KIPA MPYA SIMBA MAMBO BADO


DIDIER Gomes, Kocha Mkuu wa Simba amesema kuwa kipa wake Jeremia Kisubi bado anahitaji muda ili kuweza kufanya vizuri.

Kisubi kwa sasa yupo ndani ya kikosi hicho ambacho kinafanya maandalizi ya mwisho kuelekea kwenye mchezo wa Ligi ya Mabingwa Afrika dhidi ya Jwaneng Galaxy ya Botswana.

Gomes amesema anatambua uwezo wa nyota huyo na amekuwa akifanya vizuri kwenye mazoezi lakini bado kuweza kuanza katika kikosi cha kwanza kwa kuwa hajawa imara.

"Kisubi ni kipa mzuri lakini bado hajawa imara kwa sasa kwa sababu alikuwa anaumwa kwa muda mefu na wakati huu anaendelea na mazoezi.

"Jambo ambalo linasubiriwa kwake ni kuwa katika hali yake ya kawaida na hiyo itafanya tuwe na chaguo kubwa kwenye upande wa makipa,".



Comments

Popular posts from this blog

ISHU YA MORRISON KUHUSU MKATABA WAKE IPO MIKONONI MWA KAMATI YA SHERIA NA HADHI ZA WACHEZAJI

BREAKING: MASHABIKI RUKSA KWENDA UWANJANI, UTARATIBU WATAJWA

AFRICAN LYON WADAI KUWA WAZO LA VISIT TANZANIA NA LOGO MPYA YA SIMBA IMETOKA KWAO