenye mechi za kimataifa. Hili linakuja kutokana na rekodi kuonyesha kwamba wachezaji wake wengi muhimu wamekuwa wakikutana na minyoosho ya maana huku Gomes akikiri kwamba ligi ni ngumu na ushindani ni mkubwa. Iliwatokea Liverpool ya Ulaya msimu uliopita baada ya kuwakosa nyota wake muhimu kutokana na kupatwa minyoosho uwanjani miongoni mwao alikuwa ni beki kisiki Virgil van Djik ambaye aligongwa na alikaa nje msimu mzima wa 2020/21 na timu yake ikapoteza ubingwa. Hapa Championi Jumatatu inakuletea orodha ya wachezaji walioanza na majanga 2021/22 huku Simba ikiwa ni namba moja kwa timu yenye wachezaji wengi wenye majanga:- Joash Onyango Beki kisiki wa Simba hana bahati na mechi kubwa kwa kuwa aliwahi kupata maumivu kwenye mchezo dhidi...